야고보서 4장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 야고보서 (James) · 17절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Mapigano na magombano yote kati yenu yanatoka wapi? Hutoka katika tamaa zenu mbaya ambazo hupigana daima ndani yenu. | From whence come wars and fightings among you? come they not hence, even of your lusts that war in your members? |
| 2 | Mnatamani vitu na kwa vile hamvipati mko tayari kuua; mwatamani sana kupata vitu, lakini hamvipati, hivyo mnagombana na kupigana. Hampati kile mnachotaka kwa sababu hamkiombi kwa Mungu. | Ye lust, and have not: ye kill, and desire to have, and cannot obtain: ye fight and war, yet ye have not, because ye ask not. |
| 3 | Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. | Ye ask, and receive not, because ye ask amiss, that ye may consume it upon your lusts. |
| 4 | Ninyi ni watu msio na uaminifu kama wazinzi. Je, hamjui kwamba kuwa rafiki wa ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Yeyote anayetaka kuwa rafiki wa ulimwengu anajifanya adui wa Mungu. | Ye adulterers and adulteresses, know ye not that the friendship of the world is enmity with God? whosoever therefore will be a friend of the world is the enemy of God. |
| 5 | Msifikiri kwamba Maandiko Matakatifu yamesema maneno ya bure, yanaposema: "Roho ambaye Mungu amemweka ndani yetu ana wivu mkubwa." | Do ye think that the scripture saith in vain, The spirit that dwelleth in us lusteth to envy? |
| 6 | Lakini, neema tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: "Mungu huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu." | But he giveth more grace. Wherefore he saith, God resisteth the proud, but giveth grace unto the humble. |
| 7 | Basi, jiwekeni chini ya Mungu; mpingeni Ibilisi naye atawakimbieni. | Submit yourselves therefore to God. Resist the devil, and he will flee from you. |
| 8 | Mkaribieni Mungu, naye atakuja karibu nanyi. Osheni mikono yenu enyi wakosefu! Safisheni mioyo yenu enyi wanafiki! | Draw nigh to God, and he will draw nigh to you. Cleanse your hands, ye sinners; and purify your hearts, ye double minded. |
| 9 | Oneni huzuni, lieni na kuomboleza; kicheko chenu na kiwe kilio; na furaha yenu iwe huzuni kubwa. | Be afflicted, and mourn, and weep: let your laughter be turned to mourning, and your joy to heaviness. |
| 10 | Nyenyekeeni mbele ya Bwana, naye atawainueni. | Humble yourselves in the sight of the Lord, and he shall lift you up. |
| 11 | Ndugu, msilaumiane ninyi kwa ninyi. Anayemlaumu ndugu yake na kumhukumu, huyo huilaumu na kuihukumu Sheria. Kama ukiihukumu Sheria, basi, wewe huitii Sheria, bali waihukumu. | Speak not evil one of another, brethren. He that speaketh evil of his brother, and judgeth his brother, speaketh evil of the law, and judgeth the law: but if thou judge the law, thou art not a doer of the law, but a judge. |
| 12 | Mungu peke yake ndiye mwenye kuweka Sheria na kuhukumu. Ni yeye peke yake anayeweza kuokoa na kuangamiza. Basi, wewe ni nani hata umhukumu binadamu mwenzako? | There is one lawgiver, who is able to save and to destroy: who art thou that judgest another? |
| 13 | Basi, sasa sikilizeni ninyi mnaosema: "Leo au kesho tutakwenda katika mji fulani na kukaa huko mwaka mzima tukifanya biashara na kupata faida." | Go to now, ye that say, To day or to morrow we will go into such a city, and continue there a year, and buy and sell, and get gain: |
| 14 | Ninyi hamjui hata maisha yenu yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi tu na kutoweka tena. | Whereas ye know not what shall be on the morrow. For what is your life? It is even a vapour, that appeareth for a little time, and then vanisheth away. |
| 15 | Mngalipaswa kusema: "Bwana akitujalia tutaishi na tutafanya hiki au kile." | For that ye ought to say, If the Lord will, we shall live, and do this, or that. |
| 16 | Lakini sasa mwajivuna na kujigamba; majivuno ya namna hiyo ni mabaya. | But now ye rejoice in your boastings: all such rejoicing is evil. |
| 17 | Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi. | Therefore to him that knoweth to do good, and doeth it not, to him it is sin. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL