마가복음 3장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마가복음 (Mark) · 35절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yesu aliingia tena katika sunagogi na mle ndani mlikuwa na mtu aliyekuwa na mkono uliopooza. | And he entered again into the synagogue; and there was a man there which had a withered hand. |
| 2 | Humo baadhi ya watu walimngojea amponye mtu huyo siku ya sabato ili wapate kumshtaki. | And they watched him, whether he would heal him on the sabbath day; that they might accuse him. |
| 3 | Yesu akamwambia huyo mtu aliyekuwa na mkono uliopooza, "Njoo hapa katikati." | And he saith unto the man which had the withered hand, Stand forth. |
| 4 | Kisha, akawauliza, "Je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuua?" Lakini wao hawakusema neno. | And he saith unto them, Is it lawful to do good on the sabbath days, or to do evil? to save life, or to kill? But they held their peace. |
| 5 | Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, "Nyosha mkono wako!" Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena. | And when he had looked round about on them with anger, being grieved for the hardness of their hearts, he saith unto the man, Stretch forth thine hand. And he stretched it out: and his hand was restored whole as the other. |
| 6 | Mara Mafarisayo wakatoka nje, wakafanya shauri pamoja na watu wa kikundi cha Herode jinsi ya kumwangamiza Yesu. | And the Pharisees went forth, and straightway took counsel with the Herodians against him, how they might destroy him. |
| 7 | Yesu aliondoka hapo pamoja na wanafunzi wake, akaenda kando ya ziwa, na umati wa watu ukamfuata. Watu hao walikuwa wametoka Yerusalemu, Yudea, | But Jesus withdrew himself with his disciples to the sea: and a great multitude from Galilee followed him, and from Judea, |
| 8 | Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda. | And from Jerusalem, and from Idumea, and from beyond Jordan; and they about Tyre and Sidon, a great multitude, when they had heard what great things he did, came unto him. |
| 9 | Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga. | And he spake to his disciples, that a small ship should wait on him because of the multitude, lest they should throng him. |
| 10 | Alikuwa amewaponya watu wengi, na wagonjwa wote wakawa wanamsonga ili wapate kumgusa. | For he had healed many; insomuch that they pressed upon him for to touch him, as many as had plagues. |
| 11 | Na watu waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu walipomwona, walijitupa chini mbele yake na kupaaza sauti, "Wewe ni Mwana wa Mungu!" | And unclean spirits, when they saw him, fell down before him, and cried, saying, Thou art the Son of God. |
| 12 | Lakini Yesu akawaamuru kwa ukali wasimjulishe kwa watu. | And he straitly charged them that they should not make him known. |
| 13 | Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea, | And he goeth up into a mountain, and calleth unto him whom he would: and they came unto him. |
| 14 | naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri | And he ordained twelve, that they should be with him, and that he might send them forth to preach, |
| 15 | na wawe na mamlaka ya kuwafukuza pepo. | And to have power to heal sicknesses, and to cast out devils: |
| 16 | Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro), | And Simon he surnamed Peter; |
| 17 | Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake "wanangurumo"), | And James the son of Zebedee, and John the brother of James; and he surnamed them Boanerges, which is, The sons of thunder: |
| 18 | Andrea na Filipo, Batholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanani na | And Andrew, and Philip, and Bartholomew, and Matthew, and Thomas, and James the son of Alpheus, and Thaddeus, and Simon the Canaanite, |
| 19 | Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu. | And Judas Iscariot, which also betrayed him: and they went into an house. |
| 20 | Kisha Yesu alikwenda nyumbani. Umati wa watu ukakusanyika tena, hata Yesu na wafuasi wake wasiweze kupata nafasi ya kula chakula. | And the multitude cometh together again, so that they could not so much as eat bread. |
| 21 | Basi, watu wa jamaa yake walipopata habari hiyo wakatoka kwenda kumchukua maana walikuwa wanasema kwamba amepatwa na wazimu. | And when his friends heard of it, they went out to lay hold on him: for they said, He is beside himself. |
| 22 | Nao walimu wa Sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, "Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo." | And the scribes which came down from Jerusalem said, He hath Beelzebub, and by the prince of the devils casteth he out devils. |
| 23 | Hapo Yesu akawaita, akawaambia kwa mifano, "Shetani anawezaje kumfukuza Shetani? | And he called them unto him, and said unto them in parables, How can Satan cast out Satan? |
| 24 | Ikiwa utawala mmoja umegawanyika makundimakundi yanayopigana, utawala huo hauwezi kudumu. | And if a kingdom be divided against itself, that kingdom cannot stand. |
| 25 | Tena, ikiwa jamaa moja imegawanyika makundimakundi yanayopingana, jamaa hiyo itaangamia. | And if a house be divided against itself, that house cannot stand. |
| 26 | Ikiwa basi, utawala wa Shetani umegawanyika vikundivikundi hauwezi kudumu, bali utaangamia kabisa. | And if Satan rise up against himself, and be divided, he cannot stand, but hath an end. |
| 27 | "Hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake, isipokuwa kwanza amemfunga huyo mtu mwenye nguvu; hapo ndipo atakapoweza kumnyang'anya mali yake. | No man can enter into a strong man’s house, and spoil his goods, except he will first bind the strong man; and then he will spoil his house. |
| 28 | "Kweli nawaambieni, watu watasamehewa dhambi zao zote na kufuru zao zote; | Verily I say unto you, All sins shall be forgiven unto the sons of men, and blasphemies wherewith soever they shall blaspheme: |
| 29 | lakini anayesema mabaya dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa kamwe; ana hatia ya dhambi ya milele." | But he that shall blaspheme against the Holy Ghost hath never forgiveness, but is in danger of eternal damnation: |
| 30 | (Yesu alisema hivyo kwa sababu walikuwa wanasema, "Ana pepo mchafu.") | Because they said, He hath an unclean spirit. |
| 31 | Mama yake Yesu na ndugu zake walifika hapo, wakasimama nje, wakampelekea ujumbe kutaka kumwona. | There came then his brethren and his mother, and, standing without, sent unto him, calling him. |
| 32 | Umati wa watu ulikuwa umekaa hapo kumzunguka. Basi, wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanataka kukuona." | And the multitude sat about him, and they said unto him, Behold, thy mother and thy brethren without seek for thee. |
| 33 | Yesu akawaambia, "Mama yangu na ndugu zangu ni kina nani?" | And he answered them, saying, Who is my mother, or my brethren? |
| 34 | Hapo akawatazama watu waliokuwa wamemzunguka, akasema, "Tazameni! Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. | And he looked round about on them which sat about him, and said, Behold my mother and my brethren! |
| 35 | Mtu yeyote anayefanya anayotaka Mungu, huyo ndiye kaka yangu, dada yangu na mama yangu." | For whosoever shall do the will of God, the same is my brother, and my sister, and mother. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL