누가복음 22장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 71절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa chachu, iitwayo Pasaka, ilikuwa inakaribia. | Now the feast of unleavened bread drew nigh, which is called the Passover. |
| 2 | Makuhani wakuu na walimu wa Sheria wakawa wanatafuta njia ya kumwua Yesu, lakini waliwaogopa watu. | And the chief priests and scribes sought how they might kill him; for they feared the people. |
| 3 | Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwae Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. | Then entered Satan into Judas surnamed Iscariot, being of the number of the twelve. |
| 4 | Yuda akaenda akajadiliana na makuhani wakuu na walinzi wa Hekalu kuhusu atakavyomsaliti Yesu kwao. | And he went his way, and communed with the chief priests and captains, how he might betray him unto them. |
| 5 | Nao wakafurahi na kupatana naye kumlipa fedha. | And they were glad, and covenanted to give him money. |
| 6 | Yuda akakubali, na akawa anatafuta nafasi nzuri ya kumkabidhi kwao bila umati wa watu kujua. | And he promised, and sought opportunity to betray him unto them in the absence of the multitude. |
| 7 | Basi, siku ya Mikate Isiyotiwa chachu ikafika. Hiyo ndiyo siku ambayo mwana kondoo wa Pasaka huchinjwa. | Then came the day of unleavened bread, when the passover must be killed. |
| 8 | Hivyo Yesu akawatuma Petro na Yohane, akawaambia, "Nendeni mkatuandalie karamu ili tupate kula Pasaka." | And he sent Peter and John, saying, Go and prepare us the passover, that we may eat. |
| 9 | Nao wakamwuliza, "Unataka tuiandae wapi?" | And they said unto him, Where wilt thou that we prepare? |
| 10 | Akawaambia, "Sikilizeni! Mtakapokuwa mnakwenda mjini, mtakutana na mwanamume anayebeba mtungi wa maji. Mfuateni mpaka ndani ya nyumba atakayoingia. | And he said unto them, Behold, when ye are entered into the city, there shall a man meet you, bearing a pitcher of water; follow him into the house where he entereth in. |
| 11 | Mwambieni mwenye nyumba: Mwalimu anakuuliza, kiko wapi kile chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu? | And ye shall say unto the goodman of the house, The Master saith unto thee, Where is the guestchamber, where I shall eat the passover with my disciples? |
| 12 | Naye atawaonyesheni chumba kikubwa ghorofani ambacho kimepambwa. Andalieni humo." | And he shall shew you a large upper room furnished: there make ready. |
| 13 | Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu sawa kama Yesu alivyokuwa amewaambia; wakaandaa karamu ya Pasaka. | And they went, and found as he had said unto them: and they made ready the passover. |
| 14 | Saa ilipotimia, Yesu akakaa kula chakula pamoja na mitume wake. | And when the hour was come, he sat down, and the twelve apostles with him. |
| 15 | Akawaambia, "Nimetamani sana kula Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. | And he said unto them, With desire I have desired to eat this passover with you before I suffer: |
| 16 | Maana nawaambieni, sitaila tena hadi hapo itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu." | For I say unto you, I will not any more eat thereof, until it be fulfilled in the kingdom of God. |
| 17 | Kisha akatwaa kikombe, akashukuru akasema, "Pokeeni, mgawanye ninyi kwa ninyi. | And he took the cup, and gave thanks, and said, Take this, and divide it among yourselves: |
| 18 | Kwa maana nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka Ufalme wa Mungu utakapokuja." | For I say unto you, I will not drink of the fruit of the vine, until the kingdom of God shall come. |
| 19 | Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, "Huu ni mwili wangu, unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka." | And he took bread, and gave thanks, and brake it, and gave unto them, saying, This is my body which is given for you: this do in remembrance of me. |
| 20 | Akafanya vivyo hivyo na kikombe, baada ya chakula, akisema, "Kikombe hiki ni agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu inayomwagika kwa ajili yenu. | Likewise also the cup after supper, saying, This cup is the new testament in my blood, which is shed for you. |
| 21 | "Lakini, tazameni! Yule atakayenisaliti yuko nami hapa mezani. | But, behold, the hand of him that betrayeth me is with me on the table. |
| 22 | Kweli Mwana wa Mtu anakwenda kuuawa kama ilivyopangwa, lakini ole wake mtu anayemsaliti." | And truly the Son of man goeth, as it was determined: but woe unto that man by whom he is betrayed! |
| 23 | Hapo wakaanza kuulizana wao kwa wao ni nani kati yao atakayefanya jambo hilo. | And they began to enquire among themselves, which of them it was that should do this thing. |
| 24 | Kulitokea ubishi kati ya hao mitume kuhusu nani miongoni mwao anayefikiriwa kuwa mkuu zaidi kuliko wengine. | And there was also a strife among them, which of them should be accounted the greatest. |
| 25 | Yesu akawaambia, "Wafalme wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, nao huitwa wafadhili wa watu. | And he said unto them, The kings of the Gentiles exercise lordship over them; and they that exercise authority upon them are called benefactors. |
| 26 | Lakini isiwe hivyo kati yenu; bali, yule aliye mkuu kati yenu ni lazima awe mdogo wa wote, na aliye kiongozi lazima awe kama mtumishi. | But ye shall not be so: but he that is greatest among you, let him be as the younger; and he that is chief, as he that doth serve. |
| 27 | Kwa maana, ni nani aliye mkuu: yule anayeketi mezani kula chakula, ama yule anayetumikia? Bila shaka ni yule anayeketi mezani kula chakula! Hata hivyo, mimi niko hapa kati yenu kama mtumishi. | For whether is greater, he that sitteth at meat, or he that serveth? is not he that sitteth at meat? but I am among you as he that serveth. |
| 28 | "Ninyi ndio mliobaki nami wakati wote wa majaribu yangu; | Ye are they which have continued with me in my temptations. |
| 29 | na, kama vile Baba yangu alivyonikabidhi Ufalme, vivyo hivyo nami nitawakabidhi ninyi Ufalme. | And I appoint unto you a kingdom, as my Father hath appointed unto me; |
| 30 | Mtakula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na mtaketi katika viti vya enzi kuyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. | That ye may eat and drink at my table in my kingdom, and sit on thrones judging the twelve tribes of Israel. |
| 31 | "Simoni, Simoni! Sikiliza! Shetani alitaka kuwapepeta ninyi kama mtu anavyopepeta ngano. | And the Lord said, Simon, Simon, behold, Satan hath desired to have you, that he may sift you as wheat: |
| 32 | Lakini mimi nimekuombea ili imani yako isipungue. Nawe utakaponirudia, watie moyo ndugu zako." | But I have prayed for thee, that thy faith fail not: and when thou art converted, strengthen thy brethren. |
| 33 | Naye Petro akamjibu, "Bwana, mimi niko tayari kwenda pamoja nawe gerezani, na hata kufa." | And he said unto him, Lord, I am ready to go with thee, both into prison, and to death. |
| 34 | Yesu akamjibu, "Nakwambia wewe Petro, kabla jogoo hajawika leo utakuwa umenikana mara tatu." | And he said, I tell thee, Peter, the cock shall not crow this day, before that thou shalt thrice deny that thou knowest me. |
| 35 | Kisha, Yesu akawauliza wanafunzi wake, "Wakati nilipowatuma bila mfuko wa fedha wala mkoba wala viatu, mlitindikiwa chochote?" Wakajibu, "La." | And he said unto them, When I sent you without purse, and scrip, and shoes, lacked ye any thing? And they said, Nothing. |
| 36 | Naye akawaambia, "Lakini sasa, yule aliye na mfuko wa fedha auchukue; na aliye na mkoba, hali kadhalika. Na yeyote asiye na upanga, auze koti lake anunue mmoja. | Then said he unto them, But now, he that hath a purse, let him take it, and likewise his scrip: and he that hath no sword, let him sell his garment, and buy one. |
| 37 | Maana nawaambieni, haya maneno ya Maandiko Matakatifu: Aliwekwa kundi moja na wahalifu, ni lazima yatimie. Naam, yale yanayonihusu yanafikia ukamilifu wake." | For I say unto you, that this that is written must yet be accomplished in me, And he was reckoned among the transgressors: for the things concerning me have an end. |
| 38 | Nao wakasema, "Bwana, tazama; hapa kuna panga mbili." Naye akasema, "Basi!" | And they said, Lord, behold, here are two swords. And he said unto them, It is enough. |
| 39 | Yesu akatoka, na kama ilivyokuwa desturi yake, akaenda katika mlima wa Mizeituni; wanafunzi wake wakamfuata. | And he came out, and went, as he was wont, to the mount of Olives; and his disciples also followed him. |
| 40 | Alipofika huko akawaambia, "Salini, msije mkaingia katika kishawishi." | And when he was at the place, he said unto them, Pray that ye enter not into temptation. |
| 41 | Kisha akawaacha, akaenda umbali wa mtu kuweza kutupa jiwe, akapiga magoti, akasali: | And he was withdrawn from them about a stone’s cast, and kneeled down, and prayed, |
| 42 | "Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki; hata hivyo, mapenzi yako yatimizwe, wala siyo yangu." | Saying, Father, if thou be willing, remove this cup from me: nevertheless not my will, but thine, be done. |
| 43 | Hapo, malaika kutoka mbinguni, akamtokea ili kumtia moyo. | And there appeared an angel unto him from heaven, strengthening him. |
| 44 | Akiwa katika uchungu mkubwa, alisali kwa bidii zaidi; na jasho likamtoka, kama matone ya damu, likatiririka mpaka chini. | And being in an agony he prayed more earnestly: and his sweat was as it were great drops of blood falling down to the ground. |
| 45 | Baada ya kusali, aliwarudia wanafunzi wake, akawakuta wamelala, kwani walikuwa na huzuni. | And when he rose up from prayer, and was come to his disciples, he found them sleeping for sorrow, |
| 46 | Akawaambia, "Mbona mnalala? Amkeni msali, msije mkaingia katika kishawishi." | And said unto them, Why sleep ye? rise and pray, lest ye enter into temptation. |
| 47 | Alipokuwa bado anaongea, kundi la watu likaja likiongozwa na yule aliyeitwa Yuda, mmoja wa wale mitume kumi na wawili. Yuda akaenda kumsalimu Yesu kwa kumbusu. | And while he yet spake, behold a multitude, and he that was called Judas, one of the twelve, went before them, and drew near unto Jesus to kiss him. |
| 48 | Lakini Yesu akamwambia, "Yuda! Je, unamsaliti Mwana wa Mtu kwa kumbusu?" | But Jesus said unto him, Judas, betrayest thou the Son of man with a kiss? |
| 49 | Wale wanafunzi wake walipoona hayo wakasema, "Bwana, tutumie panga zetu?" | When they which were about him saw what would follow, they said unto him, Lord, shall we smite with the sword? |
| 50 | Na mmoja wao akampiga upanga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio lake la kulia. | And one of them smote the servant of the high priest, and cut off his right ear. |
| 51 | Hapo, Yesu akasema, "Acha! Hii inatosha." Akaligusa sikio la mtu huyo akaliponya. | And Jesus answered and said, Suffer ye thus far. And he touched his ear, and healed him. |
| 52 | Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa Hekalu na wazee waliokuja kumkamata: "Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi? | Then Jesus said unto the chief priests, and captains of the temple, and the elders, which were come to him, Be ye come out, as against a thief, with swords and staves? |
| 53 | Nilipokuwa pamoja nanyi kila siku Hekaluni hamkunitia nguvuni. Lakini, huu ndio wakati wenu hasa, ndio wakati wa utawala wa giza." | When I was daily with you in the temple, ye stretched forth no hands against me: but this is your hour, and the power of darkness. |
| 54 | Basi, wakamkamata, wakamchukua na kwenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Petro akawa anamfuata nyuma kwa mbali. | Then took they him, and led him, and brought him into the high priest’s house. And Peter followed afar off. |
| 55 | Moto ulikuwa umewashwa katikati ya ua, nao wakawa wameketi pamoja Petro akiwa miongoni mwao. | And when they had kindled a fire in the midst of the hall, and were set down together, Peter sat down among them. |
| 56 | Mjakazi mmoja alipomwona Petro ameketi karibu na moto, akamkodolea macho, akasema, "Mtu huyu alikuwa pia pamoja na Yesu." | But a certain maid beheld him as he sat by the fire, and earnestly looked upon him, and said, This man was also with him. |
| 57 | Lakini Petro akakana akisema, "Wee! simjui mimi." | And he denied him, saying, Woman, I know him not. |
| 58 | Baadaye kidogo, mtu mwingine akamwona Petro, akasema, "Wewe ni mmoja wao." Lakini Petro akajibu "Bwana we; si mimi!" | And after a little while another saw him, and said, Thou art also of them. And Peter said, Man, I am not. |
| 59 | Kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasisitiza, "Hakika huyu alikuwa pamoja naye; ametoka Galilaya ati." | And about the space of one hour after another confidently affirmed, saying, Of a truth this fellow also was with him: for he is a Galilean. |
| 60 | Lakini Petro akasema, "Bwana wee; sijui hata unachosema!" Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika. | And Peter said, Man, I know not what thou sayest. And immediately, while he yet spake, the cock crew. |
| 61 | Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: "Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." | And the Lord turned, and looked upon Peter. And Peter remembered the word of the Lord, how he had said unto him, Before the cock crow, thou shalt deny me thrice. |
| 62 | Hapo akatoka nje, akalia sana. | And Peter went out, and wept bitterly. |
| 63 | Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki. | And the men that held Jesus mocked him, and smote him. |
| 64 | Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, "Ni nani aliyekupiga? Hebu bashiri tuone!" | And when they had blindfolded him, they struck him on the face, and asked him, saying, Prophesy, who is it that smote thee? |
| 65 | Wakamtolea maneno mengi ya matusi. | And many other things blasphemously spake they against him. |
| 66 | Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo. | And as soon as it was day, the elders of the people and the chief priests and the scribes came together, and led him into their council, saying, |
| 67 | Nao wakamwambia, "Twambie! Je, wewe ndiwe Kristo?" Lakini Yesu akawaambia, "Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki; | Art thou the Christ? tell us. And he said unto them, If I tell you, ye will not believe: |
| 68 | na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu. | And if I also ask you, ye will not answer me, nor let me go. |
| 69 | Lakini tangu sasa, Mwana wa Mtu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi." | Hereafter shall the Son of man sit on the right hand of the power of God. |
| 70 | Hapo wote wakasema, "Ndiyo kusema wewe ni Mwana wa Mungu?" Naye akasema, "Ninyi mnasema kwamba mimi ndiye." | Then said they all, Art thou then the Son of God? And he said unto them, Ye say that I am. |
| 71 | Nao wakasema, "Je, tunahitaji ushahidi mwingine? Sisi wenyewe tumesikia akisema kwa mdomo wake mwenyewe." | And they said, What need we any further witness? for we ourselves have heard of his own mouth. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL