고린도후서 3장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 고린도후서 (2 Corinthians) · 18절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Je, tunaanza tena kujipendekeza? Je, tunahitaji barua ya utambulisho kwenu, au kutoka kwenu, kama watu wengine? | Do we begin again to commend ourselves? or need we, as some others, epistles of commendation to you, or letters of commendation from you? |
| 2 | Ninyi wenyewe ni barua yetu; barua iliyoandikwa mioyoni mwetu kila mtu aione na kuisoma. | Ye are our epistle written in our hearts, known and read of all men: |
| 3 | Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua ya Kristo aliyoipeleka kwa mikono yetu. Barua yenyewe imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu hai; imeandikwa si juu ya kipande cha jiwe, bali juu ya mioyo ya watu. | Forasmuch as ye are manifestly declared to be the epistle of Christ ministered by us, written not with ink, but with the Spirit of the living God; not in tables of stone, but in fleshy tables of the heart. |
| 4 | Tunaweza kusema hayo kwa sababu ya tumaini letu tulilo nalo kwa Mungu kwa njia ya Kristo. | And such trust have we through Christ to God-ward: |
| 5 | Si kwamba sisi tunaweza kufanya chochote kwa nguvu zetu wenyewe, ila uwezo wetu wote hutoka kwa Mungu: | Not that we are sufficient of ourselves to think any thing as of ourselves; but our sufficiency is of God; |
| 6 | maana yeye ndiye aliyetuwezesha kulihudumia Agano Jipya ambalo si agano la sheria iliyoandikwa, bali Agano la Roho. Maana sheria iliyoandikwa huleta kifo, lakini Roho huleta uzima. | Who also hath made us able ministers of the new testament; not of the letter, but of the spirit: for the letter killeth, but the spirit giveth life. |
| 7 | Sheria iliwekwa kwa kuandikwa juu ya vipande vya mawe. Ingawaje mwisho wake umekuwa kifo, utukufu wake ulikuwa mkuu mno hata wana wa Israeli wasiweze kuutazama uso wa Mose kwa sababu ya mng'ao wake. Tena mng'ao huo ulikuwa wa muda tu. Basi, ikiwa huduma ya kile ambacho kimesababisha kifo imefanyika kwa utukufu mwingi kiasi hicho, | But if the ministration of death, written and engraven in stones, was glorious, so that the children of Israel could not stedfastly behold the face of Moses for the glory of his countenance; which glory was to be done away: |
| 8 | basi, huduma ya Roho ina utukufu mkuu zaidi. | How shall not the ministration of the spirit be rather glorious? |
| 9 | Ikiwa basi, kulikuwa na utukufu katika huduma ile iliyoleta hukumu, ni wazi kwamba huduma ile iletayo kukubaliwa kuwa waadilifu itakuwa na utukufu mkuu zaidi. | For if the ministration of condemnation be glory, much more doth the ministration of righteousness exceed in glory. |
| 10 | Sasa utukufu mkuu zaidi umechukua nafasi ya ule utukufu uliokuja hapo awali, ambao fahari yake imekwisha toweka. | For even that which was made glorious had no glory in this respect, by reason of the glory that excelleth. |
| 11 | Maana ikiwa kile kilichokuwa cha muda tu kilikuwa na utukufu wake, bila shaka kile chenye kudumu milele kitakuwa na utukufu mkuu zaidi. | For if that which is done away was glorious, much more that which remaineth is glorious. |
| 12 | Kwa vile hili ndilo tumaini letu, sisi twasema kwa uhodari mkuu. | Seeing then that we have such hope, we use great plainness of speech: |
| 13 | Sisi hatufanyi kama Mose ambaye alilazimika kuufunika uso wake kwa kitambaa ili watu wa Israeli wasiuone ule mwisho wa mng'ao uliokuwa unafifia. | And not as Moses, which put a vail over his face, that the children of Israel could not stedfastly look to the end of that which is abolished: |
| 14 | Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu mtu anapoungana na Kristo. | But their minds were blinded: for until this day remaineth the same vail untaken away in the reading of the old testament; which vail is done away in Christ. |
| 15 | Naam, mpaka hivi leo kila isomwapo Sheria ya Mose akili zao huwa zimefunikwa. | But even unto this day, when Moses is read, the vail is upon their heart. |
| 16 | Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa. | Nevertheless when it shall turn to the Lord, the vail shall be taken away. |
| 17 | Hapa "Bwana" ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru. | Now the Lord is that Spirit: and where the Spirit of the Lord is, there is liberty. |
| 18 | Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, twaonyesha kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana. | But we all, with open face beholding as in a glass the glory of the Lord, are changed into the same image from glory to glory, even as by the Spirit of the Lord. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL