고린도후서 2장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 고린도후서 (2 Corinthians) · 17절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Basi nimeamua nisiwatembelee tena kuwatia huzuni. | But I determined this with myself, that I would not come again to you in heaviness. |
| 2 | Maana nikiwahuzunisha ninyi, basi, ni nani atakayenifariji? Ni walewale niliowahuzunisha! | For if I make you sorry, who is he then that maketh me glad, but the same which is made sorry by me? |
| 3 | Ndiyo maana niliwaandikia--sikutaka kuja kwenu na kuhuzunishwa na ninyi ambao ndio mngepaswa kuwa furaha yangu. Nina hakika kwamba, mimi nikifurahi, ninyi nyote pia mnafurahi. | And I wrote this same unto you, lest, when I came, I should have sorrow from them of whom I ought to rejoice; having confidence in you all, that my joy is the joy of you all. |
| 4 | Nilipowaandikia hapo awali katika hali ya huzuni na sikitiko moyoni na kwa machozi mengi, haikuwa kwa ajili ya kuwahuzunisha ninyi, bali kwa ajili ya kuwaonyesheni kwamba nawapenda mno. | For out of much affliction and anguish of heart I wrote unto you with many tears; not that ye should be grieved, but that ye might know the love which I have more abundantly unto you. |
| 5 | Ikiwa kuna mtu aliyemhuzunisha mwingine, hakunihuzunisha mimi--ila amewahuzunisha ninyi nyote, na sipendi kuwa mkali zaidi. | But if any have caused grief, he hath not grieved me, but in part: that I may not overcharge you all. |
| 6 | Adhabu aliyokwisha pata kutoka kwa wengi wenu inamtosha. | Sufficient to such a man is this punishment, which was inflicted of many. |
| 7 | Iliyobakia ni afadhali kwenu kumsamehe mtu huyo na kumpa moyo ili asije akahuzunika mno na kukata tamaa kabisa. | So that contrariwise ye ought rather to forgive him, and comfort him, lest perhaps such a one should be swallowed up with overmuch sorrow. |
| 8 | Kwa hiyo nawasihi: mwonyesheni kwamba mnampenda. | Wherefore I beseech you that ye would confirm your love toward him. |
| 9 | Madhumuni yangu kuandika ile barua yalikuwa kutaka kujua kama mko tayari kutii katika kila jambo. | For to this end also did I write, that I might know the proof of you, whether ye be obedient in all things. |
| 10 | Mkimsamehe mtu, nami pia ninamsamehe. Maana ninaposamehe--kama kweli ninacho cha kusamehe--nasamehe mbele ya Kristo kwa ajili yenu, | To whom ye forgive any thing, I forgive also: for if I forgave any thing, to whom I forgave it, for your sakes forgave I it in the person of Christ; |
| 11 | ili tusimpe nafasi Shetani atudanganye; maana twaijua mipango yake ilivyo. | Lest Satan should get an advantage of us: for we are not ignorant of his devices. |
| 12 | Nilipofika Troa kuhubiri Habari Njema ya Kristo, nilikuta mlango u wazi kwa ajili ya kazi ya Bwana. | Furthermore, when I came to Troas to preach Christ’s gospel, and a door was opened unto me of the Lord, |
| 13 | Lakini nilifadhaika sana kwa kutomkuta ndugu yetu Tito. Ndiyo maana niliwaaga wote pale nikaenda Makedonia. | I had no rest in my spirit, because I found not Titus my brother: but taking my leave of them, I went from thence into Macedonia. |
| 14 | Lakini, shukrani kwa Mungu anayetuongoza daima katika msafara wa ushindi wa Kristo. Yeye hutufanya tuueneze ukweli wa Kristo kama harufu nzuri, kila mahali. | Now thanks be unto God, which always causeth us to triumph in Christ, and maketh manifest the savour of his knowledge by us in every place. |
| 15 | Maana sisi ni kama harufu nzuri ya ubani ambayo Kristo anamtolea Mungu, harufu nzuri inayofikia wote wanaookolewa na wanaopotea. | For we are unto God a sweet savour of Christ, in them that are saved, and in them that perish: |
| 16 | Kwa wale wanaopotea, harufu hiyo ni kifo; lakini kwa wale wanaookolewa, harufu hiyo ni uhai. Nani basi, awezaye kushiriki katika kazi ya namna hiyo? | To the one we are the savour of death unto death; and to the other the savour of life unto life. And who is sufficient for these things? |
| 17 | Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo. | For we are not as many, which corrupt the word of God: but as of sincerity, but as of God, in the sight of God speak we in Christ. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL