마태복음 26장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 75절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, | And it came to pass, when Jesus had finished all these sayings, he said unto his disciples, |
| 2 | "Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe." | Ye know that after two days is the feast of the passover, and the Son of man is betrayed to be crucified. |
| 3 | Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, Kuhani Mkuu. | Then assembled together the chief priests, and the scribes, and the elders of the people, unto the palace of the high priest, who was called Caiaphas, |
| 4 | Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue. | And consulted that they might take Jesus by subtilty, and kill him. |
| 5 | Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu. | But they said, Not on the feast day, lest there be an uproar among the people. |
| 6 | Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma, | Now when Jesus was in Bethany, in the house of Simon the leper, |
| 7 | mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani. | There came unto him a woman having an alabaster box of very precious ointment, and poured it on his head, as he sat at meat. |
| 8 | Wanafunzi wake walipoona hayo wakakasirika, wakasema, "Ya nini hasara hii? | But when his disciples saw it, they had indignation, saying, To what purpose is this waste? |
| 9 | Marashi haya yangaliweza kuuzwa kwa bei kubwa, maskini wakapewa hizo fedha." | For this ointment might have been sold for much, and given to the poor. |
| 10 | Yesu alitambua mawazo yao, akawaambia, "Mbona mnamsumbua huyu mama? Yeye amenitendea jambo jema. | When Jesus understood it, he said unto them, Why trouble ye the woman? for she hath wrought a good work upon me. |
| 11 | Maskini mnao daima pamoja nanyi, lakini mimi sitakuwapo pamoja nanyi daima. | For ye have the poor always with you; but me ye have not always. |
| 12 | Huyu mama amenimiminia marashi ili kunitayarisha kwa maziko. | For in that she hath poured this ointment on my body, she did it for my burial. |
| 13 | Nawaambieni kweli, popote ambapo hii Habari Njema itahubiriwa ulimwenguni, kitendo hiki alichofanya mama huyu kitatajwa kwa kumkumbuka yeye." | Verily I say unto you, Wheresoever this gospel shall be preached in the whole world, there shall also this, that this woman hath done, be told for a memorial of her. |
| 14 | Kisha, Yuda Iskarioti, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu, | Then one of the twelve, called Judas Iscariot, went unto the chief priests, |
| 15 | akawaambia, "Mtanipa kitu gani kama nikimkabidhi Yesu kwenu?" Wakamhesabia sarafu thelathini za fedha; | And said unto them, What will ye give me, and I will deliver him unto you? And they covenanted with him for thirty pieces of silver. |
| 16 | na tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti. | And from that time he sought opportunity to betray him. |
| 17 | Siku ya kwanza kabla ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wanafunzi walimwendea Yesu wakamwuliza, "Unataka tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?" | Now the first day of the feast of unleavened bread the disciples came to Jesus, saying unto him, Where wilt thou that we prepare for thee to eat the passover? |
| 18 | Yeye akawajibu, "Nendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie: Mwalimu anasema, wakati wangu umefika; kwako nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu." | And he said, Go into the city to such a man, and say unto him, The Master saith, My time is at hand; I will keep the passover at thy house with my disciples. |
| 19 | Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaandaa Pasaka. | And the disciples did as Jesus had appointed them; and they made ready the passover. |
| 20 | Kulipokuwa jioni, Yesu akakaa mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. | Now when the even was come, he sat down with the twelve. |
| 21 | Walipokuwa wakila, Yesu akasema, "Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti." | And as they did eat, he said, Verily I say unto you, that one of you shall betray me. |
| 22 | Wanafunzi wakahuzunika sana, wakaanza kuuliza mmojammoja, "Bwana! Je, ni mimi?" | And they were exceeding sorrowful, and began every one of them to say unto him, Lord, is it I? |
| 23 | Yesu akajibu, "Atakayechovya mkate pamoja nami katika bakuli ndiye atakayenisaliti. | And he answered and said, He that dippeth his hand with me in the dish, the same shall betray me. |
| 24 | Naam, Mwana wa Mtu anakwenda zake kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, lakini ole wake mtu yule atakayemsaliti Mwana wa Mtu! Ingalikuwa afadhali kwa mtu huyo kama hangalizaliwa." | The Son of man goeth as it is written of him: but woe unto that man by whom the Son of man is betrayed! it had been good for that man if he had not been born. |
| 25 | Yuda, ambaye ndiye aliyetaka kumsaliti, akamwuliza, "Mwalimu! Je, ni mimi?" Yesu akamjibu, "Wewe umesema." | Then Judas, which betrayed him, answered and said, Master, is it I? He said unto him, Thou hast said. |
| 26 | Walipokuwa wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, "Twaeni mle; huu ni mwili wangu." | And as they were eating, Jesus took bread, and blessed it, and brake it, and gave it to the disciples, and said, Take, eat; this is my body. |
| 27 | Kisha akatwaa kikombe, akamshukuru Mungu, akawapa akisema, "Nyweni nyote; | And he took the cup, and gave thanks, and gave it to them, saying, Drink ye all of it; |
| 28 | maana hii ni damu yangu inayothibitisha agano, damu inayomwagwa kwa ajili ya watu wengi ili kuwaondolea dhambi. | For this is my blood of the new testament, which is shed for many for the remission of sins. |
| 29 | Nawaambieni, sitakunywa tena divai ya zabibu mpaka siku ile nitakapoinywa mpya pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu." | But I say unto you, I will not drink henceforth of this fruit of the vine, until that day when I drink it new with you in my Father’s kingdom. |
| 30 | Baada ya kuimba wimbo, wakaondoka, wakaenda katika mlima wa Mizeituni. | And when they had sung an hymn, they went out into the mount of Olives. |
| 31 | Kisha Yesu akawaambia, "Usiku huu wa leo, ninyi nyote mtakuwa na mashaka nami, maana Maandiko Matakatifu yasema: Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika. | Then saith Jesus unto them, All ye shall be offended because of me this night: for it is written, I will smite the shepherd, and the sheep of the flock shall be scattered abroad. |
| 32 | Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulieni Galilaya." | But after I am risen again, I will go before you into Galilee. |
| 33 | Petro akamwambia Yesu "Hata kama wote watakuwa na mashaka nawe na kukuacha, mimi sitakuacha kamwe." | Peter answered and said unto him, Though all men shall be offended because of thee, yet will I never be offended. |
| 34 | Yesu akamwambia, "Kweli nakwambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." | Jesus said unto him, Verily I say unto thee, That this night, before the cock crow, thou shalt deny me thrice. |
| 35 | Petro akamwambia, "Hata kama ni lazima nife pamoja nawe, sitakukana kamwe." Wale wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo. | Peter said unto him, Though I should die with thee, yet will I not deny thee. Likewise also said all the disciples. |
| 36 | Kisha Yesu akaenda pamoja nao bustanini Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, "Kaeni hapa nami niende pale mbele kusali." | Then cometh Jesus with them unto a place called Gethsemane, and saith unto the disciples, Sit ye here, while I go and pray yonder. |
| 37 | Akawachukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuwa na huzuni na mahangaiko. | And he took with him Peter and the two sons of Zebedee, and began to be sorrowful and very heavy. |
| 38 | Hapo akawaambia, "Nina huzuni kubwa moyoni hata karibu kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami." | Then saith he unto them, My soul is exceeding sorrowful, even unto death: tarry ye here, and watch with me. |
| 39 | Basi, akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akasali: "Baba yangu, kama inawezekana, aacha kikombe hiki cha mateso kinipite; lakini isiwe nitakavyo mimi, ila utakavyo wewe." | And he went a little further, and fell on his face, and prayed, saying, O my Father, if it be possible, let this cup pass from me: nevertheless not as I will, but as thou wilt. |
| 40 | Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, "Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? | And he cometh unto the disciples, and findeth them asleep, and saith unto Peter, What, could ye not watch with me one hour? |
| 41 | Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu." | Watch and pray, that ye enter not into temptation: the spirit indeed is willing, but the flesh is weak. |
| 42 | Akaenda tena mara ya pili akasali: "Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kinipite bila mimi kukinywa, basi, mapenzi yako yafanyike." | He went away again the second time, and prayed, saying, O my Father, if this cup may not pass away from me, except I drink it, thy will be done. |
| 43 | Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. | And he came and found them asleep again: for their eyes were heavy. |
| 44 | Basi, akawaacha, akaenda tena kusali mara ya tatu kwa maneno yaleyale. | And he left them, and went away again, and prayed the third time, saying the same words. |
| 45 | Kisha akawaendea wale wanafunzi, akawaambia, "Je, mngali mmelala na kupumzika? Tazameni! Saa yenyewe imefika, na Mwana wa Mtu atatolewa kwa watu wenye dhambi. | Then cometh he to his disciples, and saith unto them, Sleep on now, and take your rest: behold, the hour is at hand, and the Son of man is betrayed into the hands of sinners. |
| 46 | Amkeni, twendeni zetu. Tazameni! Anakuja yule atakayenisaliti." | Rise, let us be going: behold, he is at hand that doth betray me. |
| 47 | Basi, Yesu alipokuwa bado anasema nao, mara akaja Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili. Pamoja naye walikuja watu wengi wenye mapanga na marungu ambao walitumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu. | And while he yet spake, lo, Judas, one of the twelve, came, and with him a great multitude with swords and staves, from the chief priests and elders of the people. |
| 48 | Huyo aliyetaka kumsaliti Yesu, alikuwa amekwisha wapa ishara akisema: "Yule nitakayembusu ndiye; mkamateni." | Now he that betrayed him gave them a sign, saying, Whomsoever I shall kiss, that same is he: hold him fast. |
| 49 | Basi, Yuda akamkaribia Yesu, akamwambia, "Shikamoo, Mwalimu!" Kisha akambusu. | And forthwith he came to Jesus, and said, Hail, master; and kissed him. |
| 50 | Yesu akamwambia, "Rafiki, fanya ulichokuja kufanya." Hapo wale watu wakaja, wakamkamata Yesu, wakamtia nguvuni. | And Jesus said unto him, Friend, wherefore art thou come? Then came they, and laid hands on Jesus, and took him. |
| 51 | Mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono, akauchomoa upanga wake, akampiga mtumishi wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. | And, behold, one of them which were with Jesus stretched out his hand, and drew his sword, and struck a servant of the high priest’s, and smote off his ear. |
| 52 | Hapo Yesu akamwambia, "Rudisha upanga wako alani, maana yeyote anayeutumia upanga, atakufa kwa upanga. | Then said Jesus unto him, Put up again thy sword into his place: for all they that take the sword shall perish with the sword. |
| 53 | Je, hamjui kwamba ningeweza kumwomba Baba yangu naye mara angeniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? | Thinkest thou that I cannot now pray to my Father, and he shall presently give me more than twelve legions of angels? |
| 54 | Lakini yatatimiaje Maandiko Matakatifu yasemayo kwamba ndivyo inavyopaswa kuwa?" | But how then shall the scriptures be fulfilled, that thus it must be? |
| 55 | Wakati huohuo Yesu akauambia huo umati wa watu waliokuja kumtia nguvuni, "Je, mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama kwamba mimi ni mnyang'anyi? Kila siku nilikuwa Hekaluni nikifundisha, na hamkunikamata! | In that same hour said Jesus to the multitudes, Are ye come out as against a thief with swords and staves for to take me? I sat daily with you teaching in the temple, and ye laid no hold on me. |
| 56 | Lakini haya yote yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie." Kisha wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia. | But all this was done, that the scriptures of the prophets might be fulfilled. Then all the disciples forsook him, and fled. |
| 57 | Basi, hao watu waliomkamata Yesu walimpeleka nyumbani kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokusanyika walimu wa Sheria na wazee. | And they that had laid hold on Jesus led him away to Caiaphas the high priest, where the scribes and the elders were assembled. |
| 58 | Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa Kuhani Mkuu, akaingia ndani pamoja na walinzi ili apate kuona mambo yatakavyokuwa. | But Peter followed him afar off unto the high priest’s palace, and went in, and sat with the servants, to see the end. |
| 59 | Basi, makuhani wakuu na Baraza lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu wapate kumwua, | Now the chief priests, and elders, and all the council, sought false witness against Jesus, to put him to death; |
| 60 | lakini hawakupata ushahidi wowote, ingawa walikuja mashahidi wengi wa uongo. Mwishowe wakaja mashahidi wawili, | But found none: yea, though many false witnesses came, yet found they none. At the last came two false witnesses, |
| 61 | wakasema, "Mtu huyu alisema: Ninaweza kuliharibu Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu." | And said, This fellow said, I am able to destroy the temple of God, and to build it in three days. |
| 62 | Kuhani Mkuu akasimama, akamwuliza Yesu, "Je, hujibu neno? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?" | And the high priest arose, and said unto him, Answerest thou nothing? what is it which these witness against thee? |
| 63 | Lakini Yesu akakaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, "Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, twambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu!" | But Jesus held his peace. And the high priest answered and said unto him, I adjure thee by the living God, that thou tell us whether thou be the Christ, the Son of God. |
| 64 | Yesu akamwambia, "Wewe umesema! Lakini nawaambieni, tangu sasa mtamwona Mwana wa Mtu ameketi upande wa kulia wa Mwenyezi, akija juu ya mawingu ya mbinguni." | Jesus saith unto him, Thou hast said: nevertheless I say unto you, Hereafter shall ye see the Son of man sitting on the right hand of power, and coming in the clouds of heaven. |
| 65 | Hapo, Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, "Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi? Sasa mmesikia kufuru yake. | Then the high priest rent his clothes, saying, He hath spoken blasphemy; what further need have we of witnesses? behold, now ye have heard his blasphemy. |
| 66 | Ninyi mwaonaje?" Wao wakamjibu, "Anastahili kufa!" | What think ye? They answered and said, He is guilty of death. |
| 67 | Kisha wakamtemea mate usoni, wakampiga makofi. Wengine wakiwa wanampiga makofi, | Then did they spit in his face, and buffeted him; and others smote him with the palms of their hands, |
| 68 | wakasema, "Haya Kristo, tutabirie; ni nani amekupiga!" | Saying, Prophesy unto us, thou Christ, Who is he that smote thee? |
| 69 | Petro alikuwa ameketi nje uani. Basi, mtumishi mmoja wa kike akamwendea, akasema, "Wewe ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya." | Now Peter sat without in the palace: and a damsel came unto him, saying, Thou also wast with Jesus of Galilee. |
| 70 | Petro akakana mbele ya wote akisema, "Sijui hata unasema nini." | But he denied before them all, saying, I know not what thou sayest. |
| 71 | Alipokuwa akitoka mlangoni, mtumishi mwingine wa kike akamwona, akawaambia wale waliokuwa pale, "Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti." | And when he was gone out into the porch, another maid saw him, and said unto them that were there, This fellow was also with Jesus of Nazareth. |
| 72 | Petro akakana tena kwa kiapo: "Simjui mtu huyo." | And again he denied with an oath, I do not know the man. |
| 73 | Baadaye kidogo, watu waliokuwa pale wakamwendea Petro, wakamwambia, "Hakika, wewe pia ni mmoja wao, maana msemo wako unakutambulisha." | And after a while came unto him they that stood by, and said to Peter, Surely thou also art one of them; for thy speech bewrayeth thee. |
| 74 | Hapo Petro akaanza kujilaani na kuapa akisema, "Simjui mtu huyo!" Mara jogoo akawika. | Then began he to curse and to swear, saying, I know not the man. And immediately the cock crew. |
| 75 | Petro akakumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu: "Kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu." Basi, akatoka nje akalia sana. | And Peter remembered the word of Jesus, which said unto him, Before the cock crow, thou shalt deny me thrice. And he went out, and wept bitterly. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL