히브리서 13장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 히브리서 (Hebrews) · 25절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Endeleeni kupendana kidugu. | Let brotherly love continue. |
| 2 | Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua. | Be not forgetful to entertain strangers: for thereby some have entertained angels unawares. |
| 3 | Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao. | Remember them that are in bonds, as bound with them; and them which suffer adversity, as being yourselves also in the body. |
| 4 | Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi. | Marriage is honourable in all, and the bed undefiled: but whoremongers and adulterers God will judge. |
| 5 | Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: "Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa." | Let your conversation be without covetousness; and be content with such things as ye have: for he hath said, I will never leave thee, nor forsake thee. |
| 6 | Ndiyo maana tunathubutu kusema: "Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?" | So that we may boldly say, The Lord is my helper, and I will not fear what man shall do unto me. |
| 7 | wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu. Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao. | Remember them which have the rule over you, who have spoken unto you the word of God: whose faith follow, considering the end of their conversation. |
| 8 | Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele. | Jesus Christ the same yesterday, and to day, and for ever. |
| 9 | Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata. | Be not carried about with divers and strange doctrines. For it is a good thing that the heart be established with grace; not with meats, which have not profited them that have been occupied therein. |
| 10 | Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake. | We have an altar, whereof they have no right to eat which serve the tabernacle. |
| 11 | Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi. | For the bodies of those beasts, whose blood is brought into the sanctuary by the high priest for sin, are burned without the camp. |
| 12 | Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji. | Wherefore Jesus also, that he might sanctify the people with his own blood, suffered without the gate. |
| 13 | Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake. | Let us go forth therefore unto him without the camp, bearing his reproach. |
| 14 | Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja. | For here have we no continuing city, but we seek one to come. |
| 15 | Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa na midomo inayoliungama jina lake. | By him therefore let us offer the sacrifice of praise to God continually, that is, the fruit of our lips giving thanks to his name. |
| 16 | Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu zinazompendeza Mungu. | But to do good and to communicate forget not: for with such sacrifices God is well pleased. |
| 17 | Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu. | Obey them that have the rule over you, and submit yourselves: for they watch for your souls, as they that must give account, that they may do it with joy, and not with grief: for that is unprofitable for you. |
| 18 | Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima. | Pray for us: for we trust we have a good conscience, in all things willing to live honestly. |
| 19 | Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi iwezekanavyo. | But I beseech you the rather to do this, that I may be restored to you the sooner. |
| 20 | Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. | Now the God of peace, that brought again from the dead our Lord Jesus, that great shepherd of the sheep, through the blood of the everlasting covenant, |
| 21 | Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze mapenzi yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina. | Make you perfect in every good work to do his will, working in you that which is wellpleasing in his sight, through Jesus Christ; to whom be glory for ever and ever. Amen. |
| 22 | Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni. | And I beseech you, brethren, suffer the word of exhortation: for I have written a letter unto you in few words. |
| 23 | Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja kwenu. | Know ye that our brother Timothy is set at liberty; with whom, if he come shortly, I will see you. |
| 24 | Wasalimieni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italia wanawasalimuni. | Salute all them that have the rule over you, and all the saints. They of Italy salute you. |
| 25 | Tunawatakieni nyote neema ya Mungu. | Grace be with you all. Amen. Written to the Hebrews from Italy by Timothy. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL