디모데후서 3장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 디모데후서 (2 Timothy) · 17절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Kumbuka kwamba, katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. | This know also, that in the last days perilous times shall come. |
| 2 | watu watakuwa na ubinafsi, wenye tamaa ya fedha, wenye majivuno, wenye kujiona, wenye kumtukana Mungu, wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani na waovu; | For men shall be lovers of their own selves, covetous, boasters, proud, blasphemers, disobedient to parents, unthankful, unholy, |
| 3 | watatokea watu wasio na upendo moyoni, wasio na huruma, wachongezi, walafi na wakali; watachukia chochote kilicho chema; | Without natural affection, trucebreakers, false accusers, incontinent, fierce, despisers of those that are good, |
| 4 | watakuwa wahaini, wakaidi na waliojaa kiburi; watapenda anasa kuliko kumpenda Mungu. | Traitors, heady, highminded, lovers of pleasures more than lovers of God; |
| 5 | Kwa nje wataonekana kama watu wenye kumcha Mungu, lakini wataikana nguvu yake. Jiepushe kabisa na watu wa namna hiyo. | Having a form of godliness, but denying the power thereof: from such turn away. |
| 6 | Baadhi yao huenda katika nyumba za watu na huwateka wanawake dhaifu waliolemewa mizigo ya dhambi na ambao wanaongozwa na tamaa za kila aina; | For of this sort are they which creep into houses, and lead captive silly women laden with sins, led away with divers lusts, |
| 7 | wanawake ambao wanajaribu daima kujifunza lakini hawawezi kuufikia ujuzi wa huo ukweli. | Ever learning, and never able to come to the knowledge of the truth. |
| 8 | Watu hao huupinga ukweli kama vile Yane na Yambre walivyompinga Mose. | Now as Jannes and Jambres withstood Moses, so do these also resist the truth: men of corrupt minds, reprobate concerning the faith. |
| 9 | Lakini hawataweza kuendelea zaidi kwa maana upumbavu wao utaonekana wazi kwa wote. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Yane na Yambre. | But they shall proceed no further: for their folly shall be manifest unto all men, as theirs also was. |
| 10 | Wewe lakini, umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu katika maisha, imani yangu, uvumilivu wangu, upendo wangu, subira yangu, | But thou hast fully known my doctrine, manner of life, purpose, faith, longsuffering, charity, patience, |
| 11 | udhalimu na mateso yangu. Unayajua mambo yaliyonipata huko Antiokia, Ikonio na Lustra. Nilivumilia udhalimu mkubwa mno! Lakini Bwana aliniokoa katika mambo hayo yote. | Persecutions, afflictions, which came unto me at Antioch, at Iconium, at Lystra; what persecutions I endured: but out of them all the Lord delivered me. |
| 12 | Kila mtu anayetaka kuishi maisha ya kumcha Mungu katika kuungana na Kristo Yesu lazima adhulumiwe. | Yea, and all that will live godly in Christ Jesus shall suffer persecution. |
| 13 | Watu waovu na wadanyanyifu watazidi kuwa waovu zaidi na zaidi kwa kuwadanganya wengine na kudanganyika wao wenyewe. | But evil men and seducers shall wax worse and worse, deceiving, and being deceived. |
| 14 | Lakini wewe dumu katika ukweli ule uliofundishwa, ukaukubali kabisa. Unawajua wale waliokuwa walimu wako. | But continue thou in the things which thou hast learned and hast been assured of, knowing of whom thou hast learned them; |
| 15 | Unakumbuka kwamba tangu utoto wako umeyajua Maandiko Matakatifu ambayo yaweza kukupatia hekima iletayo wokovu kwa njia ya imani kwa Kristo Yesu. | And that from a child thou hast known the holy scriptures, which are able to make thee wise unto salvation through faith which is in Christ Jesus. |
| 16 | Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundishia ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili, | All scripture is given by inspiration of God, and is profitable for doctrine, for reproof, for correction, for instruction in righteousness: |
| 17 | ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila tendo jema. | That the man of God may be perfect, throughly furnished unto all good works. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL