요한복음 16장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 요한복음 (John) · 33절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | "Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. | These things have I spoken unto you, that ye should not be offended. |
| 2 | Watu watawatenga ninyi na masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua ninyi atadhani anamhudumia Mungu. | They shall put you out of the synagogues: yea, the time cometh, that whosoever killeth you will think that he doeth God service. |
| 3 | Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi. | And these things will they do unto you, because they have not known the Father, nor me. |
| 4 | Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni. "Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi. | But these things have I told you, that when the time shall come, ye may remember that I told you of them. And these things I said not unto you at the beginning, because I was with you. |
| 5 | Lakini sasa namwendea yule aliyenituma; na hakuna hata mmoja wenu anayeniuliza: Unakwenda wapi? | But now I go my way to him that sent me; and none of you asketh me, Whither goest thou? |
| 6 | Kwa kuwa nimewaambieni mambo hayo mmejaa huzuni mioyoni mwenu. | But because I have said these things unto you, sorrow hath filled your heart. |
| 7 | Lakini, nawaambieni ukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu. | Nevertheless I tell you the truth; It is expedient for you that I go away: for if I go not away, the Comforter will not come unto you; but if I depart, I will send him unto you. |
| 8 | Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu. | And when he is come, he will reprove the world of sin, and of righteousness, and of judgment: |
| 9 | Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; | Of sin, because they believe not on me; |
| 10 | kuhusu uadilifu, kwa sababu naenda zangu kwa Baba, nanyi hamtaniona tena; | Of righteousness, because I go to my Father, and ye see me no more; |
| 11 | kuhusu hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa. | Of judgment, because the prince of this world is judged. |
| 12 | "Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili. | I have yet many things to say unto you, but ye cannot bear them now. |
| 13 | Lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza kwenye ukweli wote; maana hatasema kwa mamlaka yake mwenyewe, bali atawaambieni yote atakayosikia, na atasema mambo yatakayokuwa yanakuja. | Howbeit when he, the Spirit of truth, is come, he will guide you into all truth: for he shall not speak of himself; but whatsoever he shall hear, that shall he speak: and he will shew you things to come. |
| 14 | Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu. | He shall glorify me: for he shall receive of mine, and shall shew it unto you. |
| 15 | Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu; ndiyo maana nimesema kwamba huyo Roho Mtakatifu atawaambieni yale atakayopata kutoka kwangu. | All things that the Father hath are mine: therefore said I, that he shall take of mine, and shall shew it unto you. |
| 16 | "Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona!" | A little while, and ye shall not see me: and again, a little while, and ye shall see me, because I go to the Father. |
| 17 | Hapo baadhi ya wanafunzi wake wakaulizana, "Ana maana gani anapotwambia: Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona? Tena anasema: Kwa kuwa ninakwenda kwa Baba!" | Then said some of his disciples among themselves, What is this that he saith unto us, A little while, and ye shall not see me: and again, a little while, and ye shall see me: and, Because I go to the Father? |
| 18 | Basi, wakawa wanaulizana, "Ana maana gani anaposema: Bado kitambo kidogo? Hatuelewi anaongelea nini." | They said therefore, What is this that he saith, A little while? we cannot tell what he saith. |
| 19 | Yesu alijua kwamba walitaka kumwuliza, basi akawaambia, "Je, mnaulizana juu ya yale niliyosema: Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona; na baada ya kitambo kidogo tena mtaniona? | Now Jesus knew that they were desirous to ask him, and said unto them, Do ye enquire among yourselves of that I said, A little while, and ye shall not see me: and again, a little while, and ye shall see me? |
| 20 | Nawaambieni kweli, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi: mtaona huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. | Verily, verily, I say unto you, That ye shall weep and lament, but the world shall rejoice: and ye shall be sorrowful, but your sorrow shall be turned into joy. |
| 21 | Wakati mama anapojifungua huona huzuni kwa sababu saa ya maumivu imefika; lakini akisha jifungua hayakumbuki tena maumivu hayo kwa sababu ya furaha kwamba mtu amezaliwa duniani. | A woman when she is in travail hath sorrow, because her hour is come: but as soon as she is delivered of the child, she remembereth no more the anguish, for joy that a man is born into the world. |
| 22 | Ninyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu. | And ye now therefore have sorrow: but I will see you again, and your heart shall rejoice, and your joy no man taketh from you. |
| 23 | Siku hiyo hamtaniomba chochote. Kweli nawaambieni, chochote mtakachomwomba Baba kwa jina langu, atawapeni. | And in that day ye shall ask me nothing. Verily, verily, I say unto you, Whatsoever ye shall ask the Father in my name, he will give it you. |
| 24 | Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike. | Hitherto have ye asked nothing in my name: ask, and ye shall receive, that your joy may be full. |
| 25 | "Nimewaambieni mambo hayo kwa mafumbo. Lakini wakati utakuja ambapo sitasema tena nanyi kwa mafumbo, bali nitawaambieni waziwazi juu ya Baba. | These things have I spoken unto you in proverbs: but the time cometh, when I shall no more speak unto you in proverbs, but I shall shew you plainly of the Father. |
| 26 | Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; | At that day ye shall ask in my name: and I say not unto you, that I will pray the Father for you: |
| 27 | maana yeye mwenyewe anawapenda ninyi, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Mungu. | For the Father himself loveth you, because ye have loved me, and have believed that I came out from God. |
| 28 | Mimi nilitoka kwa Baba, nikaja ulimwenguni; na sasa nauacha ulimwengu na kurudi kwa Baba." | I came forth from the Father, and am come into the world: again, I leave the world, and go to the Father. |
| 29 | Basi, wanafunzi wake wakamwambia, "Ahaa! Sasa unasema waziwazi kabisa bila kutumia mafumbo. | His disciples said unto him, Lo, now speakest thou plainly, and speakest no proverb. |
| 30 | Sasa tunajua kwamba wewe unajua kila kitu, na huna haja ya kuulizwa maswali na mtu yeyote; kwa hiyo tunaamini kwamba umetoka kwa Mungu." | Now are we sure that thou knowest all things, and needest not that any man should ask thee: by this we believe that thou camest forth from God. |
| 31 | Yesu akawajibu, "Je, mnaamini sasa? | Jesus answered them, Do ye now believe? |
| 32 | Wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo ninyi nyote mtatawanyika kila mtu kwake, nami nitaachwa peke yangu. Kumbe, lakini mimi siko peke yangu, maana Baba yu pamoja nami. | Behold, the hour cometh, yea, is now come, that ye shall be scattered, every man to his own, and shall leave me alone: and yet I am not alone, because the Father is with me. |
| 33 | Nimewaambieni mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!" | These things I have spoken unto you, that in me ye might have peace. In the world ye shall have tribulation: but be of good cheer; I have overcome the world. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL