누가복음 23장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 56절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Kisha, wote kwa jumla, wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato. | And the whole multitude of them arose, and led him unto Pilate. |
| 2 | Wakaanza kumshtaki wakisema: "Tulimkuta mtu huyu akiwapotosha watu wetu, akipinga kulipa kodi kwa Kaisari na kujiita ati yeye ni Kristo, Mfalme." | And they began to accuse him, saying, We found this fellow perverting the nation, and forbidding to give tribute to Cesar, saying that he himself is Christ a King. |
| 3 | Pilato akamwuliza Yesu, "Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamjibu, "Wewe umesema." | And Pilate asked him, saying, Art thou the King of the Jews? And he answered him and said, Thou sayest it. |
| 4 | Pilato akawaambia makuhani wakuu na umati wa watu, "Sioni kosa lolote katika mtu huyu." | Then said Pilate to the chief priests and to the people, I find no fault in this man. |
| 5 | Lakini wao wakasisitiza wakisema: "Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika nchi yote ya Yudea; alianza Galilaya, na sasa yuko hapa." | And they were the more fierce, saying, He stirreth up the people, teaching throughout all Jewry, beginning from Galilee to this place. |
| 6 | Pilato aliposikia hayo, akauliza, "Je, mtu huyu ni mwenyeji wa Galilaya?" | When Pilate heard of Galilee, he asked whether the man were a Galilean. |
| 7 | Alipojua kwamba Yesu alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka kwa Herode, ambaye wakati huo alikuwa Yerusalemu. | And as soon as he knew that he belonged unto Herod’s jurisdiction, he sent him to Herod, who himself also was at Jerusalem at that time. |
| 8 | Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu akitenda mwujiza. | And when Herod saw Jesus, he was exceeding glad: for he was desirous to see him of a long season, because he had heard many things of him; and he hoped to have seen some miracle done by him. |
| 9 | Basi, akamwuliza maswali mengi kwa muda mrefu, lakini Yesu hakumjibu neno. | Then he questioned with him in many words; but he answered him nothing. |
| 10 | Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakajitokeza mbele, wakatoa mashtaka yao kwa nguvu sana. | And the chief priests and scribes stood and vehemently accused him. |
| 11 | Basi, herode pamoja na maaskari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato. | And Herod with his men of war set him at nought, and mocked him, and arrayed him in a gorgeous robe, and sent him again to Pilate. |
| 12 | Herode na Pilato, ambao hapo awali walikuwa maadui, tangu siku hiyo wakawa marafiki. | And the same day Pilate and Herod were made friends together: for before they were at enmity between themselves. |
| 13 | Basi, Pilato akaitisha mkutano wa makuhani wakuu, viongozi na watu, | And Pilate, when he had called together the chief priests and the rulers and the people, |
| 14 | akawaambia, "Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake. | Said unto them, Ye have brought this man unto me, as one that perverteth the people: and, behold, I, having examined him before you, have found no fault in this man touching those things whereof ye accuse him: |
| 15 | Wala si mimi tu, bali hata Herode hakuona kosa lolote, kwa maana amemrudisha kwangu. Ni dhahiri kwamba mtu huyu hakufanya chochote kinachostahili adhabu ya kifo. | No, nor yet Herod: for I sent you to him; and, lo, nothing worthy of death is done unto him. |
| 16 | Hivyo, nitaamuru apigwe viboko, halafu nitamwachilia." | I will therefore chastise him, and release him. |
| 17 | Kila sikukuu ya Pasaka, ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja. | (For of necessity he must release one unto them at the feast.) |
| 18 | Lakini wote wakapiga kelele pamoja: "Mwondoe huyo, utufungulie Baraba!" | And they cried out all at once, saying, Away with this man, and release unto us Barabbas: |
| 19 | (Baraba alikuwa ametiwa ndani kwa kusababisha uasi katika mji na pia kwa sababu ya kuua.) | (Who for a certain sedition made in the city, and for murder, was cast into prison.) |
| 20 | Pilato alitaka kumwachilia Yesu, hivyo akasema nao tena; | Pilate therefore, willing to release Jesus, spake again to them. |
| 21 | lakini wao wakapiga kelele: "Msulubishe, msulubishe!" | But they cried, saying, Crucify him, crucify him. |
| 22 | Pilato akawaambia mara ya tatu, "Amefanya kosa gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie." | And he said unto them the third time, Why, what evil hath he done? I have found no cause of death in him: I will therefore chastise him, and let him go. |
| 23 | Lakini wao wakazidi kupiga kelele kwa nguvu sana, kwamba Yesu ni lazima asulubiwe. Mwishowe, sauti zao zikashinda. | And they were instant with loud voices, requiring that he might be crucified. And the voices of them and of the chief priests prevailed. |
| 24 | Basi, Pilato akaamua kwamba matakwa yao yatimizwe. | And Pilate gave sentence that it should be as they required. |
| 25 | Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa sababu ya uasi na kuua; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka. | And he released unto them him that for sedition and murder was cast into prison, whom they had desired; but he delivered Jesus to their will. |
| 26 | Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu. | And as they led him away, they laid hold upon one Simon, a Cyrenian, coming out of the country, and on him they laid the cross, that he might bear it after Jesus. |
| 27 | Watu, umati kwa umati, walimfuata; miongoni mwao wakiwemo wanawake waliokuwa wanaomboleza na kumlilia. | And there followed him a great company of people, and of women, which also bewailed and lamented him. |
| 28 | Yesu akawageukia, akasema, "Enyi kina mama wa Yerusalemu! Msinililie mimi, ila lieni kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya watoto wenu. | But Jesus turning unto them said, Daughters of Jerusalem, weep not for me, but weep for yourselves, and for your children. |
| 29 | Maana, hakika siku zitakuja ambapo watasema: Heri yao wale walio tasa, ambao hawakupata kuzaa wala kunyonyesha watoto! | For, behold, the days are coming, in the which they shall say, Blessed are the barren, and the wombs that never bare, and the paps which never gave suck. |
| 30 | Wakati huo, ndipo watu wataanza kuiambia milima: Tuangukieni! na vilima, Tufunikeni! | Then shall they begin to say to the mountains, Fall on us; and to the hills, Cover us. |
| 31 | Kwa maana, kama watu wanautendea mti mbichi namna hiyo, itakuwaje kwa mti mkavu?" | For if they do these things in a green tree, what shall be done in the dry? |
| 32 | Waliwachukua pia watu wengine wawili, wahalifu, wauawe pamoja naye. | And there were also two other, malefactors, led with him to be put to death. |
| 33 | Walipofika mahali paitwapo, "Fuvu la Kichwa," ndipo wakamsulubisha Yesu pamoja na wale wahalifu wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto. | And when they were come to the place, which is called Calvary, there they crucified him, and the malefactors, one on the right hand, and the other on the left. |
| 34 | Yesu akasema, "Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya." Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. | Then said Jesus, Father, forgive them; for they know not what they do. And they parted his raiment, and cast lots. |
| 35 | Watu wakawa wamesimama pale wakitazama. Nao viongozi wakamdhihaki wakisema: "Amewaokoa wengine; sasa na ajiokoe mwenyewe, kama yeye ndiye Kristo, mteule wa Mungu!" | And the people stood beholding. And the rulers also with them derided him, saying, He saved others; let him save himself, if he be Christ, the chosen of God. |
| 36 | Askari nao walimdhihaki pia; walimwendea wakampa siki | And the soldiers also mocked him, coming to him, and offering him vinegar, |
| 37 | wakisema: "Kama kweli wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe." | And saying, If thou be the king of the Jews, save thyself. |
| 38 | Vilevile maandishi haya yalikuwa yameandikwa na kuwekwa juu yake: "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi." | And a superscription also was written over him in letters of Greek, and Latin, and Hebrew, THIS IS THE KING OF THE JEWS. |
| 39 | Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: "Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia." | And one of the malefactors which were hanged railed on him, saying, If thou be Christ, save thyself and us. |
| 40 | Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: "Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo. | But the other answering rebuked him, saying, Dost not thou fear God, seeing thou art in the same condemnation? |
| 41 | Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya." | And we indeed justly; for we receive the due reward of our deeds: but this man hath done nothing amiss. |
| 42 | Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako." | And he said unto Jesus, Lord, remember me when thou comest into thy kingdom. |
| 43 | Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi." | And Jesus said unto him, Verily I say unto thee, To day shalt thou be with me in paradise. |
| 44 | Ilikuwa yapata saa sita mchana; jua likaacha kuangaza, giza likafunika nchi yote mpaka saa tisa, | And it was about the sixth hour, and there was a darkness over all the earth until the ninth hour. |
| 45 | na pazia lililokuwa limetundikwa Hekaluni likapasuka vipande viwili. | And the sun was darkened, and the veil of the temple was rent in the midst. |
| 46 | Yesu akalia kwa sauti kubwa: "Baba, naiweka roho yangu mikononi mwako." Alipokwisha sema hayo, akakata roho. | And when Jesus had cried with a loud voice, he said, Father, into thy hands I commend my spirit: and having said thus, he gave up the ghost. |
| 47 | Hapo, yule jemadari alipoona yaliyotukia akamsifu Mungu akisema: "Hakika huyu alikuwa mtu mwema." | Now when the centurion saw what was done, he glorified God, saying, Certainly this was a righteous man. |
| 48 | Watu wale wote waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya tukio hilo, walipoona hayo yaliyotukia, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni. | And all the people that came together to that sight, beholding the things which were done, smote their breasts, and returned. |
| 49 | Marafiki zake wote pamoja na wale wanawake walioandamana naye kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali kutazama tukio hilo. | And all his acquaintance, and the women that followed him from Galilee, stood afar off, beholding these things. |
| 50 | Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yosefu, mwenyeji wa kijiji kimoja cha Wayahudi kiitwacho Armathaya. Alikuwa mtu mwema anayeheshimika; | And, behold, there was a man named Joseph, a counsellor; and he was a good man, and a just: |
| 51 | Alikuwa akitazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja wa Baraza kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao. | (The same had not consented to the counsel and deed of them;) he was of Arimathea, a city of the Jews: who also himself waited for the kingdom of God. |
| 52 | Basi, yeye alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. | This man went unto Pilate, and begged the body of Jesus. |
| 53 | Kisha, akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika. | And he took it down, and wrapped it in linen, and laid it in a sepulchre that was hewn in stone, wherein never man before was laid. |
| 54 | Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza. | And that day was the preparation, and the sabbath drew on. |
| 55 | Wale wanawake walioandamana na Yesu kutoka Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa | And the women also, which came with him from Galilee, followed after, and beheld the sepulchre, and how his body was laid. |
| 56 | Halafu, walirudi nyumbani, wakatayarisha manukato na marashi kuyapaka mwili wa Yesu. Siku ya Sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria. | And they returned, and prepared spices and ointments; and rested the sabbath day according to the commandment. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL