히브리서 1장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 히브리서 (Hebrews) · 14절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii, | God, who at sundry times and in divers manners spake in time past unto the fathers by the prophets, |
| 2 | lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu na akamteua avimiliki vitu vyote. | Hath in these last days spoken unto us by his Son, whom he hath appointed heir of all things, by whom also he made the worlds; |
| 3 | Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu. | Who being the brightness of his glory, and the express image of his person, and upholding all things by the word of his power, when he had by himself purged our sins, sat down on the right hand of the Majesty on high; |
| 4 | Mwana ni mkuu zaidi kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu zaidi kuliko jina lao. | Being made so much better than the angels, as he hath by inheritance obtained a more excellent name than they. |
| 5 | Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: "Wewe ni Mwanangu; Mimi leo nimekuwa Baba yako." Wala hakusema juu ya malaika yeyote: "Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu." | For unto which of the angels said he at any time, Thou art my Son, this day have I begotten thee? And again, I will be to him a Father, and he shall be to me a Son? |
| 6 | Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, alisema: "Malaika wote wa Mungu wanapaswa kumwabudu." | And again, when he bringeth in the firstbegotten into the world, he saith, And let all the angels of God worship him. |
| 7 | Lakini kuhusu malaika, Mungu alisema: "Mungu awafanya malaika wake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa ndimi za moto." | And of the angels he saith, Who maketh his angels spirits, and his ministers a flame of fire. |
| 8 | Lakini kumhusu Mwana, Mungu alisema: "Utawala wako ee Mungu, wadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki. | But unto the Son he saith, Thy throne, O God, is for ever and ever: a sceptre of righteousness is the sceptre of thy kingdom. |
| 9 | Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa zaidi kuliko wenzako." | Thou hast loved righteousness, and hated iniquity; therefore God, even thy God, hath anointed thee with the oil of gladness above thy fellows. |
| 10 | Pia alisema: "Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo, mbingu ni kazi ya mikono yako. | And, Thou, Lord, in the beginning hast laid the foundation of the earth; and the heavens are the works of thine hands: |
| 11 | Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zote zitachakaa kama vazi. | They shall perish; but thou remainest; and they all shall wax old as doth a garment; |
| 12 | Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma." | And as a vesture shalt thou fold them up, and they shall be changed: but thou art the same, and thy years shall not fail. |
| 13 | Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: "Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako." | But to which of the angels said he at any time, Sit on my right hand, until I make thine enemies thy footstool? |
| 14 | Malaika ni roho tu wanaomtumikia Mungu, na Mungu huwatuma wawasaidie wale watakaopokea wokovu. | Are they not all ministering spirits, sent forth to minister for them who shall be heirs of salvation? |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL