마가복음 4장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마가복음 (Mark) · 41절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa. | And he began again to teach by the sea side: and there was gathered unto him a great multitude, so that he entered into a ship, and sat in the sea; and the whole multitude was by the sea on the land. |
| 2 | Aliwafundisha mambo mengi kwa mifano, na katika mafundisho yake aliwaambia, | And he taught them many things by parables, and said unto them in his doctrine, |
| 3 | "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. | Hearken; Behold, there went out a sower to sow: |
| 4 | Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. | And it came to pass, as he sowed, some fell by the way side, and the fowls of the air came and devoured it up. |
| 5 | Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Mbegu hizo ziliota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina. | And some fell on stony ground, where it had not much earth; and immediately it sprang up, because it had no depth of earth: |
| 6 | Jua lilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka. | But when the sun was up, it was scorched; and because it had no root, it withered away. |
| 7 | Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka. | And some fell among thorns, and the thorns grew up, and choked it, and it yielded no fruit. |
| 8 | Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia." | And other fell on good ground, and did yield fruit that sprang up and increased; and brought forth, some thirty, and some sixty, and some an hundred. |
| 9 | Kisha akawaambia, "Mwenye masikio na asikie!" | And he said unto them, He that hath ears to hear, let him hear. |
| 10 | Yesu alipokuwa peke yake, baadhi ya wale waliomsikia walimwendea pamoja na wale kumi na wawili, wakamwuliza juu ya hiyo mifano. | And when he was alone, they that were about him with the twelve asked of him the parable. |
| 11 | Naye akawaambia, "Ninyi mmejaliwa kujua siri ya Utawala wa Mungu, lakini wale walio nje wataambiwa kila kitu kwa mifano, | And he said unto them, Unto you it is given to know the mystery of the kingdom of God: but unto them that are without, all these things are done in parables: |
| 12 | ili, Watazame kweli, lakini wasione. Wasikie kweli, lakini wasielewe. La sivyo, wangemgeukia Mungu, naye angewasamehe." | That seeing they may see, and not perceive; and hearing they may hear, and not understand; lest at any time they should be converted, and their sins should be forgiven them. |
| 13 | Basi, Yesu akawauliza, "Je, ninyi hamwelewi mfano huu? Mtawezaje basi, kuelewa mfano wowote? | And he said unto them, Know ye not this parable? and how then will ye know all parables? |
| 14 | Mpanzi hupanda neno la Mungu. | The sower soweth the word. |
| 15 | Watu wengine ni kama wale walio njiani ambapo mbegu zilianguka. Hawa hulisikia hilo neno lakini mara Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao. | And these are they by the way side, where the word is sown; but when they have heard, Satan cometh immediately, and taketh away the word that was sown in their hearts. |
| 16 | Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu wanapolisikia hilo neno hulipokea kwa furaha. | And these are they likewise which are sown on stony ground; who, when they have heard the word, immediately receive it with gladness; |
| 17 | Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno mara wanakata tamaa. | And have no root in themselves, and so endure but for a time: afterward, when affliction or persecution ariseth for the word’s sake, immediately they are offended. |
| 18 | Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaolisikia hilo neno, | And these are they which are sown among thorns; such as hear the word, |
| 19 | lakini wasiwasi wa ulimwengu huu, anasa za mali na tamaa za kila namna huwaingia na kulisonga hilo neno, nao hawazai matunda. | And the cares of this world, and the deceitfulness of riches, and the lusts of other things entering in, choke the word, and it becometh unfruitful. |
| 20 | Lakini wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa katika udongo mzuri. Hawa hulisikia hilo neno, wakalipokea, wakazaa matunda: wengine thelathini, wengine sitini na wengine mia moja." | And these are they which are sown on good ground; such as hear the word, and receive it, and bring forth fruit, some thirtyfold, some sixty, and some an hundred. |
| 21 | Yesu akaendelea kuwaambia, "Je, watu huwasha taa wakaileta ndani na kuifunika kwa pishi au kuiweka mvunguni? La! Huiweka juu ya kinara. | And he said unto them, Is a candle brought to be put under a bushel, or under a bed? and not to be set on a candlestick? |
| 22 | Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa. | For there is nothing hid, which shall not be manifested; neither was any thing kept secret, but that it should come abroad. |
| 23 | Mwenye masikio na asikie!" | If any man have ears to hear, let him hear. |
| 24 | Akawaambia pia, "Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa. | And he said unto them, Take heed what ye hear: with what measure ye mete, it shall be measured to you: and unto you that hear shall more be given. |
| 25 | Aliye na kitu atapewa zaidi; asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa." | For he that hath, to him shall be given: and he that hath not, from him shall be taken even that which he hath. |
| 26 | Yesu akaendelea kusema, "Ufalme wa Mungu ni kama ifuatavyo. Mtu hupanda mbegu shambani. | And he said, So is the kingdom of God, as if a man should cast seed into the ground; |
| 27 | Usiku hulala, mchana yu macho na wakati huo mbegu zinaota na kukua; yeye hajui inavyofanyika. | And should sleep, and rise night and day, and the seed should spring and grow up, he knoweth not how. |
| 28 | Udongo wenyewe huiwezesha mimea kukua na kuzaa matunda: kwanza huchipua jani changa, kisha suke, na mwishowe nafaka ndani ya suke. | For the earth bringeth forth fruit of herself; first the blade, then the ear, after that the full corn in the ear. |
| 29 | Nafaka inapoiva, huyo mtu huanza kutumia mundu wake, maana wakati wa mavuno umefika." | But when the fruit is brought forth, immediately he putteth in the sickle, because the harvest is come. |
| 30 | Tena, Yesu akasema, "Tuufananishe Utawala wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani? | And he said, Whereunto shall we liken the kingdom of God? or with what comparison shall we compare it? |
| 31 | Ni kama mbegu ya haradali ambayo ni ndogo kuliko mbegu zote. | It is like a grain of mustard seed, which, when it is sown in the earth, is less than all the seeds that be in the earth: |
| 32 | Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake." | But when it is sown, it groweth up, and becometh greater than all herbs, and shooteth out great branches; so that the fowls of the air may lodge under the shadow of it. |
| 33 | Yesu aliwahubiria ujumbe wake kwa mifano mingine mingi ya namna hiyo; aliongea nao kadiri walivyoweza kusikia. | And with many such parables spake he the word unto them, as they were able to hear it. |
| 34 | Hakuongea nao chochote bila kutumia mifano; lakini alipokuwa pamoja na wanafunzi wake peke yao alikuwa akiwafafanulia kila kitu. | But without a parable spake he not unto them: and when they were alone, he expounded all things to his disciples. |
| 35 | Jioni, siku hiyohiyo, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Tuvuke ziwa, twende ng'ambo." | And the same day, when the even was come, he saith unto them, Let us pass over unto the other side. |
| 36 | Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Palikuwapo pia mashua nyingine hapo. | And when they had sent away the multitude, they took him even as he was in the ship. And there were also with him other little ships. |
| 37 | Basi, dhoruba kali ikaanza kuvuma, mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikaanza kujaa maji. | And there arose a great storm of wind, and the waves beat into the ship, so that it was now full. |
| 38 | Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, "Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?" | And he was in the hinder part of the ship, asleep on a pillow: and they awake him, and say unto him, Master, carest thou not that we perish? |
| 39 | Basi, akaamka, akaukemea ule upepo na kuyaamrisha mawimbi ya ziwa, "Kimya! Tulia!" Hapo upepo ukakoma, kukawa shwari kabisa. | And he arose, and rebuked the wind, and said unto the sea, Peace, be still. And the wind ceased, and there was a great calm. |
| 40 | Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Mbona mnaogopa? Je, bado hamna imani?" | And he said unto them, Why are ye so fearful? how is it that ye have no faith? |
| 41 | Nao wakaogopa sana, wakawa wanaulizana, "Huyu ni nani basi, hata upepo na mawimbi vinamtii?" | And they feared exceedingly, and said one to another, What manner of man is this, that even the wind and the sea obey him? |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL