에베소서 5장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 에베소서 (Ephesians) · 33절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Kwa hiyo, mwigeni Mungu, maana ninyi ni watoto wake wapenzi. | Be ye therefore followers of God, as dear children; |
| 2 | Upendo uongoze maisha yenu, kama vile Kristo alivyotupenda, na kwa ajili yetu akajitoa mwenyewe kama dhabihu yenye harufu nzuri na tambiko impendezayo Mungu. | And walk in love, as Christ also hath loved us, and hath given himself for us an offering and a sacrifice to God for a sweetsmelling savour. |
| 3 | Kwa vile ninyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu. | But fornication, and all uncleanness, or covetousness, let it not be once named among you, as becometh saints; |
| 4 | Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa. | Neither filthiness, nor foolish talking, nor jesting, which are not convenient: but rather giving of thanks. |
| 5 | Jueni wazi kwamba mwasherati yeyote au mchafu au mfisadi, (ufisadi ni sawa na kuabudu sanamu), au mtu yeyote wa aina hiyo hataambulia chochote katika Utawala wa Kristo na wa Mungu. | For this ye know, that no whoremonger, nor unclean person, nor covetous man, who is an idolater, hath any inheritance in the kingdom of Christ and of God. |
| 6 | Msikubali kudanganywa na mtu kwa maneno matupu; maana, kwa sababu ya mambo kama hayo ghadhabu ya Mungu huwajia wote wasiomtii. | Let no man deceive you with vain words: for because of these things cometh the wrath of God upon the children of disobedience. |
| 7 | Basi, msishirikiane nao. | Be not ye therefore partakers with them. |
| 8 | Zamani ninyi mlikuwa gizani, lakini sasa ninyi mko katika mwanga kwa kuungana na Bwana. Ishini kama watoto wa mwanga: | For ye were sometimes darkness, but now are ye light in the Lord: walk as children of light: |
| 9 | maana matokeo ya mwanga ni wema kamili, uadilifu na ukweli. | (For the fruit of the Spirit is in all goodness and righteousness and truth;) |
| 10 | Jaribuni kujua yale yanayompendeza Bwana. | Proving what is acceptable unto the Lord. |
| 11 | Msishiriki katika matendo yasiyofaa, ya giza bali yafichueni. | And have no fellowship with the unfruitful works of darkness, but rather reprove them. |
| 12 | Mambo yanayotendwa kwa siri ni aibu hata kuyataja. | For it is a shame even to speak of those things which are done of them in secret. |
| 13 | Lakini mambo yale yanayotendwa katika mwanga, ukweli wake hudhihirishwa; | But all things that are reproved are made manifest by the light: for whatsoever doth make manifest is light. |
| 14 | na kila kilichodhihirishwa huwa mwanga. Ndiyo maana Maandiko yasema: "Amka wewe uliyelala, fufuka kutoka wafu, naye Kristo atakuangaza." | Wherefore he saith, Awake thou that sleepest, and arise from the dead, and Christ shall give thee light. |
| 15 | Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima. | See then that ye walk circumspectly, not as fools, but as wise, |
| 16 | Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. | Redeeming the time, because the days are evil. |
| 17 | Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana. | Wherefore be ye not unwise, but understanding what the will of the Lord is. |
| 18 | Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. | And be not drunk with wine, wherein is excess; but be filled with the Spirit; |
| 19 | Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. | Speaking to yourselves in psalms and hymns and spiritual songs, singing and making melody in your heart to the Lord; |
| 20 | Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo. | Giving thanks always for all things unto God and the Father in the name of our Lord Jesus Christ; |
| 21 | Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo. | Submitting yourselves one to another in the fear of God. |
| 22 | Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. | Wives, submit yourselves unto your own husbands, as unto the Lord. |
| 23 | Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. | For the husband is the head of the wife, even as Christ is the head of the church: and he is the saviour of the body. |
| 24 | Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote. | Therefore as the church is subject unto Christ, so let the wives be to their own husbands in every thing. |
| 25 | Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. | Husbands, love your wives, even as Christ also loved the church, and gave himself for it; |
| 26 | Alifanya hivyo, ili kwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada ya kulifanya safi kwa kuliosha katika maji, | That he might sanctify and cleanse it with the washing of water by the word, |
| 27 | kusudi ajipatie kanisa lililo takatifu na safu kabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au chochote cha namna hiyo. | That he might present it to himself a glorious church, not having spot, or wrinkle, or any such thing; but that it should be holy and without blemish. |
| 28 | Basi, waume wanapaswa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. | So ought men to love their wives as their own bodies. He that loveth his wife loveth himself. |
| 29 | (Hakuna mtu yeyote auchukiaye mwili wake; badala ya kuuchukia, huulisha na kuuvika. Ndivyo naye Kristo anavyolitunza kanisa, | For no man ever yet hated his own flesh; but nourisheth and cherisheth it, even as the Lord the church: |
| 30 | maana sisi ni viungo vya mwili wake.) | For we are members of his body, of his flesh, and of his bones. |
| 31 | Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja." | For this cause shall a man leave his father and mother, and shall be joined unto his wife, and they two shall be one flesh. |
| 32 | Kuna ukweli uliofichika katika maneno haya, nami naona kwamba yamhusu Kristo na kanisa lake. | This is a great mystery: but I speak concerning Christ and the church. |
| 33 | Lakini yanawahusu ninyi pia: kila mume lazima ampende mkewe kama nafsi yake mwenyewe, naye mke anapaswa kumstahi mumewe. | Nevertheless let every one of you in particular so love his wife even as himself; and the wife see that she reverence her husband. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL