사도행전 14장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 사도행전 (Acts) · 28절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Kule Ikonio, mambo yalikuwa kama yalivyokuwa kule Antiokia; Paulo na Barnaba walikwenda katika sunagogi la Wayahudi wakaongea kwa uhodari hata Wayahudi wengi na Wagiriki wakawa waumini. | And it came to pass in Iconium, that they went both together into the synagogue of the Jews, and so spake, that a great multitude both of the Jews and also of the Greeks believed. |
| 2 | Lakini Wayahudi wengine waliokataa kuwa waumini walichochea na kutia chuki katika mioyo ya watu wa mataifa mengine ili wawapinge hao ndugu. | But the unbelieving Jews stirred up the Gentiles, and made their minds evil affected against the brethren. |
| 3 | Paulo na Barnaba waliendelea kukaa huko kwa muda mrefu. Waliongea kwa uhodari juu ya Bwana, naye Bwana akathibitisha ukweli wa ujumbe walioutoa juu ya neema yake, kwa kuwawezesha kutenda miujiza na maajabu. | Long time therefore abode they speaking boldly in the Lord, which gave testimony unto the word of his grace, and granted signs and wonders to be done by their hands. |
| 4 | Watu wa mji huo waligawanyika: wengine waliwaunga mkono Wayahudi, na wengine walikuwa upande wa mitume. | But the multitude of the city was divided: and part held with the Jews, and part with the apostles. |
| 5 | Mwishowe, baadhi ya watu wa mataifa mengine na Wayahudi, wakishirikiana na wakuu wao, waliazimu kuwatendea vibaya hao mitume na kuwapiga mawe. | And when there was an assault made both of the Gentiles, and also of the Jews with their rulers, to use them despitefully, and to stone them, |
| 6 | Mitume walipogundua jambo hilo, walikimbilia Lustra na Derbe, miji ya Lukaonia, na katika sehemu za jirani, | They were ware of it, and fled unto Lystra and Derbe, cities of Lycaonia, and unto the region that lieth round about: |
| 7 | wakawa wanahubiri Habari Njema huko. | And there they preached the gospel. |
| 8 | Kulikuwa na mtu mmoja huko Lustra ambaye alikuwa amelemaa miguu tangu kuzaliwa, na alikuwa hajapata kutembea kamwe. | And there sat a certain man at Lystra, impotent in his feet, being a cripple from his mother’s womb, who never had walked: |
| 9 | Mtu huyo alikuwa anamsikiliza Paulo alipokuwa anahubiri. Paulo alimtazama kwa makini, na alipoona kuwa alikuwa na imani ya kuweza kuponywa, | The same heard Paul speak: who stedfastly beholding him, and perceiving that he had faith to be healed, |
| 10 | akasema kwa sauti kubwa, "Simama wima kwa miguu yako!" Huyo mtu aliyelemaa akainuka ghafla, akaanza kutembea. | Said with a loud voice, Stand upright on thy feet. And he leaped and walked. |
| 11 | Umati wa watu walipoona alichofanya Paulo, ulianza kupiga kelele kwa lugha ya Kilukaonia: "Miungu imetujia katika sura za binadamu!" | And when the people saw what Paul had done, they lifted up their voices, saying in the speech of Lycaonia, The gods are come down to us in the likeness of men. |
| 12 | Barnaba akaitwa Zeu, na Paulo, kwa vile yeye ndiye aliyekuwa anaongea, akaitwa Herme. | And they called Barnabas, Jupiter; and Paul, Mercurius, because he was the chief speaker. |
| 13 | Naye kuhani wa hekalu la Zeu lililokuwa nje ya mji akaleta fahali na shada za maua mbele ya mlango mkuu wa mji, na pamoja na ule umati wa watu akataka kuwatambikia mitume. | Then the priest of Jupiter, which was before their city, brought oxen and garlands unto the gates, and would have done sacrifice with the people. |
| 14 | Barnaba na Paulo walipopata habari hiyo waliyararua mavazi yao na kukimbilia katika lile kundi la watu wakisema kwa sauti kubwa: | Which when the apostles, Barnabas and Paul, heard of, they rent their clothes, and ran in among the people, crying out, |
| 15 | "Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama ninyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo. | And saying, Sirs, why do ye these things? We also are men of like passions with you, and preach unto you that ye should turn from these vanities unto the living God, which made heaven, and earth, and the sea, and all things that are therein: |
| 16 | Zamani Mungu aliruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda. | Who in times past suffered all nations to walk in their own ways. |
| 17 | Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha." | Nevertheless he left not himself without witness, in that he did good, and gave us rain from heaven, and fruitful seasons, filling our hearts with food and gladness. |
| 18 | Ingawa walisema hivyo haikuwa rahisi kuwazuia wale watu wasiwatambikie. | And with these sayings scarce restrained they the people, that they had not done sacrifice unto them. |
| 19 | Lakini Wayahudi kadhaa walikuja kutoka Antiokia na Ikonio, wakawafanya watu wajiunge nao, wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji wakidhani amekwisha kufa. | And there came thither certain Jews from Antioch and Iconium, who persuaded the people, and, having stoned Paul, drew him out of the city, supposing he had been dead. |
| 20 | Lakini waumini walipokusanyika na kumzunguka, aliamka akarudi mjini. Kesho yake, yeye pamoja na Barnaba walikwenda Derbe. | Howbeit, as the disciples stood round about him, he rose up, and came into the city: and the next day he departed with Barnabas to Derbe. |
| 21 | Baada ya Paulo na Barnabas kuhubiri Habari Njema huko Derbe na kupata wafuasi wengi, walifunga safari kwenda Antiokia kwa kupitia Lustra na Ikonio. | And when they had preached the gospel to that city, and had taught many, they returned again to Lystra, and to Iconium, and Antioch, |
| 22 | Waliwaimarisha waumini wa miji hiyo na kuwatia moyo wabaki imara katika imani. Wakawaambia, "Ni lazima sisi sote tupitie katika taabu nyingi ili tuingie katika ufalme wa Mungu." | Confirming the souls of the disciples, and exhorting them to continue in the faith, and that we must through much tribulation enter into the kingdom of God. |
| 23 | Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada ya kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini. | And when they had ordained them elders in every church, and had prayed with fasting, they commended them to the Lord, on whom they believed. |
| 24 | Baada ya kupitia katika nchi ya Pisidia, walifika Pamfulia. | And after they had passed throughout Pisidia, they came to Pamphylia. |
| 25 | Baada ya kuhubiri ule ujumbe huko Perga, walikwenda Atalia. | And when they had preached the word in Perga, they went down into Attalia: |
| 26 | Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza. | And thence sailed to Antioch, from whence they had been recommended to the grace of God for the work which they fulfilled. |
| 27 | Walipofika huko Antiokia walifanya mkutano wa kanisa la mahali hapo, wakawapa taarifa juu ya mambo Mungu aliyofanya pamoja nao, na jinsi alivyowafungulia mlango watu wa mataifa mengine mlango wa kuingia katika imani. | And when they were come, and had gathered the church together, they rehearsed all that God had done with them, and how he had opened the door of faith unto the Gentiles. |
| 28 | Wakakaa pamoja na wale waumini kwa muda mrefu. | And there they abode long time with the disciples. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL