로그인

디모데후서 2장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 디모데후서 (2 Timothy) · 26절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvu katika neema tunayopata katika kuungana na Kristo Yesu. Thou therefore, my son, be strong in the grace that is in Christ Jesus.
2 Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha wengine pia. And the things that thou hast heard of me among many witnesses, the same commit thou to faithful men, who shall be able to teach others also.
3 Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo yesu. Thou therefore endure hardness, as a good soldier of Jesus Christ.
4 Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida ili aweze kumpendeza mkuu wa jeshi. No man that warreth entangleth himself with the affairs of this life; that he may please him who hath chosen him to be a soldier.
5 Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. And if a man also strive for masteries, yet is he not crowned, except he strive lawfully.
6 Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno. The husbandman that laboureth must be first partaker of the fruits.
7 Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uyaelewe yote. Consider what I say; and the Lord give thee understanding in all things.
8 Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri. Remember that Jesus Christ of the seed of David was raised from the dead according to my gospel:
9 Kwa sababu ya kuihubiri Habari Njema mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo, Wherein I suffer trouble, as an evil doer, even unto bonds; but the word of God is not bound.
10 na hivyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele. Therefore I endure all things for the elect’s sakes, that they may also obtain the salvation which is in Christ Jesus with eternal glory.
11 Usemi huu ni wa kweli: "Ikiwa tulikufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye. It is a faithful saying: For if we be dead with him, we shall also live with him:
12 Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana. If we suffer, we shall also reign with him: if we deny him, he also will deny us:
13 Tukikosa kuwa waaminifu, yeye hubaki mwaminifu daima, maana yeye hawezi kujikana mwenyewe." If we believe not, yet he abideth faithful: he cannot deny himself.
14 Basi, wakumbushe watu wako mambo haya, na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia. Of these things put them in remembrance, charging them before the Lord that they strive not about words to no profit, but to the subverting of the hearers.
15 Jitahidi kupata kibali kamili mbele ya Mungu kama mfanyakazi ambaye haoni haya juu ya kazi yake, na ambaye hufundisha sawa ule ujumbe wa kweli. Study to shew thyself approved unto God, a workman that needeth not to be ashamed, rightly dividing the word of truth.
16 Jiepushe na majadiliano ya kidunia na ya kipumbavu; kwani hayo huzidi kuwatenga watu mbali na Mungu. But shun profane and vain babblings: for they will increase unto more ungodliness.
17 Mafundisho ya aina hiyo ni kama donda linalokula mwili. Miongoni mwa hao waliofundisha hayo ni Humenayo na Fileto. And their word will eat as doth a canker: of whom is Hymeneus and Philetus;
18 Hawa wamepotoka kabisa mbali na ukweli, na wanatia imani ya watu wengine katika wasiwasi kwa kusema ati ufufuo wetu umekwisha fanyika. Who concerning the truth have erred, saying that the resurrection is past already; and overthrow the faith of some.
19 Lakini msingi thabiti uliowekwa na Mungu uko imara, na juu yake yameandikwa maneno haya: "Bwana anawafahamu wale walio wake," na "Kila asemaye yeye ni wa Bwana, ni lazima aachane na uovu." Nevertheless the foundation of God standeth sure, having this seal, The Lord knoweth them that are his. And, Let every one that nameth the name of Christ depart from iniquity.
20 Katika nyumba kubwa kuna mabakuli na vyombo vya kila namna: vingine ni vya fedha na dhahabu, vingine vya mbao na udongo, vingine ni vya matumizi ya pekee na vingine kwa ajili ya matumizi ya kawaida. But in a great house there are not only vessels of gold and of silver, but also of wood and of earth; and some to honour, and some to dishonour.
21 Basi, kama mtu atajitakasa kwa kujitenga mbali na mambo hayo yote maovu, atakuwa chombo cha matumizi ya pekee, kwa sababu amewekwa wakfu, anamfaa Bwana wake na yupo tayari kwa kila kazi njema. If a man therefore purge himself from these, he shall be a vessel unto honour, sanctified, and meet for the master’s use, and prepared unto every good work.
22 Jiepushe na tamaa za ujana, fuata uadilifu, imani, upendo, amani, pamoja na watu wote ambao wanamwomba Bwana kwa moyo safi. Flee also youthful lusts: but follow righteousness, faith, charity, peace, with them that call on the Lord out of a pure heart.
23 Epuka ubishi wa kijinga na kipumbavu; wajua kwamba hayo huleta magomvi. But foolish and unlearned questions avoid, knowing that they do gender strifes.
24 Mtumishi wa Bwana asigombane. Anapaswa kuwa mpole kwa watu wote, mwalimu mwema na mvumilivu, And the servant of the Lord must not strive; but be gentle unto all men, apt to teach, patient,
25 ambaye ni mpole anapowaonya wapinzani wake, kwani huenda Mungu akawajalia nafasi ya kutubu, wakapata kuujua ukweli. In meekness instructing those that oppose themselves; if God peradventure will give them repentance to the acknowledging of the truth;
26 Hapo fahamu zao zitawarudia tena, wakaponyoka katika mtego wa Ibilisi aliyewanasa na kuwafanya wayatii matakwa yake. And that they may recover themselves out of the snare of the devil, who are taken captive by him at his will.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL