마태복음 8장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 34절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makundi mengi ya watu yalimfuata. | When he was come down from the mountain, great multitudes followed him. |
| 2 | Basi, akaja mtu mmoja mwenye ukoma, akamsujudia akisema, "Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa!" | And, behold, there came a leper and worshipped him, saying, Lord, if thou wilt, thou canst make me clean. |
| 3 | Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa na kusema, "Nataka! Takasika." Mara huyo mtu akapona ukoma wake. | And Jesus put forth his hand, and touched him, saying, I will; be thou clean. And immediately his leprosy was cleansed. |
| 4 | Kisha Yesu akamwambia, "Sikiliza, usimwambie mtu yeyote, ila nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka iliyoamriwa na Mose kuwathibitishia kwamba umepona." | And Jesus saith unto him, See thou tell no man; but go thy way, shew thyself to the priest, and offer the gift that Moses commanded, for a testimony unto them. |
| 5 | Yesu alipokuwa anaingia mjini Kafarnaumu, ofisa mmoja Mroma alimwendea, akamsihi | And when Jesus was entered into Capernaum, there came unto him a centurion, beseeching him, |
| 6 | akisema, "Mheshimiwa, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza na anaumwa sana." | And saying, Lord, my servant lieth at home sick of the palsy, grievously tormented. |
| 7 | Yesu akamwambia, "Nitakuja kumponya." | And Jesus saith unto him, I will come and heal him. |
| 8 | Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, sistahili uingie nyumbani mwangu. Lakini sema tu neno, na mtumishi wangu atapona. | The centurion answered and said, Lord, I am not worthy that thou shouldest come under my roof: but speak the word only, and my servant shall be healed. |
| 9 | Maana, hata mimi niliye mtu chini ya mamlaka ya wengine, ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, Nenda! naye huenda; na mwingine, Njoo! naye huja; na mtumishi wangu, Fanya kitu hiki! naye hufanya." | For I am a man under authority, having soldiers under me: and I say to this man, Go, and he goeth; and to another, Come, and he cometh; and to my servant, Do this, and he doeth it. |
| 10 | Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia watu waliokuwa wanamfuata, "Kweli nawaambieni, sijapata kumwona mtu yeyote katika Israeli aliye na imani kama hii. | When Jesus heard it, he marvelled, and said to them that followed, Verily I say unto you, I have not found so great faith, no, not in Israel. |
| 11 | Basi, nawaambieni kwamba watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni. | And I say unto you, That many shall come from the east and west, and shall sit down with Abraham, and Isaac, and Jacob, in the kingdom of heaven. |
| 12 | Lakini wale ambao wangalipaswa kuwa katika Ufalme huo watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno." | But the children of the kingdom shall be cast out into outer darkness: there shall be weeping and gnashing of teeth. |
| 13 | Kisha Yesu akamwambia huyo ofisa Mroma, "Nenda nyumbani; na iwe kama ulivyoamini." Na mtumishi wake akapona saa ileile. | And Jesus said unto the centurion, Go thy way; and as thou hast believed, so be it done unto thee. And his servant was healed in the selfsame hour. |
| 14 | Yesu alifika nyumbani kwa Petro, akamkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, ana homa kali. | And when Jesus was come into Peter’s house, he saw his wife’s mother laid, and sick of a fever. |
| 15 | Basi, Yesu akamgusa huyo mama mkono, na homa ikamwacha; akasimama, akamtumikia. | And he touched her hand, and the fever left her: and she arose, and ministered unto them. |
| 16 | Ilipokuwa jioni, walimletea watu wengi waliokuwa wamepagawa na pepo; naye, kwa kusema neno tu, akawafukuza hao pepo. Aliwaponya pia watu wote waliokuwa wagonjwa. | When the even was come, they brought unto him many that were possessed with devils: and he cast out the spirits with his word, and healed all that were sick: |
| 17 | Alifanya hivyo ili yale aliyosema nabii Isaya yatimie: "Yeye mwenyewe ameondoa udhaifu wetu, ameyachukua magonjwa yetu." | That it might be fulfilled which was spoken by Esaias the prophet, saying, Himself took our infirmities, and bare our sicknesses. |
| 18 | Yesu alipoona kundi la watu limemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake waende ng'ambo ya ziwa. | Now when Jesus saw great multitudes about him, he gave commandment to depart unto the other side. |
| 19 | Mwalimu mmoja wa Sheria akamwendea, akamwambia, "Mwalimu, mimi nitakufuata kokote uendako." | And a certain scribe came, and said unto him, Master, I will follow thee whithersoever thou goest. |
| 20 | Yesu akamjibu, "Mbweha wana mapango, na ndege wana viota; lakini Mwana wa Mtu hana mahali pa kupumzikia." | And Jesus saith unto him, The foxes have holes, and the birds of the air have nests; but the Son of man hath not where to lay his head. |
| 21 | Kisha mtu mwingine miongoni mwa wanafunzi wake akamwambia, "Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzike baba yangu." | And another of his disciples said unto him, Lord, suffer me first to go and bury my father. |
| 22 | Lakini Yesu akamwambia, "Nifuate! Waache wafu wazike wafu wao." | But Jesus said unto him, Follow me; and let the dead bury their dead. |
| 23 | Yesu alipanda mashua, na wanafunzi wake wakaenda pamoja naye. | And when he was entered into a ship, his disciples followed him. |
| 24 | Ghafla, dhoruba kali ikatokea ziwani, hata mawimbi yakaanza kuifunika mashua. Yesu alikuwa amelala usingizi. | And, behold, there arose a great tempest in the sea, insomuch that the ship was covered with the waves: but he was asleep. |
| 25 | Wanafunzi wakamwendea, wakamwamsha wakisema, "Bwana, tuokoe, tunaangamia!" | And his disciples came to him, and awoke him, saying, Lord, save us: we perish. |
| 26 | Yesu akawaambia, "Enyi watu wenye imani haba; mbona mnaogopa?" Basi, akainuka, akazikemea pepo na mawimbi; kukawa shwari kabisa. | And he saith unto them, Why are ye fearful, O ye of little faith? Then he arose, and rebuked the winds and the sea; and there was a great calm. |
| 27 | Watu wakashangaa, wakasema, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na mawimbi vinamtii!" | But the men marvelled, saying, What manner of man is this, that even the winds and the sea obey him! |
| 28 | Yesu alifika katika nchi ya Wagerasi, ng'ambo ya ziwa, na huko watu wawili waliopagawa na pepo wakakutana naye wakitokea makaburini. Watu hawa walikuwa wenye kutisha mno, hata hakuna mtu aliyethubutu kupita katika njia hiyo. | And when he was come to the other side into the country of the Gergesenes, there met him two possessed with devils, coming out of the tombs, exceeding fierce, so that no man might pass by that way. |
| 29 | Nao wakaanza kupiga kelele, "Una shauri gani nasi, wewe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya wakati wake?" | And, behold, they cried out, saying, What have we to do with thee, Jesus, thou Son of God? art thou come hither to torment us before the time? |
| 30 | Karibu na mahali hapo kulikuwa na nguruwe wengi wakichungwa. | And there was a good way off from them an herd of many swine feeding. |
| 31 | Basi, hao pepo wakamsihi, "Ikiwa utatutoa, basi uturuhusu tuwaingie nguruwe wale." | So the devils besought him, saying, If thou cast us out, suffer us to go away into the herd of swine. |
| 32 | Yesu akawaambia, "Haya, nendeni." Hapo wakawatoka watu hao, wakawaingia nguruwe. Kundi lote la nguruwe likaporomoka kwenye ule mteremko mkali, likatumbukia ziwani; nguruwe wote wakafa maji. | And he said unto them, Go. And when they were come out, they went into the herd of swine: and, behold, the whole herd of swine ran violently down a steep place into the sea, and perished in the waters. |
| 33 | Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakaenda mjini. Huko walitoa habari zote na mambo yaliyowapata wale watu waliokuwa wamepagawa. | And they that kept them fled, and went their ways into the city, and told every thing, and what was befallen to the possessed of the devils. |
| 34 | Basi, watu wote katika mji ule walitoka, wakamwendea Yesu; na walipomwona, wakamsihi aondoke katika nchi yao. | And, behold, the whole city came out to meet Jesus: and when they saw him, they besought him that he would depart out of their coasts. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL