로그인

빌레몬서 1장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 빌레몬서 (Philemon) · 25절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, na ndugu Timotheo, ninakuandikia wewe Filemoni mpendwa, mfanyakazi mwenzetu Paul, a prisoner of Jesus Christ, and Timothy our brother, unto Philemon our dearly beloved, and fellowlabourer,
2 na kanisa linalokutana nyumbani kwako, na wewe dada Afia, na askari mwenzetu Arkupo. And to our beloved Apphia, and Archippus our fellowsoldier, and to the church in thy house:
3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana yesu Kristo. Grace to you, and peace, from God our Father and the Lord Jesus Christ.
4 Kila wakati ninaposali nakukumbuka wewe Filemoni, na kumshukuru Mungu I thank my God, making mention of thee always in my prayers,
5 maana nasikia habari za imani yako kwa Bwana wetu Yesu na upendo wako kwa watu wote wa Mungu. Hearing of thy love and faith, which thou hast toward the Lord Jesus, and toward all saints;
6 Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo. That the communication of thy faith may become effectual by the acknowledging of every good thing which is in you in Christ Jesus.
7 Ndugu, upendo wako yameniletea furaha kubwa na kunipa moyo sana! Nawe umeichangamsha mioyo ya watu wa Mungu. For we have great joy and consolation in thy love, because the bowels of the saints are refreshed by thee, brother.
8 Kwa sababu hiyo, ningeweza, kwa uhodari kabisa, nikiwa ndugu yako katika Kristo, kukuamuru ufanye unachopaswa kufanya. Wherefore, though I might be much bold in Christ to enjoin thee that which is convenient,
9 Lakini kwa sababu ya upendo, ni afadhali zaidi nikuombe. Nafanya hivi ingawa mimi ni Paulo, balozi wa Kristo Yesu, na sasa pia mfungwa kwa ajili yake. Yet for love’s sake I rather beseech thee, being such an one as Paul the aged, and now also a prisoner of Jesus Christ.
10 Basi, ninalo ombi moja kwako kuhusu mwanangu Onesimo, ambaye ni mwanangu katika Kristo kwani nimekuwa baba yake nikiwa kifungoni. I beseech thee for my son Onesimus, whom I have begotten in my bonds:
11 Ni Onesimo yuleyule ambaye wakati mmoja alikuwa hakufai kitu, lakini sasa ananifaa mimi na wewe pia. Which in time past was to thee unprofitable, but now profitable to thee and to me:
12 Sasa namrudisha kwako, naye ni kama moyo wangu mimi mwenyewe. Whom I have sent again: thou therefore receive him, that is, mine own bowels:
13 Ningependa akae nami hapa anisaidie badala yako wakati niwapo kifungoni kwa sababu ya Habari Njema. Whom I would have retained with me, that in thy stead he might have ministered unto me in the bonds of the gospel:
14 Lakini sitafanya chochote bila kibali chako. Sipendi kukulazimisha unisaidie, kwani wema wako unapaswa kutokana na hiari yako wewe mwenyewe na si kwa kulazimika. But without thy mind would I do nothing; that thy benefit should not be as it were of necessity, but willingly.
15 Labda Onesimo aliondoka kwako kwa kitambo tu, kusudi uweze tena kuwa naye daima. For perhaps he therefore departed for a season, that thou shouldest receive him for ever;
16 Na sasa yeye si mtumwa tu, ila ni bora zaidi ya mtumwa: yeye ni ndugu yetu mpenzi. Na wa maana sana kwangu mimi, na kwako atakuwa wa maana zaidi kama mtumwa na kama ndugu katika Bwana. Not now as a servant, but above a servant, a brother beloved, specially to me, but how much more unto thee, both in the flesh, and in the Lord?
17 Basi, ikiwa wanitambua mimi kuwa mwenzako, mpokee tena kama vile ungenipokea mimi mwenyewe. If thou count me therefore a partner, receive him as myself.
18 Kama alikuwa amekukosea kitu, au alikuwa na deni lako, basi, unidai mimi. If he hath wronged thee, or oweth thee ought, put that on mine account;
19 Naandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe: Mimi Paulo nitalipa! (Tena sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako.) I Paul have written it with mine own hand, I will repay it: albeit I do not say to thee how thou owest unto me even thine own self besides.
20 Haya, basi, ndugu yangu, nifanyie jambo hilo kwa ajili ya jina la Bwana; burudisha moyo wangu kama ndugu katika Kristo. Yea, brother, let me have joy of thee in the Lord: refresh my bowels in the Lord.
21 Naandika nikitumaini kwamba utanikubalia ombi langu; tena najua kwamba utafanya hata zaidi ya haya ninayokuomba. Having confidence in thy obedience I wrote unto thee, knowing that thou wilt also do more than I say.
22 Pamoja na hayo, nitayarishie chumba kwani natumaini kwamba kwa sala zenu, Mungu atanijalia niwatembeleeni. But withal prepare me also a lodging: for I trust that through your prayers I shall be given unto you.
23 Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu, anakusalimu. There salute thee Epaphras, my fellowprisoner in Christ Jesus;
24 Nao akina Marko, Aristarko, Dema na Luka, wafanyakazi wenzangu, wanakusalimu. Marcus, Aristarchus, Demas, Lucas, my fellowlabourers.
25 Nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. The grace of our Lord Jesus Christ be with your spirit. Amen. Written from Rome to Philemon, by Onesimus a servant.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL