로그인

마태복음 23장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 39절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake, Then spake Jesus to the multitude, and to his disciples,
2 "Walimu wa Sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua Sheria ya Mose. Saying, The scribes and the Pharisees sit in Moses’ seat:
3 Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri. All therefore whatsoever they bid you observe, that observe and do; but do not ye after their works: for they say, and do not.
4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba. For they bind heavy burdens and grievous to be borne, and lay them on men’s shoulders; but they themselves will not move them with one of their fingers.
5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya Sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao. But all their works they do for to be seen of men: they make broad their phylacteries, and enlarge the borders of their garments,
6 Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika masunagogi. And love the uppermost rooms at feasts, and the chief seats in the synagogues,
7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: Mwalimu. And greetings in the markets, and to be called of men, Rabbi, Rabbi.
8 Lakini ninyi msiitwe kamwe Mwalimu, maana mwalimu wenu ni mmoja tu, nanyi nyote ni ndugu. But be not ye called Rabbi: for one is your Master, even Christ; and all ye are brethren.
9 Wala msimwite mtu yeyote Baba hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu aliye mbinguni. And call no man your father upon the earth: for one is your Father, which is in heaven.
10 Wala msiitwe Viongozi, maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo. Neither be ye called masters: for one is your Master, even Christ.
11 Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu. But he that is greatest among you shall be your servant.
12 Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa. And whosoever shall exalt himself shall be abased; and he that shall humble himself shall be exalted.
13 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Ufalme wa mbinguni mbele ya macho ya watu. Ninyi wenyewe hamwingii ndani, wala hamwaruhusu wanaotaka kuingia waingie. But woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye shut up the kingdom of heaven against men: for ye neither go in yourselves, neither suffer ye them that are entering to go in.
14 Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnawanyonya wajane na kujisingizia kuwa watu wema kwa kusali sala ndefu. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali. Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye devour widows’ houses, and for a pretence make long prayer: therefore ye shall receive the greater damnation.
15 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate dini yenu. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika moto wa Jehanamu kuliko ninyi wenyewe. Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye compass sea and land to make one proselyte, and when he is made, ye make him twofold more the child of hell than yourselves.
16 "Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa dhahabu ya Hekalu, kiapo hicho kinamshika. Woe unto you, ye blind guides, which say, Whosoever shall swear by the temple, it is nothing; but whosoever shall swear by the gold of the temple, he is a debtor!
17 Enyi vipofu wapumbavu! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu au Hekalu linalofanya hiyo dhahabu kuwa takatifu? Ye fools and blind: for whether is greater, the gold, or the temple that sanctifieth the gold?
18 Tena mwasema ati mtu akiapa kwa madhabahu si kitu; lakini akiapa kwa zawadi iliyowekwa juu ya madhabahu, kiapo hicho humshika. And, Whosoever shall swear by the altar, it is nothing; but whosoever sweareth by the gift that is upon it, he is guilty.
19 Enyi vipofu! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, au madhabahu ambayo hufanya hiyo zawadi kuwa takatifu? Ye fools and blind: for whether is greater, the gift, or the altar that sanctifieth the gift?
20 Anayeapa kwa madhabahu ameapa kwa hiyo madhabahu, na kwa chochote kilichowekwa juu yake. Whoso therefore shall swear by the altar, sweareth by it, and by all things thereon.
21 Na anayeapa kwa Hekalu ameapa kwa hilo Hekalu na pia kwa yule akaaye ndani yake. And whoso shall swear by the temple, sweareth by it, and by him that dwelleth therein.
22 Na anayeapa kwa mbingu ameapa kwa kiti cha enzi cha Mungu, na kwa huyo aketiye juu yake. And he that shall swear by heaven, sweareth by the throne of God, and by him that sitteth thereon.
23 Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu zaka, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya Sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine. Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye pay tithe of mint and anise and cummin, and have omitted the weightier matters of the law, judgment, mercy, and faith: these ought ye to have done, and not to leave the other undone.
24 Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia! Ye blind guides, which strain at a gnat, and swallow a camel.
25 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo. Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye make clean the outside of the cup and of the platter, but within they are full of extortion and excess.
26 Mfarisayo kipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia. Thou blind Pharisee, cleanse first that which is within the cup and platter, that the outside of them may be clean also.
27 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu. Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for ye are like unto whited sepulchres, which indeed appear beautiful outward, but are within full of dead men’s bones, and of all uncleanness.
28 Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu. Even so ye also outwardly appear righteous unto men, but within ye are full of hypocrisy and iniquity.
29 "Ole wenu walimu wa Sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya watu wema. Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! because ye build the tombs of the prophets, and garnish the sepulchres of the righteous,
30 Mwasema: Kama sisi tungaliishi nyakati za wazee wetu hatungalishirikiana nao katika mauaji ya manabii! And say, If we had been in the days of our fathers, we would not have been partakers with them in the blood of the prophets.
31 Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua manabii. Wherefore ye be witnesses unto yourselves, that ye are the children of them which killed the prophets.
32 Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu waliyoianza! Fill ye up then the measure of your fathers.
33 Enyi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu? Ye serpents, ye generation of vipers, how can ye escape the damnation of hell?
34 Ndiyo maana mimi ninawapelekea ninyi manabii, watu wenye hekima na walimu; mtawaua na kuwasulubisha baadhi yao, na wengine mtawapiga viboko katika masunagogi yenu na kuwasaka katika kila mji. Wherefore, behold, I send unto you prophets, and wise men, and scribes: and some of them ye shall kill and crucify; and some of them shall ye scourge in your synagogues, and persecute them from city to city:
35 Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kuuawa kwa Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Zakariya, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua Hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu. That upon you may come all the righteous blood shed upon the earth, from the blood of righteous Abel unto the blood of Zacharias son of Barachias, whom ye slew between the temple and the altar.
36 Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya mambo haya. Verily I say unto you, All these things shall come upon this generation.
37 "Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka. O Jerusalem, Jerusalem, thou that killest the prophets, and stonest them which are sent unto thee, how often would I have gathered thy children together, even as a hen gathereth her chickens under her wings, and ye would not!
38 Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame. Behold, your house is left unto you desolate.
39 Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana." For I say unto you, Ye shall not see me henceforth, till ye shall say, Blessed is he that cometh in the name of the Lord.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL