마태복음 9장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 38절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yesu alipanda mashua, akavuka ziwa na kufika katika mji wake. | And he entered into a ship, and passed over, and came into his own city. |
| 2 | Hapo watu walimletea mtu mmoja aliyepooza mwili, amelazwa juu ya kitanda. Yesu alipoona imani yao, akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Jipe moyo mwanangu! Umesamehewa dhambi zako." | And, behold, they brought to him a man sick of the palsy, lying on a bed: and Jesus seeing their faith said unto the sick of the palsy; Son, be of good cheer; thy sins be forgiven thee. |
| 3 | Baadhi ya walimu wa Sheria wakaanza kufikiri, "Mtu huyu anamkufuru Mungu!" | And, behold, certain of the scribes said within themselves, This man blasphemeth. |
| 4 | Yesu aliyajua mawazo yao, akasema, "Kwa nini mnawaza mabaya mioyoni mwenu? | And Jesus knowing their thoughts said, Wherefore think ye evil in your hearts? |
| 5 | Ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Simama, utembee? | For whether is easier, to say, Thy sins be forgiven thee; or to say, Arise, and walk? |
| 6 | Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani." Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, "Inuka, chukua kitanda chako, uende nyumbani kwako." | But that ye may know that the Son of man hath power on earth to forgive sins, (then saith he to the sick of the palsy,) Arise, take up thy bed, and go unto thine house. |
| 7 | Huyo mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akaenda nyumbani kwake. | And he arose, and departed to his house. |
| 8 | Watu wote katika ule umati walipoona hayo, walishangaa na kuogopa; wakamtukuza Mungu aliyewapa binadamu uwezo wa namna hiyo. | But when the multitudes saw it, they marvelled, and glorified God, which had given such power unto men. |
| 9 | Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda zake, alimwona mtu mmoja aitwaye Mathayo, ameketi katika ofisi ya ushuru. Basi, Yesu akamwambia, "Nifuate." Naye Mathayo akainuka, akamfuata. | And as Jesus passed forth from thence, he saw a man, named Matthew, sitting at the receipt of custom: and he saith unto him, Follow me. And he arose, and followed him. |
| 10 | Yesu alipokuwa nyumbani ameketi kula chakula, watoza ushuru wengi na wahalifu walikuja wakaketi pamoja naye na wanafunzi wake. | And it came to pass, as Jesus sat at meat in the house, behold, many publicans and sinners came and sat down with him and his disciples. |
| 11 | Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi wake, "Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?" | And when the Pharisees saw it, they said unto his disciples, Why eateth your Master with publicans and sinners? |
| 12 | Yesu aliwasikia, akasema, "Watu wenye afya hawahitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, ila wenye dhambi. | But when Jesus heard that, he said unto them, They that be whole need not a physician, but they that are sick. |
| 13 | Basi, kajifunzeni maana ya maneno haya: Nataka huruma, wala si dhabihu. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi." | But go ye and learn what that meaneth, I will have mercy, and not sacrifice: for I am not come to call the righteous, but sinners to repentance. |
| 14 | Kisha wanafunzi wa Yohane mbatizaji walimwendea Yesu, wakamwuliza, "Sisi na Mafarisayo hufunga mara nyingi; mbona wanafunzi wako hawafungi?" | Then came to him the disciples of John, saying, Why do we and the Pharisees fast oft, but thy disciples fast not? |
| 15 | Yesu akawajibu, "Je, walioalikwa arusini wanaweza kuomboleza wakati bwana arusi yupo pamoja nao? La hasha! Lakini wakati utafika ambapo bwana arusi ataondolewa kati yao; wakati huo ndipo watakapofunga. | And Jesus said unto them, Can the children of the bridechamber mourn, as long as the bridegroom is with them? but the days will come, when the bridegroom shall be taken from them, and then shall they fast. |
| 16 | "Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu. Maana kiraka hicho kitararua hilo vazi kuukuu, na pale palipokuwa pameraruka pataongezeka. | No man putteth a piece of new cloth unto an old garment, for that which is put in to fill it up taketh from the garment, and the rent is made worse. |
| 17 | Wala hakuna mtu awekaye divai mpya katika viriba vikuukuu. Akifanya hivyo, viriba hupasuka na divai ikamwagika, navyo viriba vikaharibika. Ila divai mpya hutiwa katika viriba vipya, na vyote viwili, viriba na divai, vikahifadhiwa salama." | Neither do men put new wine into old bottles: else the bottles break, and the wine runneth out, and the bottles perish: but they put new wine into new bottles, and both are preserved. |
| 18 | Yesu alipokuwa akisema hayo, ofisa mmoja Myahudi alifika, akamwinamia na kusema, "Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini, tafadhali njoo umwekee mkono wako naye ataishi." | While he spake these things unto them, behold, there came a certain ruler, and worshipped him, saying, My daughter is even now dead: but come and lay thy hand upon her, and she shall live. |
| 19 | Yesu akaondoka pamoja na wanafunzi wake, akamfuata. | And Jesus arose, and followed him, and so did his disciples. |
| 20 | Mama mmoja, mgonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, alimfuata Yesu nyuma, akagusa pindo la vazi lake. | And, behold, a woman, which was diseased with an issue of blood twelve years, came behind him, and touched the hem of his garment: |
| 21 | Alifanya hivyo kwani alifikiri moyoni: "Nikigusa tu vazi lake, nitapona." | For she said within herself, If I may but touch his garment, I shall be whole. |
| 22 | Basi, Yesu akageuka akamwona, akamwambia, "Binti, jipe moyo! Imani yako imekuponya." Mama huyo akapona saa ileile. | But Jesus turned him about, and when he saw her, he said, Daughter, be of good comfort; thy faith hath made thee whole. And the woman was made whole from that hour. |
| 23 | Kisha Yesu akaingia nyumbani kwa yule ofisa. Na alipowaona wapiga filimbi na umati wa watu wanaofanya matanga, | And when Jesus came into the ruler’s house, and saw the minstrels and the people making a noise, |
| 24 | akasema, "Ondokeni hapa! Msichana huyu hakufa, amelala tu." Nao wakamcheka. | He said unto them, Give place: for the maid is not dead, but sleepeth. And they laughed him to scorn. |
| 25 | Basi, umati wa watu ulipoondolewa, Yesu aliingia ndani, akamshika huyo msichana mkono, naye akasimama. | But when the people were put forth, he went in, and took her by the hand, and the maid arose. |
| 26 | Habari hiyo ikavuma sana katika nchi ile yote. | And the fame hereof went abroad into all that land. |
| 27 | Yesu aliondoka hapo, na alipokuwa anakwenda, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele, "Mwana wa Daudi, utuhurumie!" | And when Jesus departed thence, two blind men followed him, crying, and saying, Thou Son of David, have mercy on us. |
| 28 | Yesu alipoingia nyumbani, vipofu hao wawili wakamwendea, naye akawauliza, "Je, mnaamini kwamba naweza kuwafanyia jambo hilo?" Nao wakamjibu, "Naam, Mheshimiwa." | And when he was come into the house, the blind men came to him: and Jesus saith unto them, Believe ye that I am able to do this? They said unto him, Yea, Lord. |
| 29 | Hapo Yesu akayagusa macho yao, akasema, "Na iwe kwenu kama mnavyoamini." | Then touched he their eyes, saying, According to your faith be it unto you. |
| 30 | Macho yao yakafunguliwa. Naye Yesu akawaonya kwa ukali: "Msimwambie mtu yeyote jambo hili." | And their eyes were opened; and Jesus straitly charged them, saying, See that no man know it. |
| 31 | Lakini wao wakaondoka, wakaeneza habari za Yesu katika nchi ile yote. | But they, when they were departed, spread abroad his fame in all that country. |
| 32 | Watu walipokuwa wanakwenda zao, wengine walimletea Yesu mtu mmoja aliyekuwa bubu kwa sababu alikuwa amepagawa na pepo. | As they went out, behold, they brought to him a dumb man possessed with a devil. |
| 33 | Mara tu huyo pepo alipotolewa, mtu huyo aliyekuwa bubu akaanza kuongea tena. Watu wakashangaa na kusema, "Jambo kama hili halijapata kuonekana katika Israeli!" | And when the devil was cast out, the dumb spake: and the multitudes marvelled, saying, It was never so seen in Israel. |
| 34 | Lakini Mafarisayo wakawa wanasema, "Anawatoa pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo wabaya." | But the Pharisees said, He casteth out devils through the prince of the devils. |
| 35 | Yesu alitembelea miji yote na vijiji, akafundisha katika masunagogi yao akihubiri Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila namna. | And Jesus went about all the cities and villages, teaching in their synagogues, and preaching the gospel of the kingdom, and healing every sickness and every disease among the people. |
| 36 | Basi, alipowaona watu, makundi kwa makundi, aliwaonea huruma kwa sababu walikuwa hoi na wenye wasiwasi kama kondoo wasio na mchungaji. | But when he saw the multitudes, he was moved with compassion on them, because they fainted, and were scattered abroad, as sheep having no shepherd. |
| 37 | Hapo akawaambia wanafunzi wake, "Mavuno ni mengi, lakini wavunaji ni wachache. | Then saith he unto his disciples, The harvest truly is plenteous, but the labourers are few; |
| 38 | Kwa hivyo mwombeni mwenye shamba atume wavunaji shambani mwake." | Pray ye therefore the Lord of the harvest, that he will send forth labourers into his harvest. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL