로그인

디모데후서 4장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 디모데후서 (2 Timothy) · 22절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme: I charge thee therefore before God, and the Lord Jesus Christ, who shall judge the quick and the dead at his appearing and his kingdom;
2 hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote. Preach the word; be instant in season, out of season; reprove, rebuke, exhort with all longsuffering and doctrine.
3 Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia. For the time will come when they will not endure sound doctrine; but after their own lusts shall they heap to themselves teachers, having itching ears;
4 Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. And they shall turn away their ears from the truth, and shall be turned unto fables.
5 Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako. But watch thou in all things, endure afflictions, do the work of an evangelist, make full proof of thy ministry.
6 Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa dhabihu na wakati wa kufariki kwangu umefika. For I am now ready to be offered, and the time of my departure is at hand.
7 Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza. I have fought a good fight, I have finished my course, I have kept the faith:
8 Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake. Henceforth there is laid up for me a crown of righteousness, which the Lord, the righteous judge, shall give me at that day: and not to me only, but unto all them also that love his appearing.
9 Fanya bidii kuja kwangu karibuni. Do thy diligence to come shortly unto me:
10 Dema ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia. For Demas hath forsaken me, having loved this present world, and is departed unto Thessalonica; Crescens to Galatia, Titus unto Dalmatia.
11 Luka peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko uje naye, kwa maana ataweza kunisaidia katika kazi yangu. Only Luke is with me. Take Mark, and bring him with thee: for he is profitable to me for the ministry.
12 Nilimtuma Tukiko kule Efeso. And Tychicus have I sent to Ephesus.
13 Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo kule Troa; niletee pia vile vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwa kwa ngozi. The cloke that I left at Troas with Carpus, when thou comest, bring with thee, and the books, but especially the parchments.
14 Yule sonara aitwaye Aleksanda amenitendea maovu mengi; Bwana atamlipa kufuatana na hayo matendo yake. Alexander the coppersmith did me much evil: the Lord reward him according to his works:
15 Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali. Of whom be thou ware also; for he hath greatly withstood our words.
16 Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo! At my first answer no man stood with me, but all men forsook me: I pray God that it may not be laid to their charge.
17 Lakini, Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba. Notwithstanding the Lord stood with me, and strengthened me; that by me the preaching might be fully known, and that all the Gentiles might hear: and I was delivered out of the mouth of the lion.
18 Bwana ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka katika Utawala wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele! Amina. And the Lord shall deliver me from every evil work, and will preserve me unto his heavenly kingdom: to whom be glory for ever and ever. Amen.
19 Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo. Salute Prisca and Aquila, and the household of Onesiphorus.
20 Erasto alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwacha Mileto kwa sababu alikuwa mgonjwa. Erastus abode at Corinth: but Trophimus have I left at Miletum sick.
21 Fanya bidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo, Pude, Lino na Klaudia wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote. Do thy diligence to come before winter. Eubulus greeteth thee, and Pudens, and Linus, and Claudia, and all the brethren.
22 Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema. The Lord Jesus Christ be with thy spirit. Grace be with you. Amen. The second epistle unto Timotheus, ordained the first bishop of the church of the Ephesians, was written from Rome, when Paul was brought before Nero the second time.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL