고린도전서 16장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 고린도전서 (1 Corinthians) · 24절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Sasa, yahusu ule mchango kwa ajili ya watu wa Mungu: fanyeni kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia. | Now concerning the collection for the saints, as I have given order to the churches of Galatia, even so do ye. |
| 2 | Kila Jumapili kila mmoja wenu atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake, ili kusiwe na haja ya kufanya mchango wakati nitakapokuja. | Upon the first day of the week let every one of you lay by him in store, as God hath prospered him, that there be no gatherings when I come. |
| 3 | Wakati nitakapokuja kwenu, nitawatuma wale mtakaowachagua miongoni mwenu wapeleke barua na zawadi zenu Yerusalemu. | And when I come, whomsoever ye shall approve by your letters, them will I send to bring your liberality unto Jerusalem. |
| 4 | Kama itafaa nami niende, basi, watakwenda pamoja nami. | And if it be meet that I go also, they shall go with me. |
| 5 | Nitakuja kwenu, baada ya kupitia Makedonia--maana nataraji kupitia Makedonia. | Now I will come unto you, when I shall pass through Macedonia: for I do pass through Macedonia. |
| 6 | Labda nitakaa kwenu kwa muda fulani, au huenda nitakaa pamoja nanyi wakati wote wa baridi, ili mpate kunisaidia niendelee na safari yangu kokote nitakakokwenda. | And it may be that I will abide, yea, and winter with you, that ye may bring me on my journey whithersoever I go. |
| 7 | Sipendi kupita kwenu harakaharaka na kuendelea na safari. Natumaini kukaa kwenu kwa kitambo fulani, Bwana akiniruhusu. | For I will not see you now by the way; but I trust to tarry a while with you, if the Lord permit. |
| 8 | Lakini nitabaki hapa Efeso mpaka siku ya Pentekoste. | But I will tarry at Ephesus until Pentecost. |
| 9 | Mlango uko wazi kabisa kwa ajili ya kazi yangu muhimu hapa, ingawa wapinzani nao ni wengi. | For a great door and effectual is opened unto me, and there are many adversaries. |
| 10 | Timotheo akija, angalieni asiwe na hofu yoyote wakati yupo kati yenu, kwani anafanya kazi ya Bwana kama mimi. | Now if Timotheus come, see that he may be with you without fear: for he worketh the work of the Lord, as I also do. |
| 11 | Kwa hiyo mtu yeyote asimdharau, ila msaidieni aendelee na safari yake kwa amani ili aweze kurudi kwangu, maana mimi namngojea pamoja na ndugu zetu. | Let no man therefore despise him: but conduct him forth in peace, that he may come unto me: for I look for him with the brethren. |
| 12 | Kuhusu ndugu Apolo, nimemsihi sana aje kwenu pamoja na ndugu wengine, lakini hapendelei kabisa kuja sasa ila atakuja mara itakapowezekana. | As touching our brother Apollos, I greatly desired him to come unto you with the brethren: but his will was not at all to come at this time; but he will come when he shall have convenient time. |
| 13 | Kesheni, simameni imara katika imani, muwe hodari na wenye nguvu. | Watch ye, stand fast in the faith, quit you like men, be strong. |
| 14 | Kila mfanyacho kifanyike kwa upendo. | Let all your things be done with charity. |
| 15 | Ndugu, mnaifahamu jamaa ya Stefana; wao ni watu wa kwanza kabisa kuipokea imani ya Kikristo katika Akaya, na wamejitolea kuwatumikia watu wa Mungu. Ninawasihi ninyi ndugu zangu, | I beseech you, brethren, (ye know the house of Stephanas, that it is the firstfruits of Achaia, and that they have addicted themselves to the ministry of the saints,) |
| 16 | muufuate uongozi wa watu kama hao, na uongozi wa kila mtu afanyaye kazi na kutumikia pamoja nao. | That ye submit yourselves unto such, and to every one that helpeth with us, and laboureth. |
| 17 | Nafurahi sana kwamba Stefana, Fortunato na Akaiko wamefika; wamelijaza pengo lililokuwako kwa kutokuwako kwenu. | I am glad of the coming of Stephanas and Fortunatus and Achaicus: for that which was lacking on your part they have supplied. |
| 18 | Wameiburudisha roho yangu na yenu pia. Kwa hiyo inafaa kuwakumbuka watu wa namna hii. | For they have refreshed my spirit and yours: therefore acknowledge ye them that are such. |
| 19 | Makanisa yote ya Asia yanawasalimuni. Akula na Priskila pamoja na watu wote wa Mungu walio nyumbani mwao wanawasalimuni sana katika Bwana. | The churches of Asia salute you. Aquila and Priscilla salute you much in the Lord, with the church that is in their house. |
| 20 | Ndugu wote wanawasalimuni. Nanyi salimianeni kwa ishara ya mapendo ya Mungu. | All the brethren greet you. Greet ye one another with an holy kiss. |
| 21 | Mimi Paulo nawasalimuni, nikiandika kwa mkono wangu mwenyewe. | The salutation of me Paul with mine own hand. |
| 22 | Yeyote asiyempenda Bwana, na alaaniwe. MARANA THA--BWANA, njoo! | If any man love not the Lord Jesus Christ, let him be Anathema Maran-atha. |
| 23 | Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. | The grace of our Lord Jesus Christ be with you. |
| 24 | Mapendo yangu yawe kwenu katika kuungana na Kristo Yesu. | My love be with you all in Christ Jesus. Amen. The first epistle to the Corinthians was written from Philippi by Stephanas, and Fortunatus, and Achaicus, and Timotheus. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL