마태복음 17장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마태복음 (Matthew) · 27절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. | And after six days Jesus taketh Peter, James, and John his brother, and bringeth them up into an high mountain apart, |
| 2 | Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru. | And was transfigured before them: and his face did shine as the sun, and his raiment was white as the light. |
| 3 | Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye. | And, behold, there appeared unto them Moses and Elias talking with him. |
| 4 | Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya." | Then answered Peter, and said unto Jesus, Lord, it is good for us to be here: if thou wilt, let us make here three tabernacles; one for thee, and one for Moses, and one for Elias. |
| 5 | Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni." | While he yet spake, behold, a bright cloud overshadowed them: and behold a voice out of the cloud, which said, This is my beloved Son, in whom I am well pleased; hear ye him. |
| 6 | Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana. | And when the disciples heard it, they fell on their face, and were sore afraid. |
| 7 | Yesu akawaendea, akawagusa, akasema, "Simameni, msiogope!" | And Jesus came and touched them, and said, Arise, and be not afraid. |
| 8 | Walipoinua macho yao hawakumwona mtu, ila Yesu peke yake. | And when they had lifted up their eyes, they saw no man, save Jesus only. |
| 9 | Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: "Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu." | And as they came down from the mountain, Jesus charged them, saying, Tell the vision to no man, until the Son of man be risen again from the dead. |
| 10 | Kisha wanafunzi wakamwuliza, "Mbona walimu wa Sheria wanasema ati ni lazima kwanza Eliya aje?" | And his disciples asked him, saying, Why then say the scribes that Elias must first come? |
| 11 | Yesu akawajibu, "Kweli, Eliya atakuja kutayarisha mambo yote. | And Jesus answered and said unto them, Elias truly shall first come, and restore all things. |
| 12 | Lakini nawaambieni, Eliya amekwisha kuja nao hawakumtambua, bali walimtendea jinsi walivyotaka. Mwana wa Mtu atateswa vivyo hivyo mikononi mwao." | But I say unto you, That Elias is come already, and they knew him not, but have done unto him whatsoever they listed. Likewise shall also the Son of man suffer of them. |
| 13 | Hapo hao wanafunzi wakafahamu kwamba alikuwa akiwaambia juu ya Yohane mbatizaji. | Then the disciples understood that he spake unto them of John the Baptist. |
| 14 | Walipojiunga tena na ule umati wa watu, mtu mmoja alimwendea Yesu, akampigia magoti, | And when they were come to the multitude, there came to him a certain man, kneeling down to him, and saying, |
| 15 | akasema, "Mheshimiwa, mwonee huruma mwanangu kwa kuwa ana kifafa, tena anateseka sana; mara nyingi yeye huanguka motoni na majini. | Lord, have mercy on my son: for he is lunatick, and sore vexed: for ofttimes he falleth into the fire, and oft into the water. |
| 16 | Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya." | And I brought him to thy disciples, and they could not cure him. |
| 17 | Yesu akajibu, "Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia ninyi mpaka lini? Mleteni hapa huyo mtoto." | Then Jesus answered and said, O faithless and perverse generation, how long shall I be with you? how long shall I suffer you? bring him hither to me. |
| 18 | Basi, Yesu akamkemea huyo pepo, naye akamtoka, na yule mtoto akapona wakati huohuo. | And Jesus rebuked the devil; and he departed out of him: and the child was cured from that very hour. |
| 19 | Kisha wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha, wakamwuliza, "Kwa nini sisi hatukuweza kumtoa yule pepo?" | Then came the disciples to Jesus apart, and said, Why could not we cast him out? |
| 20 | Yesu akawajibu, "Kwa sababu ya imani yenu haba. Nawaambieni kweli, kama tu mkiwa na imani, hata iwe ndogo kama mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu: Toka hapa uende pale, nao utakwenda. Hakuna chochote ambacho hakingewezekana kwenu." | And Jesus said unto them, Because of your unbelief: for verily I say unto you, If ye have faith as a grain of mustard seed, ye shall say unto this mountain, Remove hence to yonder place; and it shall remove; and nothing shall be impossible unto you. |
| 21 | "Pepo wa namna hii hawezi kuondolewa ila kwa sala na kufunga." | Howbeit this kind goeth not out but by prayer and fasting. |
| 22 | Walipokuwa pamoja huko Galilaya, Yesu aliwaambia, "Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa watu. | And while they abode in Galilee, Jesus said unto them, The Son of man shall be betrayed into the hands of men: |
| 23 | Watamuua, lakini siku ya tatu atafufuliwa." Wanafunzi wakahuzunika mno. | And they shall kill him, and the third day he shall be raised again. And they were exceeding sorry. |
| 24 | Walipofika Kafarnaumu watu wenye kukusanya fedha ya zaka ya Hekalu walimwendea Petro, wakamwuliza, "Je, mwalimu wenu hulipa fedha ya zaka?" | And when they were come to Capernaum, they that received tribute money came to Peter, and said, Doth not your master pay tribute? |
| 25 | Petro akajibu, "Naam, hulipa." Basi, Petro alipoingia ndani ya nyumba, kabla hata hajasema neno, Yesu akamwuliza, "Simoni, wewe unaonaje? Wafalme wa dunia hukusanya ushuru au kodi kutoka kwa kina nani? Kutoka kwa wananchi ama kutoka kwa wageni?" | He saith, Yes. And when he was come into the house, Jesus prevented him, saying, What thinkest thou, Simon? of whom do the kings of the earth take custom or tribute? of their own children, or of strangers? |
| 26 | Petro akajibu, "Kutoka kwa wageni." Yesu akamwambia, "Haya basi, wananchi hawahusiki. | Peter saith unto him, Of strangers. Jesus saith unto him, Then are the children free. |
| 27 | Lakini kusudi tusiwakwaze, nenda ziwani ukatupe ndoana; chukua samaki wa kwanza atakayenaswa, fungua kinywa chake, na ndani utakuta fedha taslimu ya zaka. Ichukue ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako." | Notwithstanding, lest we should offend them, go thou to the sea, and cast an hook, and take up the fish that first cometh up; and when thou hast opened his mouth, thou shalt find a piece of money: that take, and give unto them for me and thee. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL