에베소서 6장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 에베소서 (Ephesians) · 24절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Enyi watoto, watiini wazazi wenu Kikristo maana hili ni jambo jema. | Children, obey your parents in the Lord: for this is right. |
| 2 | "Waheshimu Baba na mama yako," hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, | Honour thy father and mother; (which is the first commandment with promise;) |
| 3 | "Upate fanaka na miaka mingi duniani." | That it may be well with thee, and thou mayest live long on the earth. |
| 4 | Nanyi akina baba, msiwachukize watoto wenu ila waleeni katika nidhamu na mafundisho ya Kikristo. | And, ye fathers, provoke not your children to wrath: but bring them up in the nurture and admonition of the Lord. |
| 5 | Enyi watumwa, watiini mabwana zenu hapa duniani kwa hofu na tetemeko; fanyeni hivyo kwa unyofu wa moyo kana kwamba mnamtumikia Kristo. | Servants, be obedient to them that are your masters according to the flesh, with fear and trembling, in singleness of your heart, as unto Christ; |
| 6 | Fanyeni hivyo si tu wakati wanapowatazama ili mjipendekeze kwao, bali tumikieni kwa moyo kama atakavyo Mungu kwa sababu ninyi ni watumishi wa Kristo. | Not with eyeservice, as menpleasers; but as the servants of Christ, doing the will of God from the heart; |
| 7 | Muwe radhi kutumikia kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya watu. | With good will doing service, as to the Lord, and not to men: |
| 8 | Kumbukeni kwamba kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka kwa Bwana. | Knowing that whatsoever good thing any man doeth, the same shall he receive of the Lord, whether he be bond or free. |
| 9 | Nanyi mnaotumikiwa, watendeeni vivyo hivyo watumwa wenu, na acheni kutumia vitisho. Kumbukeni kwamba ninyi pia kama vile wao, mnaye Bwana yuleyule mbinguni, kwake cheo cha mtu si kitu. | And, ye masters, do the same things unto them, forbearing threatening: knowing that your Master also is in heaven; neither is there respect of persons with him. |
| 10 | Hatimaye, nawatakeni muwe imara katika kuungana na Bwana na kwa msaada wa nguvu yake kuu. | Finally, my brethren, be strong in the Lord, and in the power of his might. |
| 11 | Vaeni silaha anazowapeni Mungu mpate kuzipinga mbinu mbaya za Ibilisi. | Put on the whole armour of God, that ye may be able to stand against the wiles of the devil. |
| 12 | Maana vita vyenu si vita kati yetu na binadamu, bali ni vita dhidi ya jeshi ovu la ulimwengu wa roho; tunapigana na watawala, wakuu na wenye nguvu wanaomiliki ulimwengu huu wa giza. | For we wrestle not against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this world, against spiritual wickedness in high places. |
| 13 | Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika muweze kuyapinga mashambulio ya adui; na mkisha pigana mpaka mwisho, muwe bado thabiti. | Wherefore take unto you the whole armour of God, that ye may be able to withstand in the evil day, and having done all, to stand. |
| 14 | Basi, simameni imara! Ukweli uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, | Stand therefore, having your loins girt about with truth, and having on the breastplate of righteousness; |
| 15 | na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. | And your feet shod with the preparation of the gospel of peace; |
| 16 | Zaidi ya hayo yote, imani iwe daima kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule Mwovu. | Above all, taking the shield of faith, wherewith ye shall be able to quench all the fiery darts of the wicked. |
| 17 | Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. | And take the helmet of salvation, and the sword of the Spirit, which is the word of God: |
| 18 | Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu. | Praying always with all prayer and supplication in the Spirit, and watching thereunto with all perseverance and supplication for all saints; |
| 19 | Niombeeni nami pia ili niongeapo Mungu anijalie cha kusema, niweze kuwajulisha watu fumbo la Habari Njema kwa uthabiti. | And for me, that utterance may be given unto me, that I may open my mouth boldly, to make known the mystery of the gospel, |
| 20 | Mimi ni balozi kwa ajili ya Habari Njema hiyo ingawa sasa niko kifungoni. Ombeni, basi, ili niweze kuwa hodari katika kuitangaza kama inipasavyo. | For which I am an ambassador in bonds: that therein I may speak boldly, as I ought to speak. |
| 21 | Tukiko, ndugu yetu mpenzi na mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawapeni habari zangu zote mpate kujua ninachofanya. | But that ye also may know my affairs, and how I do, Tychicus, a beloved brother and faithful minister in the Lord, shall make known to you all things: |
| 22 | Namtuma kwenu awapeni habari zetu mpate kuwa na moyo. | Whom I have sent unto you for the same purpose, that ye might know our affairs, and that he might comfort your hearts. |
| 23 | Ninawatakieni ninyi ndugu amani, upendo na imani kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. | Peace be to the brethren, and love with faith, from God the Father and the Lord Jesus Christ. |
| 24 | Nawatakia neema ya Mungu wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa mapendo yasiyo na mwisho. | Grace be with all them that love our Lord Jesus Christ in sincerity. Amen. Written from Rome unto the Ephesians by Tychicus. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL