누가복음 7장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 50절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu. | Now when he had ended all his sayings in the audience of the people, he entered into Capernaum. |
| 2 | Huko kulikuwa na jemadari mmoja Mroma ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu kufa. | And a certain centurion’s servant, who was dear unto him, was sick, and ready to die. |
| 3 | Yule jemadari aliposikia habari za Yesu, aliwatuma wazee fulani Wayahudi waende kumwomba aje amponye mtumishi wake. | And when he heard of Jesus, he sent unto him the elders of the Jews, beseeching him that he would come and heal his servant. |
| 4 | Walipofika kwa Yesu, walimsihi sana, wakasema: "Huyu anastahili afanyiwe jambo hilo, | And when they came to Jesus, they besought him instantly, saying, That he was worthy for whom he should do this: |
| 5 | maana analipenda taifa letu, na ndiye aliyetujengea lile sunagogi." | For he loveth our nation, and he hath built us a synagogue. |
| 6 | Basi, Yesu akaenda pamoja nao. Alipokuwa karibu kufika nyumbani kwa yule jemadari Mroma, yule jemadari aliwatuma marafiki zake wamwambie Yesu: "Bwana, usijisumbue zaidi, maana mimi sistahili uingie nyumbani mwangu. | Then Jesus went with them. And when he was now not far from the house, the centurion sent friends to him, saying unto him, Lord, trouble not thyself: for I am not worthy that thou shouldest enter under my roof: |
| 7 | Ndio maana sikujiona nastahili hata kuja kwako; amuru tu, na mtumishi wangu atapona. | Wherefore neither thought I myself worthy to come unto thee: but say in a word, and my servant shall be healed. |
| 8 | Mimi pia ni mtu niliye chini ya mamlaka, na ninao askari chini yangu. Namwambia mmoja, Nenda!, naye huenda; namwambia mwingine, Njoo! naye huja; na nikimwambia mtumishi wangu, Fanya hiki!, hufanya." | For I also am a man set under authority, having under me soldiers, and I say unto one, Go, and he goeth; and to another, Come, and he cometh; and to my servant, Do this, and he doeth it. |
| 9 | Yesu aliposikia hayo, alishangaa; halafu akauelekea ule umati wa watu uliokuwa unamfuata, akasema, "Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli." | When Jesus heard these things, he marvelled at him, and turned him about, and said unto the people that followed him, I say unto you, I have not found so great faith, no, not in Israel. |
| 10 | Wale watu walipowasili nyumbani walimkuta yule mtumishi hajambo kabisa. | And they that were sent, returning to the house, found the servant whole that had been sick. |
| 11 | Baadaye kidogo Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake pamoja na kundi kubwa la watu waliandamana naye. | And it came to pass the day after, that he went into a city called Nain; and many of his disciples went with him, and much people. |
| 12 | Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya kijana mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama. | Now when he came nigh to the gate of the city, behold, there was a dead man carried out, the only son of his mother, and she was a widow: and much people of the city was with her. |
| 13 | Bwana alipomwona mama huyo, alimwonea huruma, akamwambia, "Usilie." | And when the Lord saw her, he had compassion on her, and said unto her, Weep not. |
| 14 | Kisha akaenda, akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wanalichukua wakasimama. Halafu akasema, "Kijana! Nakuamuru, amka!" | And he came and touched the bier: and they that bare him stood still. And he said, Young man, I say unto thee, Arise. |
| 15 | Yule aliyekufa akaketi, akaanza kuongea. Na Yesu akamkabidhi kwa mama yake. | And he that was dead sat up, and began to speak. And he delivered him to his mother. |
| 16 | Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema: "Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake." | And there came a fear on all: and they glorified God, saying, That a great prophet is risen up among us; and, That God hath visited his people. |
| 17 | Habari hizo zikaenea kote katika Uyahudi na katika nchi za jirani. | And this rumour of him went forth throughout all Judea, and throughout all the region round about. |
| 18 | Wanafunzi wa Yohane walimpa habari Yohane juu ya mambo hayo yote. Naye Yohane, baada ya kuwaita wawili kati ya wanafunzi wake, | And the disciples of John shewed him of all these things. |
| 19 | aliwatuma kwa Bwana wamwulize: "Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?" | And John calling unto him two of his disciples sent them to Jesus, saying, Art thou he that should come? or look we for another? |
| 20 | Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, "Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?" | When the men were come unto him, they said, John Baptist hath sent us unto thee, saying, Art thou he that should come? or look we for another? |
| 21 | Wakati huohuo, Yesu alikuwa anawaponya watu wengi waliokuwa wanateseka kwa magonjwa na waliopagawa na pepo wabaya, akawawezesha vipofu wengi kuona tena. | And in that same hour he cured many of their infirmities and plagues, and of evil spirits; and unto many that were blind he gave sight. |
| 22 | Basi, Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari njema. | Then Jesus answering said unto them, Go your way, and tell John what things ye have seen and heard; how that the blind see, the lame walk, the lepers are cleansed, the deaf hear, the dead are raised, to the poor the gospel is preached. |
| 23 | Heri mtu yule ambaye hana mashaka nami!" | And blessed is he, whosoever shall not be offended in me. |
| 24 | Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: "Mlikwenda kule jangwani, hivi mlitaka kuona kitu gani? Mlitaka kuona unyasi unaotikiswa na upepo? | And when the messengers of John were departed, he began to speak unto the people concerning John, What went ye out into the wilderness for to see? A reed shaken with the wind? |
| 25 | Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevalia mavazi maridadi? La hasha! Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme! | But what went ye out for to see? A man clothed in soft raiment? Behold, they which are gorgeously apparelled, and live delicately, are in kings’ courts. |
| 26 | Basi, niambieni, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, hakika ni zaidi ya nabii. | But what went ye out for to see? A prophet? Yea, I say unto you, and much more than a prophet. |
| 27 | Huyu Yohane ndiye anayesemwa katika Maandiko Matakatifu: Hapa ni mtumishi wangu, asema Bwana; ninamtuma akutangulie, akutayarishie njia." | This is he, of whom it is written, Behold, I send my messenger before thy face, which shall prepare thy way before thee. |
| 28 | Yesu akamalizia kwa kusema, "Nawaambieni, kati ya binadamu wote hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane Mbatizaji. Hata hivyo, yule aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkubwa zaidi kuliko yeye." | For I say unto you, Among those that are born of women there is not a greater prophet than John the Baptist: but he that is least in the kingdom of God is greater than he. |
| 29 | Waliposikia hayo watu wote na watoza ushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane. | And all the people that heard him, and the publicans, justified God, being baptized with the baptism of John. |
| 30 | Lakini Mafarisayo na walimu wa Sheria walikataa mpango wa Mungu uliowahusu wakakataa kubatizwa na Yohane. | But the Pharisees and lawyers rejected the counsel of God against themselves, being not baptized of him. |
| 31 | Yesu akaendelea kusema, "Basi, nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni watu wa namna gani? | And the Lord said, Whereunto then shall I liken the men of this generation? and to what are they like? |
| 32 | Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: Tumewapigieni ngoma, lakini hamkucheza! Tumeomboleza, lakini hamkulia! | They are like unto children sitting in the marketplace, and calling one to another, and saying, We have piped unto you, and ye have not danced; we have mourned to you, and ye have not wept. |
| 33 | Kwa maana Yohane alikuja, yeye alifunga na hakunywa divai, nanyi mkasema: Amepagawa na pepo! | For John the Baptist came neither eating bread nor drinking wine; and ye say, He hath a devil. |
| 34 | Akaja Mwana wa Mtu; anakula na kunywa, mkasema: Mwangalieni mlafi huyu na mlevi; rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi! | The Son of man is come eating and drinking; and ye say, Behold a gluttonous man, and a winebibber, a friend of publicans and sinners! |
| 35 | Hata hivyo, hekima ya Mungu imethibitishwa kuwa njema na wote wale wanaoikubali." | But wisdom is justified of all her children. |
| 36 | Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani mwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula. | And one of the Pharisees desired him that he would eat with him. And he went into the Pharisee’s house, and sat down to meat. |
| 37 | Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja aliyekuwa anaishi maisha mabaya. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi. | And, behold, a woman in the city, which was a sinner, when she knew that Jesus sat at meat in the Pharisee’s house, brought an alabaster box of ointment, |
| 38 | Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi. | And stood at his feet behind him weeping, and began to wash his feet with tears, and did wipe them with the hairs of her head, and kissed his feet, and anointed them with the ointment. |
| 39 | Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, "Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi." | Now when the Pharisee which had bidden him saw it, he spake within himself, saying, This man, if he were a prophet, would have known who and what manner of woman this is that toucheth him: for she is a sinner. |
| 40 | Yesu akamwambia huyo Mfarisayo, "Simoni, ninacho kitu cha kukwambia." Naye Simoni akamwambia, "Ndio Mwalimu, sema." Yesu akasema, | And Jesus answering said unto him, Simon, I have somewhat to say unto thee. And he saith, Master, say on. |
| 41 | "Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: mmoja alikuwa amekopa dinari mia tano, na mwingine hamsini. | There was a certain creditor which had two debtors: the one owed five hundred pence, and the other fifty. |
| 42 | Waliposhindwa kulipa madeni yao, huyo mtu aliwasamehe wote wawili. Sasa ni yupi kati ya hao wawili atampenda zaidi huyo bwana?" | And when they had nothing to pay, he frankly forgave them both. Tell me therefore, which of them will love him most? |
| 43 | Simoni akamjibu, "Ni dhahiri kwamba yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi atampenda zaidi yule bwana." Yesu akamwambia, "Sawa." | Simon answered and said, I suppose that he, to whom he forgave most. And he said unto him, Thou hast rightly judged. |
| 44 | Halafu akamgeukia yule mwanamke na kumwambia Simoni, "Unamwona huyu mwanamke, sivyo? Basi, mimi nilipoingia hapa nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu yangu; lakini mwanamke huyu ameniosha miguu yangu kwa machozi yake na kunipangusa kwa nywele zake. | And he turned to the woman, and said unto Simon, Seest thou this woman? I entered into thine house, thou gavest me no water for my feet: but she hath washed my feet with tears, and wiped them with the hairs of her head. |
| 45 | Wewe hukunisalimu kwa kunibusu, lakini huyu mwanamke tangu nilipoingia hapa amekuwa akiibusu miguu yangu. | Thou gavest me no kiss: but this woman since the time I came in hath not ceased to kiss my feet. |
| 46 | Wewe hukunionyesha ukarimu wako kwa kunipaka mafuta kichwani, lakini huyu mwanamke amefanya hivyo kwa kunipaka mafuta miguu yangu. | My head with oil thou didst not anoint: but this woman hath anointed my feet with ointment. |
| 47 | Kwa hiyo nakwambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonyesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo." | Wherefore I say unto thee, Her sins, which are many, are forgiven; for she loved much: but to whom little is forgiven, the same loveth little. |
| 48 | Basi, Yesu akamwambia yule mwanamke, "Umesamehewa dhambi zako." | And he said unto her, Thy sins are forgiven. |
| 49 | Na hapo wale waliokuwa pamoja naye mezani wakaulizana, "Ni mtu wa namna gani huyu awezaye kusamehe dhambi?" | And they that sat at meat with him began to say within themselves, Who is this that forgiveth sins also? |
| 50 | Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, "Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani." | And he said to the woman, Thy faith hath saved thee; go in peace. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL