요한복음 4장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 요한복음 (John) · 54절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane. | When therefore the Lord knew how the Pharisees had heard that Jesus made and baptized more disciples than John, |
| 2 | (Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.) | (Though Jesus himself baptized not, but his disciples,) |
| 3 | Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya; | He left Judea, and departed again into Galilee. |
| 4 | na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria. | And he must needs go through Samaria. |
| 5 | Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu. | Then cometh he to a city of Samaria, which is called Sychar, near to the parcel of ground that Jacob gave to his son Joseph. |
| 6 | Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. | Now Jacob’s well was there. Jesus therefore, being wearied with his journey, sat thus on the well: and it was about the sixth hour. |
| 7 | Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, "Nipatie maji ninywe." | There cometh a woman of Samaria to draw water: Jesus saith unto her, Give me to drink. |
| 8 | (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.) | (For his disciples were gone away unto the city to buy meat.) |
| 9 | Lakini huyo mwanamke akamwambia, "Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?" (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu.) | Then saith the woman of Samaria unto him, How is it that thou, being a Jew, askest drink of me, which am a woman of Samaria? for the Jews have no dealings with the Samaritans. |
| 10 | Yesu akamjibu, "Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekwambia: Nipatie maji ninywe, ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yaliyo hai." | Jesus answered and said unto her, If thou knewest the gift of God, and who it is that saith to thee, Give me to drink; thou wouldest have asked of him, and he would have given thee living water. |
| 11 | Huyo mama akasema, "Mheshimiwa, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yaliyo hai? | The woman saith unto him, Sir, thou hast nothing to draw with, and the well is deep: from whence then hast thou that living water? |
| 12 | Au, labda wewe wajifanya mkuu kuliko babu yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo yake walikunywa maji ya kisima hiki." | Art thou greater than our father Jacob, which gave us the well, and drank thereof himself, and his children, and his cattle? |
| 13 | Yesu akamjibu, "Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. | Jesus answered and said unto her, Whosoever drinketh of this water shall thirst again: |
| 14 | Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uzima na kumpatia uzima wa milele." | But whosoever drinketh of the water that I shall give him shall never thirst; but the water that I shall give him shall be in him a well of water springing up into everlasting life. |
| 15 | Huyo mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, nipe maji hayo ili nisione kiu tena; nisije tena mpaka hapa kuteka maji." | The woman saith unto him, Sir, give me this water, that I thirst not, neither come hither to draw. |
| 16 | Yesu akamwambia, "Nenda ukamwite mumeo uje naye hapa." | Jesus saith unto her, Go, call thy husband, and come hither. |
| 17 | Huyo mwanamke akamwambia, "Mimi sina mume." Yesu akamwambia, "Umesema kweli, kwamba huna mume. | The woman answered and said, I have no husband. Jesus said unto her, Thou hast well said, I have no husband: |
| 18 | Maana umekuwa na waume watano, na huyo unayeishi naye sasa si mume wako. Hapo umesema kweli." | For thou hast had five husbands; and he whom thou now hast is not thy husband: in that saidst thou truly. |
| 19 | Huyo Mwanamke akamwambia, "Mheshimiwa, naona ya kuwa wewe u nabii. | The woman saith unto him, Sir, I perceive that thou art a prophet. |
| 20 | Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini ninyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudu Mungu ni kule Yerusalemu." | Our fathers worshipped in this mountain; and ye say, that in Jerusalem is the place where men ought to worship. |
| 21 | Yesu akamwambia, "Niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba juu ya mlima huu, wala kule Yerusalemu. | Jesus saith unto her, Woman, believe me, the hour cometh, when ye shall neither in this mountain, nor yet at Jerusalem, worship the Father. |
| 22 | Ninyi Wasamaria mnamwabudu yule msiyemjua, lakini sisi tunamjua huyo tunayemwabudu, kwa maana wokovu unatoka kwa Wayahudi. | Ye worship ye know not what: we know what we worship: for salvation is of the Jews. |
| 23 | Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka. | But the hour cometh, and now is, when the true worshippers shall worship the Father in spirit and in truth: for the Father seeketh such to worship him. |
| 24 | Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake." | God is a Spirit: and they that worship him must worship him in spirit and in truth. |
| 25 | Huyo mama akamwambia, "Najua kwamba Masiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu." | The woman saith unto him, I know that Messias cometh, which is called Christ: when he is come, he will tell us all things. |
| 26 | Yesu akamwambia, "Mimi ninayesema nawe, ndiye." | Jesus saith unto her, I that speak unto thee am he. |
| 27 | Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: "Unataka nini?" au, "Kwa nini unaongea na mwanamke?" | And upon this came his disciples, and marvelled that he talked with the woman: yet no man said, What seekest thou? or, Why talkest thou with her? |
| 28 | Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu, | The woman then left her waterpot, and went her way into the city, and saith to the men, |
| 29 | "Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?" | Come, see a man, which told me all things that ever I did: is not this the Christ? |
| 30 | Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu. | Then they went out of the city, and came unto him. |
| 31 | Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: "Mwalimu, ule chakula." | In the mean while his disciples prayed him, saying, Master, eat. |
| 32 | Lakini Yesu akawaambia, "Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi." | But he said unto them, I have meat to eat that ye know not of. |
| 33 | Wanafunzi wake wakaulizana, "Je, kuna mtu aliyemletea chakula?" | Therefore said the disciples one to another, Hath any man brought him ought to eat? |
| 34 | Yesu akawaambia, "Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake. | Jesus saith unto them, My meat is to do the will of him that sent me, and to finish his work. |
| 35 | Ninyi mwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa. | Say not ye, There are yet four months, and then cometh harvest? behold, I say unto you, Lift up your eyes, and look on the fields; for they are white already to harvest. |
| 36 | Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja. | And he that reapeth receiveth wages, and gathereth fruit unto life eternal: that both he that soweth and he that reapeth may rejoice together. |
| 37 | Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: Mmoja hupanda na mwingine huvuna. | And herein is that saying true, One soweth, and another reapeth. |
| 38 | Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanya kazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao." | I sent you to reap that whereon ye bestowed no labour: other men laboured, and ye are entered into their labours. |
| 39 | Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: "Ameniambia mambo yote niliyofanya." | And many of the Samaritans of that city believed on him for the saying of the woman, which testified, He told me all that ever I did. |
| 40 | Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili. | So when the Samaritans were come unto him, they besought him that he would tarry with them: and he abode there two days. |
| 41 | Watu wengi zaidi walimwamini kwa sababu ya ujumbe wake. | And many more believed because of his own word; |
| 42 | Wakamwambia yule mama, "Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu." | And said unto the woman, Now we believe, not because of thy saying: for we have heard him ourselves, and know that this is indeed the Christ, the Saviour of the world. |
| 43 | Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo, akaenda Galilaya. | Now after two days he departed thence, and went into Galilee. |
| 44 | Maana Yesu mwenyewe alisema waziwazi kwamba, "Nabii hapati heshima katika nchi yake." | For Jesus himself testified, that a prophet hath no honour in his own country. |
| 45 | Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo. | Then when he was come into Galilee, the Galileans received him, having seen all the things that he did at Jerusalem at the feast: for they also went unto the feast. |
| 46 | Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu. | So Jesus came again into Cana of Galilee, where he made the water wine. And there was a certain nobleman, whose son was sick at Capernaum. |
| 47 | Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi. | When he heard that Jesus was come out of Judea into Galilee, he went unto him, and besought him that he would come down, and heal his son: for he was at the point of death. |
| 48 | Yesu akamwambia, "Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!" | Then said Jesus unto him, Except ye see signs and wonders, ye will not believe. |
| 49 | Huyo ofisa akamwambia, "Mheshimiwa, tafadhali twende kabla mwanangu hajafa." | The nobleman saith unto him, Sir, come down ere my child die. |
| 50 | Yesu akamwambia, "Nenda tu, mwanao yu mzima." Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake. | Jesus saith unto him, Go thy way; thy son liveth. And the man believed the word that Jesus had spoken unto him, and he went his way. |
| 51 | Alipokuwa bado njiani, watumishi wake walikutana naye, wakamwambia kwamba mwanawe alikuwa mzima. | And as he was now going down, his servants met him, and told him, saying, Thy son liveth. |
| 52 | Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, "Jana saa saba mchana, homa ilimwacha." | Then enquired he of them the hour when he began to amend. And they said unto him, Yesterday at the seventh hour the fever left him. |
| 53 | Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: "Mwanao yu mzima." Basi, yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote. | So the father knew that it was at the same hour, in the which Jesus said unto him, Thy son liveth: and himself believed, and his whole house. |
| 54 | Hii ilikuwa ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipokuwa anatoka Yudea kwenda Galilaya. | This is again the second miracle that Jesus did, when he was come out of Judea into Galilee. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL