로그인

갈라디아서 6장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 갈라디아서 (Galatians) · 18절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Ndugu, kama mkimwona mtu fulani amekosea, basi, ninyi mnaoongozwa na Roho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe; lakini fanyeni hivyo kwa upole, mkiwa na tahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa. Brethren, if a man be overtaken in a fault, ye which are spiritual, restore such an one in the spirit of meekness; considering thyself, lest thou also be tempted.
2 Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo. Bear ye one another’s burdens, and so fulfil the law of Christ.
3 Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mwenyewe. For if a man think himself to be something, when he is nothing, he deceiveth himself.
4 Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. But let every man prove his own work, and then shall he have rejoicing in himself alone, and not in another.
5 Maana kila mmoja anao mzigo wake mwenyewe wa kubeba. For every man shall bear his own burden.
6 Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake riziki zake. Let him that is taught in the word communicate unto him that teacheth in all good things.
7 Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna. Be not deceived; God is not mocked: for whatsoever a man soweth, that shall he also reap.
8 Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uzima wa milele. For he that soweth to his flesh shall of the flesh reap corruption; but he that soweth to the Spirit shall of the Spirit reap life everlasting.
9 Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake. And let us not be weary in well doing: for in due season we shall reap, if we faint not.
10 Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na hasa ndugu wa imani yetu. As we have therefore opportunity, let us do good unto all men, especially unto them who are of the household of faith.
11 Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe. Ye see how large a letter I have written unto you with mine own hand.
12 Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha ninyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo. As many as desire to make a fair shew in the flesh, they constrain you to be circumcised; only lest they should suffer persecution for the cross of Christ.
13 Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria; huwataka ninyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu. For neither they themselves who are circumcised keep the law; but desire to have you circumcised, that they may glory in your flesh.
14 Lakini mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu. But God forbid that I should glory, save in the cross of our Lord Jesus Christ, by whom the world is crucified unto me, and I unto the world.
15 Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya. For in Christ Jesus neither circumcision availeth any thing, nor uncircumcision, but a new creature.
16 Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na huruma kwa Israeli--Wateule wa Mungu. And as many as walk according to this rule, peace be on them, and mercy, and upon the Israel of God.
17 Basi, sasa mtu yeyote asinisumbue tena, maana alama nilizo nazo mwilini mwangu ni zile za Yesu. From henceforth let no man trouble me: for I bear in my body the marks of the Lord Jesus.
18 Ndugu, nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Kristo. Amina. Brethren, the grace of our Lord Jesus Christ be with your spirit. Amen. Unto the Galatians written from Rome.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL