로그인

마태복음 27장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 66절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Kulipopambazuka, makuhani wakuu wote na wazee wa watu walifanya mashauri juu ya Yesu wapate kumwua. When the morning was come, all the chief priests and elders of the people took counsel against Jesus to put him to death:
2 Wakamfunga pingu, wakamchukua, wakamkabidhi kwa Pilato, mkuu wa mkoa. And when they had bound him, they led him away, and delivered him to Pontius Pilate the governor.
3 Hapo, Yuda ambaye ndiye aliyemsaliti, alipoona kwamba wamekwisha mhukumu Yesu, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu zile sarafu thelathini za fedha. Then Judas, which had betrayed him, when he saw that he was condemned, repented himself, and brought again the thirty pieces of silver to the chief priests and elders,
4 Akawaambia, "Nimekosa kwa kumtoa mtu asiye na hatia auawe." Lakini wao wakasema, "Yatuhusu nini sisi? Hilo ni shauri lako." Saying, I have sinned in that I have betrayed the innocent blood. And they said, What is that to us? see thou to that.
5 Naye akazitupa zile fedha Hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga. And he cast down the pieces of silver in the temple, and departed, and went and hanged himself.
6 Makuhani wakuu wakazichukua zile fedha, wakasema, "Haifai kuziweka katika hazina ya Hekalu kwa maana ni fedha za damu." And the chief priests took the silver pieces, and said, It is not lawful for to put them into the treasury, because it is the price of blood.
7 Basi, wakashauriana, wakazitumia kununua shamba la mfinyanzi liwe mahali pa kuzika wageni. And they took counsel, and bought with them the potter’s field, to bury strangers in.
8 Ndiyo maana mpaka leo shamba hilo linaitwa Shamba la Damu. Wherefore that field was called, The field of blood, unto this day.
9 Hivyo maneno ya nabii Yeremia yakatimia: "Walizichukua sarafu thelathini za fedha, thamani ya yule ambaye watu wa Israeli walipanga bei, Then was fulfilled that which was spoken by Jeremy the prophet, saying, And they took the thirty pieces of silver, the price of him that was valued, whom they of the children of Israel did value;
10 wakanunua nazo shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyoniagiza." And gave them for the potter’s field, as the Lord appointed me.
11 Yesu alisimamishwa mbele ya mkuu wa mkoa. Basi, mkuu wa mkoa akamwuliza, "Je, wewe ndiwe Mfalme wa Wayahudi?" Yesu akamwambia, "Wewe umesema." And Jesus stood before the governor: and the governor asked him, saying, Art thou the King of the Jews? And Jesus said unto him, Thou sayest.
12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipokuwa wanamshtaki, hakujibu neno. And when he was accused of the chief priests and elders, he answered nothing.
13 Hivyo Pilato akamwuliza, "Je, husikii mashtaka hayo yote wanayotoa juu yako?" Then said Pilate unto him, Hearest thou not how many things they witness against thee?
14 Lakini Yesu hakumjibu hata neno moja; hata huyo mkuu wa mkoa akashangaa sana. And he answered him to never a word; insomuch that the governor marvelled greatly.
15 Ilikuwa kawaida wakati wa Sikukuu ya Pasaka mkuu wa mkoa kuwafungulia Wayahudi mfungwa mmoja waliyemtaka. Now at that feast the governor was wont to release unto the people a prisoner, whom they would.
16 Wakati huo kulikuwa na mfungwa mmoja, jina lake Baraba. And they had then a notable prisoner, called Barabbas.
17 Hivyo, watu walipokusanyika pamoja, Pilato akawauliza, "Mwataka nimfungue yupi kati ya wawili hawa, Baraba ama Yesu aitwae Kristo?" Therefore when they were gathered together, Pilate said unto them, Whom will ye that I release unto you? Barabbas, or Jesus which is called Christ?
18 Alisema hivyo maana alijua wazi kwamba walimleta kwake kwa sababu ya wivu. For he knew that for envy they had delivered him.
19 Pilato alipokuwa amekaa katika kiti cha hukumu, mke wake akampelekea ujumbe: "Usijitie katika shauri la mtu huyu mwema, maana leo nimeteseka sana katika ndoto kwa sababu yake." When he was set down on the judgment seat, his wife sent unto him, saying, Have thou nothing to do with that just man: for I have suffered many things this day in a dream because of him.
20 Lakini makuhani wakuu na wazee wakawashawishi watu waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe. But the chief priests and elders persuaded the multitude that they should ask Barabbas, and destroy Jesus.
21 Mkuu wa mkoa akawauliza, "Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka nimfungue?" Wakamjibu, "Baraba!" The governor answered and said unto them, Whether of the twain will ye that I release unto you? They said, Barabbas.
22 Pilato akawauliza, "Sasa, nifanye nini na Yesu aitwaye Kristo?" Wote wakasema, "Asulubiwe!" Pilate saith unto them, What shall I do then with Jesus which is called Christ? They all say unto him, Let him be crucified.
23 Pilato akauliza, "Kwa nini? Amefanya kosa gani?" Wao wakazidi kupaaza sauti: "Asulubiwe!" And the governor said, Why, what evil hath he done? But they cried out the more, saying, Let him be crucified.
24 Basi, Pilato alipotambua kwamba hafanikiwi chochote na kwamba maasi yalikuwa yanaanza, alichukua maji, akanawa mikono mbele ya ule umati wa watu, akasema, "Mimi sina lawama juu ya kifo cha mtu huyu; shauri lenu wenyewe." When Pilate saw that he could prevail nothing, but that rather a tumult was made, he took water, and washed his hands before the multitude, saying, I am innocent of the blood of this just person: see ye to it.
25 Watu wote wakasema, "Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!" Then answered all the people, and said, His blood be on us, and on our children.
26 Hapo Pilato akawafungulia Baraba kutoka gerezani, lakini akamtoa Yesu asulubiwe. Then released he Barabbas unto them: and when he had scourged Jesus, he delivered him to be crucified.
27 Kisha askari wa mkuu wa mkoa wakamwingiza Yesu ndani ya ikulu, wakamkusanyikia kikosi kizima. Then the soldiers of the governor took Jesus into the common hall, and gathered unto him the whole band of soldiers.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika joho la rangi nyekundu. And they stripped him, and put on him a scarlet robe.
29 Kisha wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani, wakamwekea pia mwanzi katika mkono wake wa kulia. Wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki wakisema, "Shikamoo mfalme wa Wayahudi!" And when they had platted a crown of thorns, they put it upon his head, and a reed in his right hand: and they bowed the knee before him, and mocked him, saying, Hail, King of the Jews!
30 Wakamtemea mate, wakauchukua ule mwanzi, wakampiga nao kichwani. And they spit upon him, and took the reed, and smote him on the head.
31 Baada ya kumdhihaki, wakamvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha. And after that they had mocked him, they took the robe off from him, and put his own raiment on him, and led him away to crucify him.
32 Walipokuwa wakienda, wakamkuta mtu mmoja jina lake Simoni, mwenyeji wa Kurene, wakamlazimisha kuuchukua msalaba wake Yesu. And as they came out, they found a man of Cyrene, Simon by name: him they compelled to bear his cross.
33 Walipofika mahali paitwapo Golgotha, maana yake, "Mahali pa Fuvu la kichwa," And when they were come unto a place called Golgotha, that is to say, a place of a skull,
34 wakampa mchanganyiko wa divai na nyongo. Lakini Yesu alipoonja akakataa kunywa. They gave him vinegar to drink mingled with gall: and when he had tasted thereof, he would not drink.
35 Walimsulubisha, kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura. And they crucified him, and parted his garments, casting lots: that it might be fulfilled which was spoken by the prophet, They parted my garments among them, and upon my vesture did they cast lots.
36 Wakaketi, wakawa wanamchunga. And sitting down they watched him there;
37 Juu ya kichwa chake wakaweka shtaka dhidi yake lilioandikwa, "Huyu ni Yesu, Mfalme wa Wayahudi." And set up over his head his accusation written, THIS IS JESUS THE KING OF THE JEWS.
38 Wanyang'anyi wawili walisulubishwa pia pamoja naye, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia. Then were there two thieves crucified with him, one on the right hand, and another on the left.
39 Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana wakitikisa vichwa vyao na kusema, And they that passed by reviled him, wagging their heads,
40 "Wewe! Si ulijidai kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Sasa jiokoe mwenyewe. Kama wewe ni Mwana wa Mungu, basi shuka msalabani!" And saying, Thou that destroyest the temple, and buildest it in three days, save thyself. If thou be the Son of God, come down from the cross.
41 Hali kadhalika na makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria na wazee walimdhihaki wakisema, Likewise also the chief priests mocking him, with the scribes and elders, said,
42 "Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi! Eti yeye ni mfalme wa Wayahudi! Basi, sasa na ashuke msalabani, nasi tutamwamini. He saved others; himself he cannot save. If he be the King of Israel, let him now come down from the cross, and we will believe him.
43 Alimtumainia Mungu na kusema eti yeye ni Mwana wa Mungu; basi, Mungu na amwokoe kama anamtaka." He trusted in God; let him deliver him now, if he will have him: for he said, I am the Son of God.
44 Hali kadhalika na wale waliosulubiwa pamoja naye wakamtukana. The thieves also, which were crucified with him, cast the same in his teeth.
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza. Now from the sixth hour there was darkness over all the land unto the ninth hour.
46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eli, Eli, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" And about the ninth hour Jesus cried with a loud voice, saying, Eli, Eli, lama sabachthani? that is to say, My God, my God, why hast thou forsaken me?
47 Lakini wale waliosimama pale waliposikia hivyo wakasema, "Anamwita Eliya." Some of them that stood there, when they heard that, said, This man calleth for Elias.
48 Mmoja wao akakimbia, akachukua sifongo, akaichovya katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe. And straightway one of them ran, and took a spunge, and filled it with vinegar, and put it on a reed, and gave him to drink.
49 Wengine wakasema, "Acha tuone kama Eliya anakuja kumwokoa." The rest said, Let be, let us see whether Elias will come to save him.
50 Basi, Yesu akalia tena kwa sauti kubwa, akakata roho. Jesus, when he had cried again with a loud voice, yielded up the ghost.
51 Hapo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, toka juu mpaka chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; And, behold, the veil of the temple was rent in twain from the top to the bottom; and the earth did quake, and the rocks rent;
52 makaburi yakafunguka na watu wengi wa Mungu waliokufa wakafufuliwa; And the graves were opened; and many bodies of the saints which slept arose,
53 nao, baada ya kufufuka kwake, wakatoka makaburini, wakaingia katika Mji Mtakatifu, wakaonekana na watu wengi. And came out of the graves after his resurrection, and went into the holy city, and appeared unto many.
54 Basi, jemadari na wale waliokuwa wakimlinda Yesu walipoona tetemeko la ardhi na yale mambo yaliyotukia, wakaogopa sana, wakasema, "Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu." Now when the centurion, and they that were with him, watching Jesus, saw the earthquake, and those things that were done, they feared greatly, saying, Truly this was the Son of God.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. And many women were there beholding afar off, which followed Jesus from Galilee, ministering unto him:
56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. Among which was Mary Magdalene, and Mary the mother of James and Joses, and the mother of Zebedee’s children.
57 Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. When the even was come, there came a rich man of Arimathea, named Joseph, who also himself was Jesus’ disciple:
58 Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe. He went to Pilate, and begged the body of Jesus. Then Pilate commanded the body to be delivered.
59 Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani, And when Joseph had taken the body, he wrapped it in a clean linen cloth,
60 akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake. And laid it in his own new tomb, which he had hewn out in the rock: and he rolled a great stone to the door of the sepulchre, and departed.
61 Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwa wameketi kulielekea kaburi. And there was Mary Magdalene, and the other Mary, sitting over against the sepulchre.
62 Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalio, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato, Now the next day, that followed the day of the preparation, the chief priests and Pharisees came together unto Pilate,
63 Wakasema, "Mheshimiwa, tunakumbuka kwamba yule mdanganyifu alisema kabla ya kufa ati, Baada ya siku tatu nitafufuka. Saying, Sir, we remember that that deceiver said, while he was yet alive, After three days I will rise again.
64 Kwa hiyo amuru kaburi lilindwe mpaka siku ya tatu ili wanafunzi wake wasije wakamwiba na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa awali." Command therefore that the sepulchre be made sure until the third day, lest his disciples come by night, and steal him away, and say unto the people, He is risen from the dead: so the last error shall be worse than the first.
65 Pilato akawaambia, "Haya, mnao walinzi; nendeni mkalinde kadiri mjuavyo." Pilate said unto them, Ye have a watch: go your way, make it as sure as ye can.
66 Basi, wakaenda, wakalilinda kaburi, wakatia mhuri juu ya lile jiwe na kuacha hapo askari walinzi. So they went, and made the sepulchre sure, sealing the stone, and setting a watch.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL