요한복음 8장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 요한복음 (John) · 59절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | lakini Yesu akaenda kwenye mlima wa Mizeituni. | Jesus went unto the mount of Olives. |
| 2 | Kesho yake asubuhi na mapema alikwenda tena Hekaluni. Watu wote wakamwendea, naye akaketi akawa anawafundisha. | And early in the morning he came again into the temple, and all the people came unto him; and he sat down, and taught them. |
| 3 | Basi, walimu wa Sheria na Mafarisayo wakamletea mwanamke mmoja aliyefumaniwa katika uzinzi. Wakamsimamisha katikati yao. | And the scribes and Pharisees brought unto him a woman taken in adultery; and when they had set her in the midst, |
| 4 | Kisha wakamwuliza Yesu, "Mwalimu! Mwanamke huyu alifumaniwa katika uzinzi. | They say unto him, Master, this woman was taken in adultery, in the very act. |
| 5 | Katika Sheria yetu Mose alituamuru mwanamke kama huyu apigwe mawe. Basi, wewe wasemaje?" | Now Moses in the law commanded us, that such should be stoned: but what sayest thou? |
| 6 | Walisema hivyo kumjaribu, wapate kisa cha kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini, akaandika ardhini kwa kidole. | This they said, tempting him, that they might have to accuse him. But Jesus stooped down, and with his finger wrote on the ground, as though he heard them not. |
| 7 | Walipozidi kumwuliza, Yesu akainuka, akawaambia, "Mtu asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza kumpiga jiwe." | So when they continued asking him, he lifted up himself, and said unto them, He that is without sin among you, let him first cast a stone at her. |
| 8 | Kisha akainama tena, akawa anaandika ardhini. | And again he stooped down, and wrote on the ground. |
| 9 | Waliposikia hivyo, wakaanza kutoweka mmojammoja, wakitanguliwa na wazee. Yesu akabaki peke yake, na yule mwanamke amesimama palepale. | And they which heard it, being convicted by their own conscience, went out one by one, beginning at the eldest, even unto the last: and Jesus was left alone, and the woman standing in the midst. |
| 10 | Yesu alipoinuka akamwuliza huyo mwanamke, "Wako wapi wale watu? Je, hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?" | When Jesus had lifted up himself, and saw none but the woman, he said unto her, Woman, where are those thine accusers? hath no man condemned thee? |
| 11 | Huyo mwanamke akamjibu, "Mheshimiwa, hakuna hata mmoja!" Naye Yesu akamwambia, "Wala mimi sikuhukumu. Nenda zako; na tangu sasa usitende dhambi tena." | She said, No man, Lord. And Jesus said unto her, Neither do I condemn thee: go, and sin no more. |
| 12 | Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, "Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uzima." | Then spake Jesus again unto them, saying, I am the light of the world: he that followeth me shall not walk in darkness, but shall have the light of life. |
| 13 | Basi, Mafarisayo wakamwambia, "Wewe unajishuhudia mwenyewe; kwa hiyo ushahidi wako si halali." | The Pharisees therefore said unto him, Thou bearest record of thyself; thy record is not true. |
| 14 | Yesu akawajibu, "Hata kama ninajishuhudia mwenyewe, ushahidi wangu ni wa kweli kwa sababu mimi najua nilikotoka na ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda. | Jesus answered and said unto them, Though I bear record of myself, yet my record is true: for I know whence I came, and whither I go; but ye cannot tell whence I come, and whither I go. |
| 15 | Ninyi mnahukumu kwa fikira za kibinadamu, lakini mimi simhukumu mtu. | Ye judge after the flesh; I judge no man. |
| 16 | Hata nikihukumu, hukumu yangu ni ya haki kwa sababu mimi siko peke yangu; Baba aliyenituma yuko pamoja nami. | And yet if I judge, my judgment is true: for I am not alone, but I and the Father that sent me. |
| 17 | Imeandikwa katika Sheria yenu ya kwamba ushahidi wa watu wawili ni halali. | It is also written in your law, that the testimony of two men is true. |
| 18 | Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma, ananishuhudia pia." | I am one that bear witness of myself, and the Father that sent me beareth witness of me. |
| 19 | Hapo wakamwuliza, "Baba yako yuko wapi?" Yesu akawajibu "Ninyi hamnijui mimi wala hamumjui Baba. Kama mngenijua mimi, mngemjua na Baba yangu pia." | Then said they unto him, Where is thy Father? Jesus answered, Ye neither know me, nor my Father: if ye had known me, ye should have known my Father also. |
| 20 | Yesu alisema maneno hayo kwenye chumba cha hazina alipokuwa anafundisha Hekaluni. Wala hakuna mtu aliyemtia nguvuni, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika bado. | These words spake Jesus in the treasury, as he taught in the temple: and no man laid hands on him; for his hour was not yet come. |
| 21 | Yesu akawaambia tena, "Naenda zangu nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kufika." | Then said Jesus again unto them, I go my way, and ye shall seek me, and shall die in your sins: whither I go, ye cannot come. |
| 22 | Basi, viongozi wa Wayahudi wakasema, "Je, atajiua? Mbona anasema: Niendako ninyi hamwezi kufika?" | Then said the Jews, Will he kill himself? because he saith, Whither I go, ye cannot come. |
| 23 | Yesu akawaambia, "Ninyi mmetoka papa hapa chini, mimi nimetoka juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu. | And he said unto them, Ye are from beneath; I am from above: ye are of this world; I am not of this world. |
| 24 | Ndiyo maana niliwaambieni mtakufa katika dhambi zenu. Kama msipoamini kwamba Mimi ndimi, mtakufa katika dhambi zenu." | I said therefore unto you, that ye shall die in your sins: for if ye believe not that I am he, ye shall die in your sins. |
| 25 | Nao wakamwuliza, "Wewe ni nani?" Yesu akawajibu, "Nimewaambieni tangu mwanzo! | Then said they unto him, Who art thou? And Jesus saith unto them, Even the same that I said unto you from the beginning. |
| 26 | Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu. Lakini yule aliyenituma ni kweli; nami nauambia ulimwengu mambo yale tu niliyoyasikia kutoka kwake." | I have many things to say and to judge of you: but he that sent me is true; and I speak to the world those things which I have heard of him. |
| 27 | Hawakuelewa kwamba Yesu alikuwa akisema nao juu ya Baba. | They understood not that he spake to them of the Father. |
| 28 | Basi, Yesu akawaambia, "Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu hapo ndipo mtakapojua kwamba Mimi ndimi, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha. | Then said Jesus unto them, When ye have lifted up the Son of man, then shall ye know that I am he, and that I do nothing of myself; but as my Father hath taught me, I speak these things. |
| 29 | Yule aliyenituma yuko pamoja nami; yeye hakuniacha peke yangu kwani nafanya daima yale yanayompendeza." | And he that sent me is with me: the Father hath not left me alone; for I do always those things that please him. |
| 30 | Baada ya kusema hayo watu wengi walimwamini. | As he spake these words, many believed on him. |
| 31 | Basi, Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, "Kama mkiyazingatia mafundisho yangu mtakuwa kweli wanafunzi wangu. | Then said Jesus to those Jews which believed on him, If ye continue in my word, then are ye my disciples indeed; |
| 32 | Mtaujua ukweli, nao ukweli utawapeni uhuru." | And ye shall know the truth, and the truth shall make you free. |
| 33 | Nao wakamjibu, "Sisi ni wazawa wa Abrahamu, na hatujapata kamwe kuwa watumwa wa mtu yeyote yule. Una maana gani unaposema: mtakuwa huru?" | They answered him, We be Abraham’s seed, and were never in bondage to any man: how sayest thou, Ye shall be made free? |
| 34 | Yesu akawajibu, "Kweli nawaambieni, kila mtu anayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi. | Jesus answered them, Verily, verily, I say unto you, Whosoever committeth sin is the servant of sin. |
| 35 | Mtumwa hana makao ya kudumu nyumbani, lakini mwana anayo makao ya kudumu. | And the servant abideth not in the house for ever: but the Son abideth ever. |
| 36 | Kama mwana akiwapeni uhuru mtakuwa huru kweli. | If the Son therefore shall make you free, ye shall be free indeed. |
| 37 | Najua kwamba ninyi ni wazawa wa Abrahamu. Hata hivyo, mnataka kuniua kwa sababu hamuyakubali mafundisho yangu. | I know that ye are Abraham’s seed; but ye seek to kill me, because my word hath no place in you. |
| 38 | Mimi nasema yale aliyonionyesha Baba, lakini ninyi mwafanya yale aliyowaambieni baba yenu." | I speak that which I have seen with my Father: and ye do that which ye have seen with your father. |
| 39 | Wao wakamjibu, "Baba yetu ni Abrahamu!" Yesu akawaambia, "Kama ninyi mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngefanya kama alivyofanya Abrahamu, | They answered and said unto him, Abraham is our father. Jesus saith unto them, If ye were Abraham’s children, ye would do the works of Abraham. |
| 40 | Mimi nimewaambieni ukweli niliousikia kwa Mungu; hata hivyo, ninyi mwataka kuniua. Abrahamu hakufanya hivyo! | But now ye seek to kill me, a man that hath told you the truth, which I have heard of God: this did not Abraham. |
| 41 | Ninyi mnafanya mambo yaleyale aliyofanya babu yenu." Wao wakamwambia, "Sisi si watoto haramu! Tunaye baba mmoja tu, yaani Mungu." | Ye do the deeds of your father. Then said they to him, We be not born of fornication; we have one Father, even God. |
| 42 | Yesu akawaambia, "Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi, maana mimi nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa mamlaka yangu mwenyewe, ila yeye alinituma. | Jesus said unto them, If God were your Father, ye would love me: for I proceeded forth and came from God; neither came I of myself, but he sent me. |
| 43 | Kwa nini hamwelewi hayo ninayosema? Ni kwa kuwa hamwezi kuusikiliza ujumbe wangu. | Why do ye not understand my speech? even because ye cannot hear my word. |
| 44 | Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi na mnataka tu kutekeleza tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo; hana msimamo katika ukweli, kwani ukweli haumo ndani yake. Kila asemapo uongo, husema kutokana na hali yake ya maumbile, maana yeye ni mwongo na baba wa uongo. | Ye are of your father the devil, and the lusts of your father ye will do. He was a murderer from the beginning, and abode not in the truth, because there is no truth in him. When he speaketh a lie, he speaketh of his own: for he is a liar, and the father of it. |
| 45 | Mimi nasema ukweli, na ndiyo maana ninyi hamniamini. | And because I tell you the truth, ye believe me not. |
| 46 | Nani kati yenu awezaye kuthibitisha kuwa mimi nina dhambi? Ikiwa basi nasema ukweli, kwa nini hamniamini? | Which of you convinceth me of sin? And if I say the truth, why do ye not believe me? |
| 47 | Aliye wa Mungu husikiliza maneno ya Mungu. Lakini ninyi hamsikilizi kwa sababu ninyi si (watu wa) Mungu." | He that is of God heareth God’s words: ye therefore hear them not, because ye are not of God. |
| 48 | Wayahudi wakamwambia, "Je, hatukusema kweli kwamba wewe ni Msamaria, na tena una pepo?" | Then answered the Jews, and said unto him, Say we not well that thou art a Samaritan, and hast a devil? |
| 49 | Yesu akajibu, "Mimi sina pepo; mimi namheshimu Baba yangu, lakini ninyi hamniheshimu. | Jesus answered, I have not a devil; but I honour my Father, and ye do dishonour me. |
| 50 | Mimi sijitafutii utukufu wangu mwenyewe; yuko mmoja mwenye kuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu. | And I seek not mine own glory: there is one that seeketh and judgeth. |
| 51 | Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele." | Verily, verily, I say unto you, If a man keep my saying, he shall never see death. |
| 52 | Basi, Wayahudi wakasema, "Sasa tunajua kweli kwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele! | Then said the Jews unto him, Now we know that thou hast a devil. Abraham is dead, and the prophets; and thou sayest, If a man keep my saying, he shall never taste of death. |
| 53 | Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?" | Art thou greater than our father Abraham, which is dead? and the prophets are dead: whom makest thou thyself? |
| 54 | Yesu akawajibu, "Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu. Baba yangu ambaye ninyi mwasema ni Baba yenu, ndiye anayenitukuza. | Jesus answered, If I honour myself, my honour is nothing: it is my Father that honoureth me; of whom ye say, that he is your God: |
| 55 | Ninyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika neno lake. | Yet ye have not known him; but I know him: and if I should say, I know him not, I shall be a liar like unto you: but I know him, and keep his saying. |
| 56 | Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi." | Your father Abraham rejoiced to see my day: and he saw it, and was glad. |
| 57 | Basi, Wayahudi wakamwambia, "Wewe hujatimiza miaka hamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?" | Then said the Jews unto him, Thou art not yet fifty years old, and hast thou seen Abraham? |
| 58 | Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko." | Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was, I am. |
| 59 | Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka Hekaluni. | Then took they up stones to cast at him: but Jesus hid himself, and went out of the temple, going through the midst of them, and so passed by. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL