마태복음 13장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 58절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa. | The same day went Jesus out of the house, and sat by the sea side. |
| 2 | Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashua, akaketi. Hao watu walisimama kwenye ukingo wa ziwa, | And great multitudes were gathered together unto him, so that he went into a ship, and sat; and the whole multitude stood on the shore. |
| 3 | naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano. "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. | And he spake many things unto them in parables, saying, Behold, a sower went forth to sow; |
| 4 | Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. | And when he sowed, some seeds fell by the way side, and the fowls came and devoured them up: |
| 5 | Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina. | Some fell upon stony places, where they had not much earth: and forthwith they sprung up, because they had no deepness of earth: |
| 6 | Jua lilipochomoza, zilichomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka. | And when the sun was up, they were scorched; and because they had no root, they withered away. |
| 7 | Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga. | And some fell among thorns; and the thorns sprung up, and choked them: |
| 8 | Lakini nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: nyingine punje mia moja, nyingine sitini na nyingine thelathini. | But other fell into good ground, and brought forth fruit, some an hundredfold, some sixtyfold, some thirtyfold. |
| 9 | Mwenye masikio na asikie!" | Who hath ears to hear, let him hear. |
| 10 | Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, "Kwa nini unasema na watu kwa mifano?" | And the disciples came, and said unto him, Why speakest thou unto them in parables? |
| 11 | Yesu akawajibu, "Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa. | He answered and said unto them, Because it is given unto you to know the mysteries of the kingdom of heaven, but to them it is not given. |
| 12 | Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa. | For whosoever hath, to him shall be given, and he shall have more abundance: but whosoever hath not, from him shall be taken away even that he hath. |
| 13 | Ndiyo maana ninasema nao kwa mifano, kwa sababu wanatazama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawaelewi. | Therefore speak I to them in parables: because they seeing see not; and hearing they hear not, neither do they understand. |
| 14 | Kwao yametimia yale aliyosema nabii Isaya: Kusikia mtasikia, lakini hamtaelewa; Kutazama mtatazama, lakini hamtaona. | And in them is fulfilled the prophecy of Esaias, which saith, By hearing ye shall hear, and shall not understand; and seeing ye shall see, and shall not perceive: |
| 15 | Maana akili za watu hawa zimepumbaa, wameyaziba masikio yao, wameyafumba macho yao. La sivyo, wangeona kwa macho yao. wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa akili zao, na kunigeukia, asema Bwana, nami ningewaponya. | For this people’s heart is waxed gross, and their ears are dull of hearing, and their eyes they have closed; lest at any time they should see with their eyes, and hear with their ears, and should understand with their heart, and should be converted, and I should heal them. |
| 16 | "Lakini heri yenu ninyi, maana macho yenu yanaona na masikio yenu yanasikia. | But blessed are your eyes, for they see: and your ears, for they hear. |
| 17 | Kweli nawaambieni, manabii na watu wengi wema walitamani kuyaona yale mnayoyaona, wasiyaone, na kuyasikia yale mnayoyasikia, wasiyasikie. | For verily I say unto you, That many prophets and righteous men have desired to see those things which ye see, and have not seen them; and to hear those things which ye hear, and have not heard them. |
| 18 | "Basi, ninyi sikilizeni maana ya mfano huo wa mpanzi. | Hear ye therefore the parable of the sower. |
| 19 | Yeyote asikiaye ujumbe wa ufalme bila kuuelewa, ni kama zile mbegu zilizoanguka njiani; yule Mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake. | When any one heareth the word of the kingdom, and understandeth it not, then cometh the wicked one, and catcheth away that which was sown in his heart. This is he which received seed by the way side. |
| 20 | Ile mbegu iliyopandwa penye mawe ni mfano wa mtu asikiaye ujumbe huo na mara akaupokea kwa furaha. | But he that received the seed into stony places, the same is he that heareth the word, and anon with joy receiveth it; |
| 21 | Lakini haumwingii na kuwa na mizizi ndani yake; huendelea kuuzingatia ujumbe huo kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya ujumbe huo, anakata tamaa mara. | Yet hath he not root in himself, but dureth for a while: for when tribulation or persecution ariseth because of the word, by and by he is offended. |
| 22 | Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye huo ujumbe, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali huusonga ujumbe huo, naye hazai matunda. | He also that received seed among the thorns is he that heareth the word; and the care of this world, and the deceitfulness of riches, choke the word, and he becometh unfruitful. |
| 23 | Ile mbegu iliyopandwa katika udongo mzuri ni mfano wa mtu ausikiaye ujumbe huo na kuuelewa, naye huzaa matunda; mmoja mia, mwingine sitini na mwingine thelathini." | But he that received seed into the good ground is he that heareth the word, and understandeth it; which also beareth fruit, and bringeth forth, some an hundredfold, some sixty, some thirty. |
| 24 | Yesu akawaambia watu mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. | Another parable put he forth unto them, saying, The kingdom of heaven is likened unto a man which sowed good seed in his field: |
| 25 | Lakini watu wakiwa wamelala, adui yake akaja akapanda magugu kati ya ngano, akaenda zake. | But while men slept, his enemy came and sowed tares among the wheat, and went his way. |
| 26 | Basi, mimea ilipoota na kuanza kuchanua, magugu pia yakaanza kuonekana. | But when the blade was sprung up, and brought forth fruit, then appeared the tares also. |
| 27 | Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwambia, Mheshimiwa, bila shaka ulipanda mbegu nzuri katika shamba lako. Sasa magugu yametoka wapi? | So the servants of the householder came and said unto him, Sir, didst not thou sow good seed in thy field? from whence then hath it tares? |
| 28 | Yeye akawajibu, Adui ndiye aliyefanya hivyo. Basi, watumishi wake wakamwuliza, Je, unataka twende tukayang'oe | He said unto them, An enemy hath done this. The servants said unto him, Wilt thou then that we go and gather them up? |
| 29 | Naye akawajibu, La, msije labda mnapokusanya magugu, mkang'oa na ngano pia. | But he said, Nay; lest while ye gather up the tares, ye root up also the wheat with them. |
| 30 | Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu." | Let both grow together until the harvest: and in the time of harvest I will say to the reapers, Gather ye together first the tares, and bind them in bundles to burn them: but gather the wheat into my barn. |
| 31 | Yesu akawaambia watu mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja, akaipanda katika shamba lake. | Another parable put he forth unto them, saying, The kingdom of heaven is like to a grain of mustard seed, which a man took, and sowed in his field: |
| 32 | Yenyewe ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini ikishaota huwa kubwa kuliko mimea yote. Hukua ikawa mti, na ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake." | Which indeed is the least of all seeds: but when it is grown, it is the greatest among herbs, and becometh a tree, so that the birds of the air come and lodge in the branches thereof. |
| 33 | Yesu akawaambia mfano mwingine: "Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga pishi tatu, hata unga wote ukaumuka." | Another parable spake he unto them; The kingdom of heaven is like unto leaven, which a woman took, and hid in three measures of meal, till the whole was leavened. |
| 34 | Yesu aliwaambia watu hayo yote kwa mifano. Hakuwaambia chochote bila kutumia mifano, | All these things spake Jesus unto the multitude in parables; and without a parable spake he not unto them: |
| 35 | ili jambo lililonenwa na nabii litimie: "Nitasema kwa mifano; nitawaambia mambo yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu." | That it might be fulfilled which was spoken by the prophet, saying, I will open my mouth in parables; I will utter things which have been kept secret from the foundation of the world. |
| 36 | Kisha Yesu aliwaaga wale watu, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwambia, "Tufafanulie ule mfano wa magugu shambani." | Then Jesus sent the multitude away, and went into the house: and his disciples came unto him, saying, Declare unto us the parable of the tares of the field. |
| 37 | Yesu akawaambia, "Mpanzi wa zile mbegu nzuri ni Mwana wa Mtu. | He answered and said unto them, He that soweth the good seed is the Son of man; |
| 38 | Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao Ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu. | The field is the world; the good seed are the children of the kingdom; but the tares are the children of the wicked one; |
| 39 | Adui aliyepanda yale magugu ni Ibilisi. Mavuno ni mwisho wa nyakati na wavunaji ni malaika. | The enemy that sowed them is the devil; the harvest is the end of the world; and the reapers are the angels. |
| 40 | Kama vile magugu yanavyokusanywa kuchomwa moto, ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati; | As therefore the tares are gathered and burned in the fire; so shall it be in the end of this world. |
| 41 | Mwana wa Mtu atawatuma malaika wake wawakusanye kutoka katika Ufalme wake wale wote wenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu, | The Son of man shall send forth his angels, and they shall gather out of his kingdom all things that offend, and them which do iniquity; |
| 42 | na kuwatupa katika tanuru ya moto, na huko watalia na kusaga meno. | And shall cast them into a furnace of fire: there shall be wailing and gnashing of teeth. |
| 43 | Kisha, wale wema watang'ara kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Sikieni basi, kama mna masikio! | Then shall the righteous shine forth as the sun in the kingdom of their Father. Who hath ears to hear, let him hear. |
| 44 | "Ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyofichika shambani. Mtu mmoja aliigundua, akaificha tena. Alifurahi sana hata akaenda kuuza yote aliyokuwa nayo, akalinunua shamba lile. | Again, the kingdom of heaven is like unto treasure hid in a field; the which when a man hath found, he hideth, and for joy thereof goeth and selleth all that he hath, and buyeth that field. |
| 45 | "Tena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfanyabiashara mmoja mwenye kutafuta lulu nzuri. | Again, the kingdom of heaven is like unto a merchant man, seeking goodly pearls: |
| 46 | Alipopata lulu moja ya thamani kubwa, alienda akauza yote aliyokuwa nayo, akainunua lulu ile. | Who, when he had found one pearl of great price, went and sold all that he had, and bought it. |
| 47 | "Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na wavu uliotupwa baharini, ukanasa samaki wa kila aina. | Again, the kingdom of heaven is like unto a net, that was cast into the sea, and gathered of every kind: |
| 48 | Ulipojaa, watu waliuvuta pwani, wakaketi, wakachagua samaki wazuri wakawaweka ndani ya vikapu vyao, na wabaya wakawatupa. | Which, when it was full, they drew to shore, and sat down, and gathered the good into vessels, but cast the bad away. |
| 49 | Ndivyo itakavyokuwa mwishoni mwa nyakati: malaika watatokea, watawatenganisha watu wabaya na watu wema, | So shall it be at the end of the world: the angels shall come forth, and sever the wicked from among the just, |
| 50 | na kuwatupa hao wabaya katika tanuru ya moto. Huko watalia na kusaga meno." | And shall cast them into the furnace of fire: there shall be wailing and gnashing of teeth. |
| 51 | Yesu akawauliza, "Je, mmeelewa mambo haya yote?" Wakamjibu, "Naam." | Jesus saith unto them, Have ye understood all these things? They say unto him, Yea, Lord. |
| 52 | Naye akawaambia, "Hivyo basi, kila mwalimu wa Sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale." | Then said he unto them, Therefore every scribe which is instructed unto the kingdom of heaven is like unto a man that is an householder, which bringeth forth out of his treasure things new and old. |
| 53 | Yesu alipomaliza kusema mifano hiyo alitoka mahali hapo, | And it came to pass, that when Jesus had finished these parables, he departed thence. |
| 54 | akaenda kijijini kwake. Huko akawa anawafundisha watu katika sunagogi hata wakashangaa, wakasema, "Huyu amepata wapi hekima hii na maajabu? | And when he was come into his own country, he taught them in their synagogue, insomuch that they were astonished, and said, Whence hath this man this wisdom, and these mighty works? |
| 55 | Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? | Is not this the carpenter’s son? is not his mother called Mary? and his brethren, James, and Joses, and Simon, and Judas? |
| 56 | Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?" | And his sisters, are they not all with us? Whence then hath this man all these things? |
| 57 | Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, "Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!" | And they were offended in him. But Jesus said unto them, A prophet is not without honour, save in his own country, and in his own house. |
| 58 | Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao. | And he did not many mighty works there because of their unbelief. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL