마가복음 10장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 마가복음 (Mark) · 52절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Yesu alitoka hapo akaenda mkoani Yudea na hata ng'ambo ya mto Yordani. Umati wa watu ukamwendea tena, naye akawafundisha tena kama ilivyokuwa desturi yake. | And he arose from thence, and cometh into the coasts of Judea by the farther side of Jordan: and the people resort unto him again; and, as he was wont, he taught them again. |
| 2 | Basi, Mafarisayo wakamwendea, na kwa kumjaribu wakamwuliza, "Je, ni halali mtu kumpa talaka mkewe?" | And the Pharisees came to him, and asked him, Is it lawful for a man to put away his wife? tempting him. |
| 3 | Yesu akawajibu, "Mose aliwapa maagizo gani?" | And he answered and said unto them, What did Moses command you? |
| 4 | Nao wakasema, "Mose aliagiza mume kumpatia mkewe hati ya talaka na kumwacha." | And they said, Moses suffered to write a bill of divorcement, and to put her away. |
| 5 | Yesu akawaambia, "Mose aliwaandikia amri hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. | And Jesus answered and said unto them, For the hardness of your heart he wrote you this precept. |
| 6 | Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke. | But from the beginning of the creation God made them male and female. |
| 7 | Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, | For this cause shall a man leave his father and mother, and cleave to his wife; |
| 8 | nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. | And they twain shall be one flesh: so then they are no more twain, but one flesh. |
| 9 | Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe." | What therefore God hath joined together, let not man put asunder. |
| 10 | Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo. | And in the house his disciples asked him again of the same matter. |
| 11 | Naye akawaambia, "Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe. | And he saith unto them, Whosoever shall put away his wife, and marry another, committeth adultery against her. |
| 12 | Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini." | And if a woman shall put away her husband, and be married to another, she committeth adultery. |
| 13 | Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea. | And they brought young children to him, that he should touch them: and his disciples rebuked those that brought them. |
| 14 | Yesu alipoona hivyo, alikasirika akawaambia, "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu walio kama watoto hawa. | But when Jesus saw it, he was much displeased, and said unto them, Suffer the little children to come unto me, and forbid them not: for of such is the kingdom of God. |
| 15 | Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hataingia katika Ufalme huo." | Verily I say unto you, Whosoever shall not receive the kingdom of God as a little child, he shall not enter therein. |
| 16 | Kisha akawapokea watoto hao, akawawekea mikono, akawabariki. | And he took them up in his arms, put his hands upon them, and blessed them. |
| 17 | Yesu alipoanza tena safari yake, mtu mmoja alimjia mbio, akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, "Mwalimu mwema, nifanyeje ili niupate uzima wa milele?" | And when he was gone forth into the way, there came one running, and kneeled to him, and asked him, Good Master, what shall I do that I may inherit eternal life? |
| 18 | Yesu akamjibu, "Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. | And Jesus said unto him, Why callest thou me good? there is none good but one, that is, God. |
| 19 | Unazijua amri: Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Usidanganye; Waheshimu baba na mama yako." | Thou knowest the commandments, Do not commit adultery, Do not kill, Do not steal, Do not bear false witness, Defraud not, Honour thy father and mother. |
| 20 | Naye akamjibu, "Mwalimu, hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu." | And he answered and said unto him, Master, all these have I observed from my youth. |
| 21 | Yesu akamtazama, akampenda, akamwambia, "Umepungukiwa na kitu kimoja: nenda ukauze vitu ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate." | Then Jesus beholding him loved him, and said unto him, One thing thou lackest: go thy way, sell whatsoever thou hast, and give to the poor, and thou shalt have treasure in heaven: and come, take up the cross, and follow me. |
| 22 | Aliposikia hayo, alisikitika, akaenda zake akiwa na huzuni, kwa maana alikuwa na mali nyingi. | And he was sad at that saying, and went away grieved: for he had great possessions. |
| 23 | Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, "Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!" | And Jesus looked round about, and saith unto his disciples, How hardly shall they that have riches enter into the kingdom of God! |
| 24 | Wanafunzi walishangazwa na maneno yake. Yesu akawaambia tena, "Watoto wangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu! | And the disciples were astonished at his words. But Jesus answereth again, and saith unto them, Children, how hard is it for them that trust in riches to enter into the kingdom of God! |
| 25 | Ni rahisi zaidi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu." | It is easier for a camel to go through the eye of a needle, than for a rich man to enter into the kingdom of God. |
| 26 | Wanafunzi wake wakashangaa sana wakaulizana, "Ni nani basi, atakayeweza kuokoka?" | And they were astonished out of measure, saying among themselves, Who then can be saved? |
| 27 | Yesu akawatazama, akawaambia, "Kwa binadamu haiwezekani, lakini kwa Mungu si hivyo, maana kwa Mungu mambo yote huwezekana." | And Jesus looking upon them saith, With men it is impossible, but not with God: for with God all things are possible. |
| 28 | Petro akamwambia, "Na sisi je? Tumeacha yote, tukakufuata!" | Then Peter began to say unto him, Lo, we have left all, and have followed thee. |
| 29 | Yesu akasema, "Kweli nawaambieni, kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, | And Jesus answered and said, Verily I say unto you, There is no man that hath left house, or brethren, or sisters, or father, or mother, or wife, or children, or lands, for my sake, and the gospel’s, |
| 30 | atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uzima wa milele. | But he shall receive an hundredfold now in this time, houses, and brethren, and sisters, and mothers, and children, and lands, with persecutions; and in the world to come eternal life. |
| 31 | Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza." | But many that are first shall be last; and the last first. |
| 32 | Basi, walikuwa njiani kwenda Yerusalemu, na Yesu alikuwa anawatangulia. Wanafunzi wake walijawa na hofu, na watu waliofuata waliogopa. Yesu akawachukua tena kando wale kumi na wawili, akaanza kuwaambia yale yatakayompata: | And they were in the way going up to Jerusalem; and Jesus went before them: and they were amazed; and as they followed, they were afraid. And he took again the twelve, and began to tell them what things should happen unto him, |
| 33 | "Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na walimu wa Sheria, nao watamhukumu auawe na kumkabidhi kwa watu wa mataifa. | Saying, Behold, we go up to Jerusalem; and the Son of man shall be delivered unto the chief priests, and unto the scribes; and they shall condemn him to death, and shall deliver him to the Gentiles: |
| 34 | Nao watamdhihaki; watamtemea mate, watampiga mijeledi na kumwua. Na baada ya siku tatu atafufuka." | And they shall mock him, and shall scourge him, and shall spit upon him, and shall kill him: and the third day he shall rise again. |
| 35 | Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, "Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba." | And James and John, the sons of Zebedee, come unto him, saying, Master, we would that thou shouldest do for us whatsoever we shall desire. |
| 36 | Yesu akawauliza, "Mnataka niwafanyie nini?" | And he said unto them, What would ye that I should do for you? |
| 37 | Wakamjibu, "Uturuhusu tuketi mmoja upande wako wa kulia na mwingine upande wako wa kushoto katika utukufu wa Ufalme wako." | They said unto him, Grant unto us that we may sit, one on thy right hand, and the other on thy left hand, in thy glory. |
| 38 | Yesu akawaambia, "Hamjui mnachoomba! Je, mnaweza kunywa kikombe nitakachokunywa, au kubatizwa kama nitakavyobatizwa?" | But Jesus said unto them, Ye know not what ye ask: can ye drink of the cup that I drink of? and be baptized with the baptism that I am baptized with? |
| 39 | Wakamjibu, "Tunaweza." Yesu akawaambia, "Kikombe nitakachokunywa mtakinywa kweli, na mtabatizwa kama nitakavyobatizwa. | And they said unto him, We can. And Jesus said unto them, Ye shall indeed drink of the cup that I drink of; and with the baptism that I am baptized withal shall ye be baptized: |
| 40 | Lakini ni nani atakayeketi kulia au kushoto kwangu si wajibu wangu kupanga, bali nafasi hizo watapewa wale waliotayarishiwa." | But to sit on my right hand and on my left hand is not mine to give; but it shall be given to them for whom it is prepared. |
| 41 | Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia hayo, walianza kuchukizwa na Yakobo na Yohane. | And when the ten heard it, they began to be much displeased with James and John. |
| 42 | Yesu akawaita, akawaambia, "Mnajua kwamba wale wanaofikiriwa kuwa watawala wa mataifa huwatawala watu wao kwa mabavu, na wakuu hao huwamiliki watu wao. | But Jesus called them to him, and saith unto them, Ye know that they which are accounted to rule over the Gentiles exercise lordship over them; and their great ones exercise authority upon them. |
| 43 | Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu, sharti awe mtumishi wenu. | But so shall it not be among you: but whosoever will be great among you, shall be your minister: |
| 44 | Anayetaka kuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa wote. | And whosoever of you will be the chiefest, shall be servant of all. |
| 45 | Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila alikuja kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi." | For even the Son of man came not to be ministered unto, but to minister, and to give his life a ransom for many. |
| 46 | Basi, wakafika Yeriko, naye Yesu alipokuwa anatoka katika mji huo akiwa na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mwombaji aitwaye Bartimayo mwana wa Timayo alikuwa ameketi kando ya barabara. | And they came to Jericho: and as he went out of Jericho with his disciples and a great number of people, blind Bartimeus, the son of Timeus, sat by the highway side begging. |
| 47 | Aliposikia kwamba ni Yesu wa Nazareti aliyekuwa anapita mahali hapo, alianza kupaaza sauti, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!" | And when he heard that it was Jesus of Nazareth, he began to cry out, and say, Jesus, thou Son of David, have mercy on me. |
| 48 | Watu wengi walimkemea ili anyamaze, lakini yeye akazidi kupaaza sauti, "Mwana wa Daudi, nihurumie!" | And many charged him that he should hold his peace: but he cried the more a great deal, Thou Son of David, have mercy on me. |
| 49 | Yesu alisimama, akasema, "Mwiteni." Basi, wakamwita huyo kipofu, wakamwambia, "Jipe moyo! Simama, anakuita." | And Jesus stood still, and commanded him to be called. And they call the blind man, saying unto him, Be of good comfort, rise; he calleth thee. |
| 50 | Naye akatupilia mbali vazi lake, akaruka juu, akamwendea Yesu. | And he, casting away his garment, rose, and came to Jesus. |
| 51 | Yesu akamwuliza, "Unataka nikufanyie nini?" Huyo kipofu akamwambia, "Mwalimu, naomba nipate kuona." | And Jesus answered and said unto him, What wilt thou that I should do unto thee? The blind man said unto him, Lord, that I might receive my sight. |
| 52 | Yesu akamwambia, "Nenda, imani yako imekuponya." Mara huyo kipofu akaweza kuona, akamfuata Yesu njiani. | And Jesus said unto him, Go thy way; thy faith hath made thee whole. And immediately he received his sight, and followed Jesus in the way. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL