에베소서 1장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 에베소서 (Ephesians) · 23절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, nawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Efeso, mlio waaminifu katika kuungana na Kristo Yesu. | Paul, an apostle of Jesus Christ by the will of God, to the saints which are at Ephesus, and to the faithful in Christ Jesus: |
| 2 | Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. | Grace be to you, and peace, from God our Father, and from the Lord Jesus Christ. |
| 3 | Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zote za kiroho mbinguni. | Blessed be the God and Father of our Lord Jesus Christ, who hath blessed us with all spiritual blessings in heavenly places in Christ: |
| 4 | Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituteua tuwe wake katika kuungana na Kristo ili tuwe watakatifu na bila hitilafu mbele yake. Kwa sababu ya upendo wake, | According as he hath chosen us in him before the foundation of the world, that we should be holy and without blame before him in love: |
| 5 | Mungu alikuwa ameazimia tangu zamani kutuleta kwake kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Ndivyo alivyopenda na kunuia. | Having predestinated us unto the adoption of children by Jesus Christ to himself, according to the good pleasure of his will, |
| 6 | Basi, tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu katika Mwanae mpenzi! | To the praise of the glory of his grace, wherein he hath made us accepted in the beloved. |
| 7 | Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake | In whom we have redemption through his blood, the forgiveness of sins, according to the riches of his grace; |
| 8 | aliotukirimia bila kipimo! Kwa hekima na ujuzi wake wote | Wherein he hath abounded toward us in all wisdom and prudence; |
| 9 | Mungu alitekeleza kile alichonuia, akatujulisha mpango wake uliofichika, ambao alikuwa ameazimia kuutekeleza kwa njia ya Kristo. | Having made known unto us the mystery of his will, according to his good pleasure which he hath purposed in himself: |
| 10 | Mpango huo ambao angeutimiza wakati utimiapo ni kukusanya pamoja viumbe vyote, kila kitu mbinguni na duniani, chini ya Kristo. | That in the dispensation of the fulness of times he might gather together in one all things in Christ, both which are in heaven, and which are on earth; even in him: |
| 11 | Kila kitu hufanywa kufuatana na mpango na uamuzi wa Mungu; naye Mungu ametuteua sisi tuwe watu wake kwa mapenzi yake katika kuungana na Kristo, kufuatana na azimio alilofanya tangu mwanzo. | In whom also we have obtained an inheritance, being predestinated according to the purpose of him who worketh all things after the counsel of his own will: |
| 12 | Basi, sisi tuliotangulia kumtumainia Kristo tunapaswa kuusifu utukufu wa Mungu! | That we should be to the praise of his glory, who first trusted in Christ. |
| 13 | Nanyi pia watu wa mataifa mengine, mliusikia ujumbe wa kweli yaani Habari Njema iliyowaletea wokovu, mkamwamini Kristo; naye Mungu, ili kuonyesha kuwa ninyi ni wake, akawapiga mhuri kwa kuwapeni yule Roho Mtakatifu aliyetuahidia. | In whom ye also trusted, after that ye heard the word of truth, the gospel of your salvation: in whom also after that ye believed, ye were sealed with that holy Spirit of promise, |
| 14 | Huyu Roho ni dhamana ya kurithi yote yale Mungu aliyowaahidia watu wake, na jambo hili latuhakikishia kwamba Mungu atawakomboa kabisa wote walio wake. Tuusifu utukufu wake! | Which is the earnest of our inheritance until the redemption of the purchased possession, unto the praise of his glory. |
| 15 | Kwa sababu hiyo, tangu niliposikia juu ya imani yenu kwa Bwana Yesu na mapendo yenu kwa watu wa Mungu, | Wherefore I also, after I heard of your faith in the Lord Jesus, and love unto all the saints, |
| 16 | sijaacha kamwe kumshukuru Mungu kwa ajili yenu. Ninawakumbuka katika sala zangu | Cease not to give thanks for you, making mention of you in my prayers; |
| 17 | ili Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Baba mtukufu, awajalieni Roho wake atakayewapa hekima na kuwafunulieni Mungu mpate kumjua. | That the God of our Lord Jesus Christ, the Father of glory, may give unto you the spirit of wisdom and revelation in the knowledge of him: |
| 18 | Namwomba Mungu aifunue mioyo yenu iweze kuuona mwanga wake, mpate kutambua lile tumaini alilowaitieni na utukufu mkuu wa zawadi alizowawekea watu wake, | The eyes of your understanding being enlightened; that ye may know what is the hope of his calling, and what the riches of the glory of his inheritance in the saints, |
| 19 | mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na nguvu ile kuu mno | And what is the exceeding greatness of his power to us-ward who believe, according to the working of his mighty power, |
| 20 | aliyomfufua nayo Kristo kutoka wafu, akamketisha kulia kwake mbinguni. | Which he wrought in Christ, when he raised him from the dead, and set him at his own right hand in the heavenly places, |
| 21 | Huko, Kristo anatawala juu ya kila tawala, mamlaka, enzi na ukuu; anatawala juu ya kila cheo kiwezacho kutajwa katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao. | Far above all principality, and power, and might, and dominion, and every name that is named, not only in this world, but also in that which is to come: |
| 22 | Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote. | And hath put all things under his feet, and gave him to be the head over all things to the church, |
| 23 | Kanisa ni mwili wa Kristo, na ukamilifu wake yeye anayekamilisha vitu vyote kila mahali. | Which is his body, the fulness of him that filleth all in all. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL