로그인

고린도전서 9장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 고린도전서 (1 Corinthians) · 27절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana? Am I not an apostle? am I not free? have I not seen Jesus Christ our Lord? are not ye my work in the Lord?
2 Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana. If I be not an apostle unto others, yet doubtless I am to you: for the seal of mine apostleship are ye in the Lord.
3 Hoja yangu kwa wale wanaonipinga ndiyo hii: Mine answer to them that do examine me is this,
4 Je, hatuna haki ya kula na kunywa? Have we not power to eat and to drink?
5 Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristo katika ziara zetu, kama vile wafanyavyo mitume wengine, ndugu zake Bwana, na pia Kefa? Have we not power to lead about a sister, a wife, as well as other apostles, and as the brethren of the Lord, and Cephas?
6 Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi? Or I only and Barnabas, have not we power to forbear working?
7 Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake? Who goeth a warfare any time at his own charges? who planteth a vineyard, and eateth not of the fruit thereof? or who feedeth a flock, and eateth not of the milk of the flock?
8 Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, Sheria nayo haisemi hivyo? Say I these things as a man? or saith not the law the same also?
9 Imeandikwa katika Sheria ya Mose: "Usimfunge kinywa ng'ombe anapoliwata nafaka." Je, ndio kusema Mungu anajishughulisha na ng'ombe? For it is written in the law of Moses, Thou shalt not muzzle the mouth of the ox that treadeth out the corn. Doth God take care for oxen?
10 Je, hakuwa anatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, haya yaliandikwa kwa ajili yetu; kwani yule anayelima na yule anayevuna, wote wawili wana haki ya kutumaini kupata sehemu ya mavuno. Or saith he it altogether for our sakes? For our sakes, no doubt, this is written: that he that ploweth should plow in hope; and that he that thresheth in hope should be partaker of his hope.
11 Ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambo kubwa tukichuma kwenu faida ya kidunia? If we have sown unto you spiritual things, is it a great thing if we shall reap your carnal things?
12 Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo, Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo. If others be partakers of this power over you, are not we rather? Nevertheless we have not used this power; but suffer all things, lest we should hinder the gospel of Christ.
13 Je, hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupata chakula chao Hekaluni, na kwamba wanaotolea sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka? Do ye not know that they which minister about holy things live of the things of the temple? and they which wait at the altar are partakers with the altar?
14 Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo. Even so hath the Lord ordained that they which preach the gospel should live of the gospel.
15 Lakini, mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aone kwamba najisifu bure. But I have used none of these things: neither have I written these things, that it should be so done unto me: for it were better for me to die, than that any man should make my glorying void.
16 Ikiwa ninaihubiri Habari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema! For though I preach the gospel, I have nothing to glory of: for necessity is laid upon me; yea, woe is unto me, if I preach not the gospel!
17 Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini maadam naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze. For if I do this thing willingly, I have a reward: but if against my will, a dispensation of the gospel is committed unto me.
18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri. What is my reward then? Verily that, when I preach the gospel, I may make the gospel of Christ without charge, that I abuse not my power in the gospel.
19 Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo. For though I be free from all men, yet have I made myself servant unto all, that I might gain the more.
20 Kwa Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapate Wayahudi; yaani, ingawa mimi siko chini ya Sheria, nimejiweka chini ya Sheria kwao, ili niwapate hao walio chini ya Sheria. And unto the Jews I became as a Jew, that I might gain the Jews; to them that are under the law, as under the law, that I might gain them that are under the law;
21 Na kwa wale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, nje ya Sheria, ili niwapate hao walio nje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo. To them that are without law, as without law, (being not without law to God, but under the law to Christ,) that I might gain them that are without law.
22 Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia. To the weak became I as weak, that I might gain the weak: I am made all things to all men, that I might by all means save some.
23 Nafanya haya yote kwa ajili ya Habari Njema, nipate kushiriki baraka zake. And this I do for the gospel’s sake, that I might be partaker thereof with you.
24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi? Know ye not that they which run in a race run all, but one receiveth the prize? So run, that ye may obtain.
25 Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji ya kudumu daima. And every man that striveth for the mastery is temperate in all things. Now they do it to obtain a corruptible crown; but we an incorruptible.
26 Ndivyo basi, ninavyopiga mbio nikiwa na nia ya kushinda; ndivyo ninavyopigana, na si kama bondia anayetupa ngumi zake hewani. I therefore so run, not as uncertainly; so fight I, not as one that beateth the air:
27 Naupa mwili wangu mazoezi magumu na kuutia katika nidhamu kamili, nisije mimi mwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine. But I keep under my body, and bring it into subjection: lest that by any means, when I have preached to others, I myself should be a castaway.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL