고린도전서 8장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 고린도전서 (1 Corinthians) · 13절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga. | Now as touching things offered unto idols, we know that we all have knowledge. Knowledge puffeth up, but charity edifieth. |
| 2 | Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa. | And if any man think that he knoweth any thing, he knoweth nothing yet as he ought to know. |
| 3 | Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye. | But if any man love God, the same is known of him. |
| 4 | Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu. | As concerning therefore the eating of those things that are offered in sacrifice unto idols, we know that an idol is nothing in the world, and that there is none other God but one. |
| 5 | Hata kama viko vitu viitwavyo miungu duniani au mbinguni, na hata kama wako miungu na mabwana wengi, | For though there be that are called gods, whether in heaven or in earth, (as there be gods many, and lords many,) |
| 6 | hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia yake. | But to us there is but one God, the Father, of whom are all things, and we in him; and one Lord Jesus Christ, by whom are all things, and we by him. |
| 7 | Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi. | Howbeit there is not in every man that knowledge: for some with conscience of the idol unto this hour eat it as a thing offered unto an idol; and their conscience being weak is defiled. |
| 8 | Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu. | But meat commendeth us not to God: for neither, if we eat, are we the better; neither, if we eat not, are we the worse. |
| 9 | Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi. | But take heed lest by any means this liberty of yours become a stumblingblock to them that are weak. |
| 10 | Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu? | For if any man see thee which hast knowledge sit at meat in the idol’s temple, shall not the conscience of him which is weak be emboldened to eat those things which are offered to idols; |
| 11 | Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako. | And through thy knowledge shall the weak brother perish, for whom Christ died? |
| 12 | Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo. | But when ye sin so against the brethren, and wound their weak conscience, ye sin against Christ. |
| 13 | Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi. | Wherefore, if meat make my brother to offend, I will eat no flesh while the world standeth, lest I make my brother to offend. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL