고린도전서 15장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 고린도전서 (1 Corinthians) · 58절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake. | Moreover, brethren, I declare unto you the gospel which I preached unto you, which also ye have received, and wherein ye stand; |
| 2 | Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure. | By which also ye are saved, if ye keep in memory what I preached unto you, unless ye have believed in vain. |
| 3 | Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu; | For I delivered unto you first of all that which I also received, how that Christ died for our sins according to the scriptures; |
| 4 | kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa; | And that he was buried, and that he rose again the third day according to the scriptures: |
| 5 | kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili. | And that he was seen of Cephas, then of the twelve: |
| 6 | Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa. | After that, he was seen of above five hundred brethren at once; of whom the greater part remain unto this present, but some are fallen asleep. |
| 7 | Baadaye alimtokea Yakobo kisha akawatokea mitume wote. | After that, he was seen of James; then of all the apostles. |
| 8 | Baada ya wote, akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu aliyezaliwa kabla ya wakati. | And last of all he was seen of me also, as of one born out of due time. |
| 9 | Maana mimi ni mdogo kabisa miongoni mwa mitume na wala sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililidhulumu kanisa la Mungu. | For I am the least of the apostles, that am not meet to be called an apostle, because I persecuted the church of God. |
| 10 | Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami. | But by the grace of God I am what I am: and his grace which was bestowed upon me was not in vain; but I laboured more abundantly than they all: yet not I, but the grace of God which was with me. |
| 11 | Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirio au mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndicho tunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini. | Therefore whether it were I or they, so we preach, and so ye believed. |
| 12 | Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu? | Now if Christ be preached that he rose from the dead, how say some among you that there is no resurrection of the dead? |
| 13 | Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi, Kristo naye hakufufuka; | But if there be no resurrection of the dead, then is Christ not risen: |
| 14 | na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana. | And if Christ be not risen, then is our preaching vain, and your faith is also vain. |
| 15 | Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua--kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi. | Yea, and we are found false witnesses of God; because we have testified of God that he raised up Christ: whom he raised not up, if so be that the dead rise not. |
| 16 | Maana, ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristo hakufufuka. | For if the dead rise not, then is not Christ raised: |
| 17 | Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu. | And if Christ be not raised, your faith is vain; ye are yet in your sins. |
| 18 | Zaidi ya hayo, wale wote waliokufa wakiwa wameungana na Kristo wamepotea kabisa. | Then they also which are fallen asleep in Christ are perished. |
| 19 | Kama matumaini yetu katika Kristo yanahusu tu maisha haya ya sasa, basi, sisi ni watu wa kusikitikiwa zaidi kuliko wengine wote duniani. | If in this life only we have hope in Christ, we are of all men most miserable. |
| 20 | Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, limbuko lao wale waliolala katika kifo. | But now is Christ risen from the dead, and become the firstfruits of them that slept. |
| 21 | Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutoka wafu kumesababishwa na mtu mmoja. | For since by man came death, by man came also the resurrection of the dead. |
| 22 | Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo. | For as in Adam all die, even so in Christ shall all be made alive. |
| 23 | Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristo kwanza, halafu wale walio wake Kristo wakati Kristo atakapokuja. | But every man in his own order: Christ the firstfruits; afterward they that are Christ’s at his coming. |
| 24 | Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu. | Then cometh the end, when he shall have delivered up the kingdom to God, even the Father; when he shall have put down all rule and all authority and power. |
| 25 | Maana Kristo sharti atawale mpaka Mungu atakapowashinda adui zake na kuwaweka chini ya miguu yake. | For he must reign, till he hath put all enemies under his feet. |
| 26 | Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo. | The last enemy that shall be destroyed is death. |
| 27 | Maana, Maandiko yasema: "Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake." Lakini, Maandiko yanaposema: "Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale" ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo. | For he hath put all things under his feet. But when he saith all things are put under him, it is manifest that he is excepted, which did put all things under him. |
| 28 | Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya Utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya Utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote. | And when all things shall be subdued unto him, then shall the Son also himself be subject unto him that put all things under him, that God may be all in all. |
| 29 | Kama hakuna ufufuo, je watu wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu wanatumainia kupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya nini kubatizwa kwa ajili yao? | Else what shall they do which are baptized for the dead, if the dead rise not at all? why are they then baptized for the dead? |
| 30 | Na sisi, ya nini kujitia hatarini kila saa? | And why stand we in jeopardy every hour? |
| 31 | Ndugu, mimi nakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayo juu yenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetu inanifanya nitangaze jambo hili. | I protest by your rejoicing which I have in Christ Jesus our Lord, I die daily. |
| 32 | Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, "Tule na tunywe, maana kesho tutakufa." | If after the manner of men I have fought with beasts at Ephesus, what advantageth it me, if the dead rise not? let us eat and drink; for to morrow we die. |
| 33 | Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema. | Be not deceived: evil communications corrupt good manners. |
| 34 | Amkeni! Anzeni kuishi vema, na acheni kutenda dhambi. Baadhi yenu hawamjui Mungu kabisa. Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu! | Awake to righteousness, and sin not; for some have not the knowledge of God: I speak this to your shame. |
| 35 | Lakini mtu anaweza kuuliza: "Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?" | But some man will say, How are the dead raised up? and with what body do they come? |
| 36 | Hayo ni maswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufa kwanza haitaota. | Thou fool, that which thou sowest is not quickened, except it die: |
| 37 | Unachopanda ni mbegu tu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na si mmea mzima ambao hutokea baadaye. | And that which thou sowest, thou sowest not that body that shall be, but bare grain, it may chance of wheat, or of some other grain: |
| 38 | Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutaka mwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wa pekee. | But God giveth it a body as it hath pleased him, and to every seed his own body. |
| 39 | Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu ni ya namna moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, ya ndege ni ya namna nyingine na miili ya samaki pia ni ya namna nyingine. | All flesh is not the same flesh: but there is one kind of flesh of men, another flesh of beasts, another of fishes, and another of birds. |
| 40 | Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani; uzuri wa miili ya mbinguni ni mwingine, na na uzuri wa miili ya duniani ni mwingine. | There are also celestial bodies, and bodies terrestrial: but the glory of the celestial is one, and the glory of the terrestrial is another. |
| 41 | Uko uzuri wa jua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo huhitilafiana kwa uzuri. | There is one glory of the sun, and another glory of the moon, and another glory of the stars: for one star differeth from another star in glory. |
| 42 | Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu. Kama vile mbegu, mwili huzikwa ardhini ukiwa katika hali ya kuharibika, lakini hufufuliwa katika hali ya kutoharibika. | So also is the resurrection of the dead. It is sown in corruption; it is raised in incorruption: |
| 43 | Huzikwa katika hali duni, hufufuliwa katika hali tukufu; huzikwa katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwa wenye nguvu. | It is sown in dishonour; it is raised in glory: it is sown in weakness; it is raised in power: |
| 44 | Unapozikwa ni mwili wa kawaida, unapofufuliwa ni mwili wa kiroho. Kuna mwili wa kawaida na kutakuwa na mwili wa kiroho. | It is sown a natural body; it is raised a spiritual body. There is a natural body, and there is a spiritual body. |
| 45 | Maana Maandiko yasema: "Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe mwenye uhai;" lakini adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uzima. | And so it is written, The first man Adam was made a living soul; the last Adam was made a quickening spirit. |
| 46 | Lakini unaotangulia kuwako si ule mwili wa kiroho, ila ule mwili wa kawaida kisha ule mwili wa kiroho. | Howbeit that was not first which is spiritual, but that which is natural; and afterward that which is spiritual. |
| 47 | Adamu wa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtu wa pili alitoka mbinguni. | The first man is of the earth, earthy: the second man is the Lord from heaven. |
| 48 | Wote walio wa dunia wako kama huyo mtu aliyeumbwa kwa udongo; wale walio wa mbinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni. | As is the earthy, such are they also that are earthy: and as is the heavenly, such are they also that are heavenly. |
| 49 | Kama vile tulivyofanana na yule aliyeumbwa kwa udongo, vivyo hivyo tutafanana na huyohuyo aliyetoka mbinguni. | And as we have borne the image of the earthy, we shall also bear the image of the heavenly. |
| 50 | Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika. | Now this I say, brethren, that flesh and blood cannot inherit the kingdom of God; neither doth corruption inherit incorruption. |
| 51 | Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa | Behold, I shew you a mystery; We shall not all sleep, but we shall all be changed, |
| 52 | wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana mbiu itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa. | In a moment, in the twinkling of an eye, at the last trump: for the trumpet shall sound, and the dead shall be raised incorruptible, and we shall be changed. |
| 53 | Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa. | For this corruptible must put on incorruption, and this mortal must put on immortality. |
| 54 | Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: "Kifo kimeangamizwa ushindi umekamilika!" | So when this corruptible shall have put on incorruption, and this mortal shall have put on immortality, then shall be brought to pass the saying that is written, Death is swallowed up in victory. |
| 55 | "Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?" | O death, where is thy sting? O grave, where is thy victory? |
| 56 | Ukali wa kifo hutokana na dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika Sheria. | The sting of death is sin; and the strength of sin is the law. |
| 57 | Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. | But thanks be to God, which giveth us the victory through our Lord Jesus Christ. |
| 58 | Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure. | Therefore, my beloved brethren, be ye stedfast, unmoveable, always abounding in the work of the Lord, forasmuch as ye know that your labour is not in vain in the Lord. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL