마태복음 14장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 36절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu. | At that time Herod the tetrarch heard of the fame of Jesus, |
| 2 | Basi, akawaambia watumishi wake, "Mtu huyu ni Yohane mbatizaji, amefufuka kutoka wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake." | And said unto his servants, This is John the Baptist; he is risen from the dead; and therefore mighty works do shew forth themselves in him. |
| 3 | Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake. Sababu hasa ni | For Herod had laid hold on John, and bound him, and put him in prison for Herodias’ sake, his brother Philip’s wife. |
| 4 | kwamba alikuwa amemwambia Herode, "Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!" | For John said unto him, It is not lawful for thee to have her. |
| 5 | Herode alitaka kumwua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii. | And when he would have put him to death, he feared the multitude, because they counted him as a prophet. |
| 6 | Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa, | But when Herod’s birthday was kept, the daughter of Herodias danced before them, and pleased Herod. |
| 7 | hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba. | Whereupon he promised with an oath to give her whatsoever she would ask. |
| 8 | Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, "Nipe papahapa katika sinia kichwa cha Yohane mbatizaji." | And she, being before instructed of her mother, said, Give me here John Baptist’s head in a charger. |
| 9 | Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe. | And the king was sorry: nevertheless for the oath’s sake, and them which sat with him at meat, he commanded it to be given her. |
| 10 | Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane. | And he sent, and beheaded John in the prison. |
| 11 | Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake. | And his head was brought in a charger, and given to the damsel: and she brought it to her mother. |
| 12 | Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu. | And his disciples came, and took up the body, and buried it, and went and told Jesus. |
| 13 | Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini. | When Jesus heard of it, he departed thence by ship into a desert place apart: and when the people had heard thereof, they followed him on foot out of the cities. |
| 14 | Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao. | And Jesus went forth, and saw a great multitude, and was moved with compassion toward them, and he healed their sick. |
| 15 | Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na saa zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula." | And when it was evening, his disciples came to him, saying, This is a desert place, and the time is now past; send the multitude away, that they may go into the villages, and buy themselves victuals. |
| 16 | Yesu akawaambia, "Si lazima waende, wapeni ninyi chakula." | But Jesus said unto them, They need not depart; give ye them to eat. |
| 17 | Lakini wao wakamwambia, "Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili." | And they say unto him, We have here but five loaves, and two fishes. |
| 18 | Yesu akawaambia, "Nileteeni hapa." | He said, Bring them hither to me. |
| 19 | Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akamshukuru Mungu. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. | And he commanded the multitude to sit down on the grass, and took the five loaves, and the two fishes, and looking up to heaven, he blessed, and brake, and gave the loaves to his disciples, and the disciples to the multitude. |
| 20 | Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. | And they did all eat, and were filled: and they took up of the fragments that remained twelve baskets full. |
| 21 | Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto. | And they that had eaten were about five thousand men, beside women and children. |
| 22 | Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ng'ambo ya ziwa wakati yeye anawaaga watu. | And straightway Jesus constrained his disciples to get into a ship, and to go before him unto the other side, while he sent the multitudes away. |
| 23 | Baada ya kuwaaga, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa jioni, yeye alikuwa huko peke yake, | And when he had sent the multitudes away, he went up into a mountain apart to pray: and when the evening was come, he was there alone. |
| 24 | na wakati huo ile mashua ilikwishafika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikuwa inakwenda mrama kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga. | But the ship was now in the midst of the sea, tossed with waves: for the wind was contrary. |
| 25 | Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji. | And in the fourth watch of the night Jesus went unto them, walking on the sea. |
| 26 | Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliingiwa na hofu, wakasema, "Ni mzimu!" Wakapiga kelele kwa hofu. | And when the disciples saw him walking on the sea, they were troubled, saying, It is a spirit; and they cried out for fear. |
| 27 | Mara, Yesu akasema nao, "Tulieni, ni mimi. Msiogope!" | But straightway Jesus spake unto them, saying, Be of good cheer; it is I; be not afraid. |
| 28 | Petro akamwambia, "Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako." | And Peter answered him and said, Lord, if it be thou, bid me come unto thee on the water. |
| 29 | Yesu akasema, "Haya, njoo." Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu. | And he said, Come. And when Peter was come down out of the ship, he walked on the water, to go to Jesus. |
| 30 | Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, "Bwana, niokoe!" | But when he saw the wind boisterous, he was afraid; and beginning to sink, he cried, saying, Lord, save me. |
| 31 | Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, "Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?" | And immediately Jesus stretched forth his hand, and caught him, and said unto him, O thou of little faith, wherefore didst thou doubt? |
| 32 | Basi, wakapanda mashuani, na upepo ukatulia. | And when they were come into the ship, the wind ceased. |
| 33 | Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, "Hakika wewe ni Mwana wa Mungu." | Then they that were in the ship came and worshipped him, saying, Of a truth thou art the Son of God. |
| 34 | Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti. | And when they were gone over, they came into the land of Gennesaret. |
| 35 | Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote, | And when the men of that place had knowledge of him, they sent out into all that country round about, and brought unto him all that were diseased; |
| 36 | wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake; wote waliomgusa walipona. | And besought him that they might only touch the hem of his garment: and as many as touched were made perfectly whole. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL