요한복음 7장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 요한복음 (John) · 53절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Baada ya hayo, Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya. Hakutaka kutembea mkoani Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wanataka kumwua. | After these things Jesus walked in Galilee: for he would not walk in Jewry, because the Jews sought to kill him. |
| 2 | Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. | Now the Jews’ feast of tabernacles was at hand. |
| 3 | Basi ndugu zake wakamwambia, "Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya. | His brethren therefore said unto him, Depart hence, and go into Judea, that thy disciples also may see the works that thou doest. |
| 4 | Mtu hafanyi mambo kwa siri kama anataka kujulikana kwa watu. Maadam unafanya mambo haya, basi, jidhihirishe kwa ulimwengu." | For there is no man that doeth any thing in secret, and he himself seeketh to be known openly. If thou do these things, shew thyself to the world. |
| 5 | (Hata ndugu zake hawakumwamini!) | For neither did his brethren believe in him. |
| 6 | Basi, Yesu akawaambia, "Wakati wangu ufaao haujafika bado. Lakini kwenu ninyi kila wakati unafaa. | Then Jesus said unto them, My time is not yet come: but your time is alway ready. |
| 7 | Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini mimi wanichukia kwa sababu mimi nauambia wazi kwamba matendo yake ni maovu. | The world cannot hate you; but me it hateth, because I testify of it, that the works thereof are evil. |
| 8 | Ninyi nendeni kwenye sikukuu hiyo. Mimi siendi kwenye sikukuu hiyo, maana saa yangu ifaayo haijafika." | Go ye up unto this feast: I go not up yet unto this feast; for my time is not yet full come. |
| 9 | Alisema hayo kisha akabaki huko Galilaya. | When he had said these words unto them, he abode still in Galilee. |
| 10 | Baada ya ndugu zake kwenda kwenye sikukuu, Yesu naye alikwenda, lakini hakuenda kwa hadhara bali kwa siri. | But when his brethren were gone up, then went he also up unto the feast, not openly, but as it were in secret. |
| 11 | Viongozi wa Wayahudi walikuwa wanamtafuta kwenye sikukuu hiyo; Wakauliza: "Yuko wapi?" | Then the Jews sought him at the feast, and said, Where is he? |
| 12 | Kulikuwa na minong'ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, "Ni mtu mwema." Wengine walisema, "La! Anawapotosha watu." | And there was much murmuring among the people concerning him: for some said, He is a good man: others said, Nay; but he deceiveth the people. |
| 13 | Hata hivyo hakuna mtu aliyethubutu kusema, habari zake hadharani kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. | Howbeit no man spake openly of him for fear of the Jews. |
| 14 | Sikukuu hiyo ilipofikia katikati, Yesu naye alikwenda Hekaluni, akaanza kufundisha. | Now about the midst of the feast Jesus went up into the temple, and taught. |
| 15 | Basi, Wayahudi wakashangaa na kusema "Mtu huyu amepataje elimu naye hakusoma shuleni?" | And the Jews marvelled, saying, How knoweth this man letters, having never learned? |
| 16 | Hapo Yesu akawajibu, "Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma. | Jesus answered them, and said, My doctrine is not mine, but his that sent me. |
| 17 | Mtu anayependa kufanya yale anayotaka Mungu, atajua kama mafundisho yangu yametoka kwa Mungu, au mimi najisemea tu mwenyewe. | If any man will do his will, he shall know of the doctrine, whether it be of God, or whether I speak of myself. |
| 18 | Yeye anayejisemea tu mwenyewe anatafuta sifa yake mwenyewe; lakini anayetafuta sifa ya yule aliyemtuma, huyo ni mwaminifu, na ndani yake hamna uovu wowote. | He that speaketh of himself seeketh his own glory: but he that seeketh his glory that sent him, the same is true, and no unrighteousness is in him. |
| 19 | Je, Mose hakuwapeni Sheria? Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishika Sheria. Kwa nini mnataka kuniua?" | Did not Moses give you the law, and yet none of you keepeth the law? Why go ye about to kill me? |
| 20 | Hapo watu wakamjibu, "Una wazimu wewe! Nani anataka kukuua?" | The people answered and said, Thou hast a devil: who goeth about to kill thee? |
| 21 | Yesu akawajibu, "Kuna jambo moja nililofanya, nanyi mnalistaajabia. | Jesus answered and said unto them, I have done one work, and ye all marvel. |
| 22 | Mose aliwapeni ile desturi ya kutahiri. (Si kwamba desturi hiyo ilitoka kwa Mose, bali ilitoka kwa mababu). Sasa ninyi humtahiri mtu hata siku ya Sabato. | Moses therefore gave unto you circumcision; (not because it is of Moses, but of the fathers;) and ye on the sabbath day circumcise a man. |
| 23 | Ikiwa basi, mtu hutahiriwa hata siku ya Sabato kusudi Sheria ya Mose isivunjwe, mbona mnanikasirikia kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya Sabato? | If a man on the sabbath day receive circumcision, that the law of Moses should not be broken; are ye angry at me, because I have made a man every whit whole on the sabbath day? |
| 24 | Msihukumu mambo kwa nje tu; toeni hukumu ya haki." | Judge not according to the appearance, but judge righteous judgment. |
| 25 | Baadhi ya watu wa Yerusalemu walisema, "Je, yule mtu wanayemtafuta wamuue si huyu? | Then said some of them of Jerusalem, Is not this he, whom they seek to kill? |
| 26 | Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo? | But, lo, he speaketh boldly, and they say nothing unto him. Do the rulers know indeed that this is the very Christ? |
| 27 | Kristo atakapokuja hakuna mtu atakayejua mahali alikotoka, lakini sisi tunajua alikotoka mtu huyu!" | Howbeit we know this man whence he is: but when Christ cometh, no man knoweth whence he is. |
| 28 | Basi, Yesu alipokuwa anafundisha Hekaluni alipaaza sauti na kusema, "Ati mnanijua; hata nilikotoka mnakujua! Hata hivyo, sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe; ila yeye aliyenituma mimi ni wa kweli, nanyi hamumjui. | Then cried Jesus in the temple as he taught, saying, Ye both know me, and ye know whence I am: and I am not come of myself, but he that sent me is true, whom ye know not. |
| 29 | Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma." | But I know him: for I am from him, and he hath sent me. |
| 30 | Basi, watu wakataka kumtia nguvuni, lakini hakuna mtu aliyethubutu kumkamata kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado. | Then they sought to take him: but no man laid hands on him, because his hour was not yet come. |
| 31 | Wengi katika ule umati wa watu walimwamini, wakasema, "Je, Kristo akija atafanya ishara kubwa zaidi kuliko alizozifanya huyu?" | And many of the people believed on him, and said, When Christ cometh, will he do more miracles than these which this man hath done? |
| 32 | Mafarisayo waliwasikia watu wakinong'ona maneno hayo juu ya Yesu. Basi, wao pamoja na makuhani wakuu wakawatuma walinzi wamtie nguvuni. | The Pharisees heard that the people murmured such things concerning him; and the Pharisees and the chief priests sent officers to take him. |
| 33 | Yesu akasema, "Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma. | Then said Jesus unto them, Yet a little while am I with you, and then I go unto him that sent me. |
| 34 | Mtanitafuta lakini hamtaniona, maana pale nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika." | Ye shall seek me, and shall not find me: and where I am, thither ye cannot come. |
| 35 | Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, "Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki? | Then said the Jews among themselves, Whither will he go, that we shall not find him? will he go unto the dispersed among the Gentiles, and teach the Gentiles? |
| 36 | Ana maana gani anaposema: Mtanitafuta lakini hamtanipata, na mahali nitakapokuwa ninyi hamwezi kufika?" | What manner of saying is this that he said, Ye shall seek me, and shall not find me: and where I am, thither ye cannot come? |
| 37 | Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalum. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, "Aliye na kiu na aje kwangu anywe. | In the last day, that great day of the feast, Jesus stood and cried, saying, If any man thirst, let him come unto me, and drink. |
| 38 | Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: Anayeniamini mimi, mito ya maji yenye uzima itatiririka kutoka moyoni mwake!" | He that believeth on me, as the scripture hath said, out of his belly shall flow rivers of living water. |
| 39 | (Alisema hayo kumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watampokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.) | (But this spake he of the Spirit, which they that believe on him should receive: for the Holy Ghost was not yet given; because that Jesus was not yet glorified.) |
| 40 | Baadhi ya watu katika ule umati walisikia maneno hayo, wakasema, "Kweli mtu huyu ndiye yule nabii!" | Many of the people therefore, when they heard this saying, said, Of a truth this is the Prophet. |
| 41 | Wengine wakasema, "Huyu ndiye Kristo!" Lakini wengine walisema, "Je, yawezekana Kristo akatoka Galilaya? | Others said, This is the Christ. But some said, Shall Christ come out of Galilee? |
| 42 | Maandiko Matakatifu yasemaje? Yanasema: Kristo atatoka katika ukoo wa Daudi, na atazaliwa Bethlehemu, mji wa Daudi!" | Hath not the scripture said, That Christ cometh of the seed of David, and out of the town of Bethlehem, where David was? |
| 43 | Basi, kukatokea mafarakano juu yake katika ule umati wa watu. | So there was a division among the people because of him. |
| 44 | Baadhi ya watu walitaka kumtia nguvuni lakini hakuna aliyejaribu kumkamata. | And some of them would have taken him; but no man laid hands on him. |
| 45 | Kisha wale walinzi wakarudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo; nao wakawauliza, "Kwa nini hamkumleta?" | Then came the officers to the chief priests and Pharisees; and they said unto them, Why have ye not brought him? |
| 46 | Walinzi wakawajibu, "Hakuna mtu aliyepata kamwe kusema kama asemavyo mtu huyu!" | The officers answered, Never man spake like this man. |
| 47 | Mafarisayo wakawauliza, "Je, nanyi pia mmedanganyika? | Then answered them the Pharisees, Are ye also deceived? |
| 48 | Je, mmekwisha mwona hata mmoja wa viongozi wa watu, au mmoja wa Mafarisayo aliyemwamini? | Have any of the rulers or of the Pharisees believed on him? |
| 49 | Lakini umati huu haujui Sheria ya Mose; umelaaniwa!" | But this people who knoweth not the law are cursed. |
| 50 | Mmoja wao alikuwa Nikodemo ambaye hapo awali alikuwa amemwendea Yesu. Basi, yeye akawaambia, | Nicodemus saith unto them, (he that came to Jesus by night, being one of them,) |
| 51 | "Je, Sheria yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza na kujua anafanya nini?" | Doth our law judge any man, before it hear him, and know what he doeth? |
| 52 | Nao wakamjibu, "Je, wewe pia umetoka Galilaya? Haya, kayachunguze Maandiko Matakatifu nawe utaona kwamba Galilaya hakutoki kamwe nabii!" | They answered and said unto him, Art thou also of Galilee? Search, and look: for out of Galilee ariseth no prophet. |
| 53 | Basi, wote wakaondoka, kila mtu akaenda zake; | And every man went unto his own house. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL