누가복음 6장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 49절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala. | And it came to pass on the second sabbath after the first, that he went through the corn fields; and his disciples plucked the ears of corn, and did eat, rubbing them in their hands. |
| 2 | Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, "Mbona mnafanya jambo ambalo si halali siku ya Sabato?" | And certain of the Pharisees said unto them, Why do ye that which is not lawful to do on the sabbath days? |
| 3 | Yesu akawajibu, "Je, hamjasoma jinsi alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? | And Jesus answering them said, Have ye not read so much as this, what David did, when himself was an hungred, and they which were with him; |
| 4 | Yeye aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Kisheria, ni makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kula mikate hiyo." | How he went into the house of God, and did take and eat the shewbread, and gave also to them that were with him; which it is not lawful to eat but for the priests alone? |
| 5 | Hivyo akawaambia, "Mwana wa Mtu ni Bwana wa Sabato." | And he said unto them, That the Son of man is Lord also of the sabbath. |
| 6 | Siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia katika sunagogi, akafundisha. Mle ndani mlikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. | And it came to pass also on another sabbath, that he entered into the synagogue and taught: and there was a man whose right hand was withered. |
| 7 | Walimu wa Sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisingizio cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato. | And the scribes and Pharisees watched him, whether he would heal on the sabbath day; that they might find an accusation against him. |
| 8 | Lakini Yesu alijua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, "Inuka, simama katikati." Yule mtu akaenda akasimama katikati. | But he knew their thoughts, and said to the man which had the withered hand, Rise up, and stand forth in the midst. And he arose and stood forth. |
| 9 | Kisha Yesu akawaambia, "Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?" | Then said Jesus unto them, I will ask you one thing; Is it lawful on the sabbath days to do good, or to do evil? to save life, or to destroy it? |
| 10 | Baada ya kuwatazama wote waliokuwa pale, akamwambia yule mtu, "Nyosha mkono wako." Naye akafanya hivyo, na mkono wake ukawa mzima tena. | And looking round about upon them all, he said unto the man, Stretch forth thy hand. And he did so: and his hand was restored whole as the other. |
| 11 | Lakini wao wakakasirika sana, wakajadiliana jinsi ya kumtendea Yesu maovu. | And they were filled with madness; and communed one with another what they might do to Jesus. |
| 12 | Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akimwomba Mungu. | And it came to pass in those days, that he went out into a mountain to pray, and continued all night in prayer to God. |
| 13 | Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume: | And when it was day, he called unto him his disciples: and of them he chose twelve, whom also he named apostles; |
| 14 | Simoni (ambaye Yesu alimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo, | Simon, (whom he also named Peter,) and Andrew his brother, James and John, Philip and Bartholomew, |
| 15 | Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo na Simoni (aliyeitwa Zelote), | Matthew and Thomas, James the son of Alpheus, and Simon called Zelotes, |
| 16 | Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti. | And Judas the brother of James, and Judas Iscariot, which also was the traitor. |
| 17 | Baada ya kushuka mlimani pamoja na mitume, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao. | And he came down with them, and stood in the plain, and the company of his disciples, and a great multitude of people out of all Judea and Jerusalem, and from the sea coast of Tyre and Sidon, which came to hear him, and to be healed of their diseases; |
| 18 | Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu. | And they that were vexed with unclean spirits: and they were healed. |
| 19 | Watu wote walitaka kumgusa, kwa maana nguvu ilikuwa inatoka ndani yake na kuwaponya wote. | And the whole multitude sought to touch him: for there went virtue out of him, and healed them all. |
| 20 | Yesu akawageukia wanafunzi wake, akasema: "Heri ninyi mlio maskini, maana Ufalme wa Mungu ni wenu. | And he lifted up his eyes on his disciples, and said, Blessed be ye poor: for yours is the kingdom of God. |
| 21 | Heri ninyi mnaosikia njaa sasa, maana baadaye mtashiba. Heri ninyi mnaolia sasa, maana baadaye mtacheka kwa furaha. | Blessed are ye that hunger now: for ye shall be filled. Blessed are ye that weep now: for ye shall laugh. |
| 22 | "Heri yenu ninyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu! | Blessed are ye, when men shall hate you, and when they shall separate you from their company, and shall reproach you, and cast out your name as evil, for the Son of man’s sake. |
| 23 | Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo. | Rejoice ye in that day, and leap for joy: for, behold, your reward is great in heaven: for in the like manner did their fathers unto the prophets. |
| 24 | Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri, maana mmekwisha pata faraja yenu. | But woe unto you that are rich! for ye have received your consolation. |
| 25 | Ole wenu ninyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia. | Woe unto you that are full! for ye shall hunger. Woe unto you that laugh now! for ye shall mourn and weep. |
| 26 | Ole wenu ninyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo. | Woe unto you, when all men shall speak well of you! for so did their fathers to the false prophets. |
| 27 | "Lakini nawaambieni ninyi mnaonisikiliza: wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni. | But I say unto you which hear, Love your enemies, do good to them which hate you, |
| 28 | Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. | Bless them that curse you, and pray for them which despitefully use you. |
| 29 | Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu akikunyang'anya koti lako mwachie pia shati lako. | And unto him that smiteth thee on the one cheek offer also the other; and him that taketh away thy cloke forbid not to take thy coat also. |
| 30 | Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang'anya mali yako usimtake akurudishie. | Give to every man that asketh of thee; and of him that taketh away thy goods ask them not again. |
| 31 | Watendeeni wengine kama mnavyotaka wawatendee ninyi. | And as ye would that men should do to you, do ye also to them likewise. |
| 32 | "Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda ninyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao. | For if ye love them which love you, what thank have ye? for sinners also love those that love them. |
| 33 | Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo! | And if ye do good to them which do good to you, what thank have ye? for sinners also do even the same. |
| 34 | Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile! | And if ye lend to them of whom ye hope to receive, what thank have ye? for sinners also lend to sinners, to receive as much again. |
| 35 | Ila nyinyi wapendeni adui zenu, na kuwatendea mema; kopesheni bila kutazamia malipo, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya. | But love ye your enemies, and do good, and lend, hoping for nothing again; and your reward shall be great, and ye shall be the children of the Highest: for he is kind unto the unthankful and to the evil. |
| 36 | Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma. | Be ye therefore merciful, as your Father also is merciful. |
| 37 | "Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa. | Judge not, and ye shall not be judged: condemn not, and ye shall not be condemned: forgive, and ye shall be forgiven: |
| 38 | Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho ambacho Mungu atatumia kwenu." | Give, and it shall be given unto you; good measure, pressed down, and shaken together, and running over, shall men give into your bosom. For with the same measure that ye mete withal it shall be measured to you again. |
| 39 | Akawaambia mfano huu: "Je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake? La! Wote wataanguka shimoni. | And he spake a parable unto them, Can the blind lead the blind? shall they not both fall into the ditch? |
| 40 | Mwanafunzi hamshindi mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akisha hitimu huwa kama mwalimu wake. | The disciple is not above his master: but every one that is perfect shall be as his master. |
| 41 | Unawezaje kukiona kibanzi kilicho katika jicho la mwenzio, usione boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe? | And why beholdest thou the mote that is in thy brother’s eye, but perceivest not the beam that is in thine own eye? |
| 42 | Au, unawezaje kumwambia mwenzako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicho lako, na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako. | Either how canst thou say to thy brother, Brother, let me pull out the mote that is in thine eye, when thou thyself beholdest not the beam that is in thine own eye? Thou hypocrite, cast out first the beam out of thine own eye, and then shalt thou see clearly to pull out the mote that is in thy brother’s eye. |
| 43 | "Mti mwema hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri. | For a good tree bringeth not forth corrupt fruit; neither doth a corrupt tree bring forth good fruit. |
| 44 | Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili. | For every tree is known by his own fruit. For of thorns men do not gather figs, nor of a bramble bush gather they grapes. |
| 45 | Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake. | A good man out of the good treasure of his heart bringeth forth that which is good; and an evil man out of the evil treasure of his heart bringeth forth that which is evil: for of the abundance of the heart his mouth speaketh. |
| 46 | "Mbona mwaniita Bwana, Bwana, na huku hamtimizi yale ninayosema? | And why call ye me, Lord, Lord, and do not the things which I say? |
| 47 | Nitawapeni mfano unaofaa kuonyesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza: | Whosoever cometh to me, and heareth my sayings, and doeth them, I will shew you to whom he is like: |
| 48 | Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara. | He is like a man which built an house, and digged deep, and laid the foundation on a rock: and when the flood arose, the stream beat vehemently upon that house, and could not shake it: for it was founded upon a rock. |
| 49 | Lakini yeyote anayesikia maneno yangu lakini asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!" | But he that heareth, and doeth not, is like a man that without a foundation built an house upon the earth; against which the stream did beat vehemently, and immediately it fell; and the ruin of that house was great. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL