디모데전서 2장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 디모데전서 (1 Timothy) · 15절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Kwanza kabisa, basi naomba dua, sala, maombi na sala za shukrani zitolewe kwa Mungu kwa ajili ya watu wote, | I exhort therefore, that, first of all, supplications, prayers, intercessions, and giving of thanks, be made for all men; |
| 2 | kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani pamoja na uchaji wa Mungu na mwenendo mwema. | For kings, and for all that are in authority; that we may lead a quiet and peaceable life in all godliness and honesty. |
| 3 | Jambo hili ni jema na lampendeza Mungu Mwokozi wetu, | For this is good and acceptable in the sight of God our Saviour; |
| 4 | ambaye anataka watu wote waokolewe na wapate kuujua ukweli. | Who will have all men to be saved, and to come unto the knowledge of the truth. |
| 5 | Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu, | For there is one God, and one mediator between God and men, the man Christ Jesus; |
| 6 | ambaye alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote. Huo ulikuwa uthibitisho, wakati ufaao ulipowadia. | Who gave himself a ransom for all, to be testified in due time. |
| 7 | Kwa sababu hiyo mimi nilitumwa niwe mtume na mwalimu wa watu wa mataifa, niutangaze ujumbe wa imani na ukweli. Nasema ukweli; sisemi uongo! | Whereunto I am ordained a preacher, and an apostle, (I speak the truth in Christ, and lie not;) a teacher of the Gentiles in faith and verity. |
| 8 | Basi, popote mnapokutana kufanya ibada nataka wanaume wasali, watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua mikono yao wakisali bila hasira wala ubishi. | I will therefore that men pray every where, lifting up holy hands, without wrath and doubting. |
| 9 | Hali kadhalika, nawataka wanawake wawe wanyofu na wenye busara kuhusu mavazi yao; wavae sawasawa na si kwa urembo wa mitindo ya kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, | In like manner also, that women adorn themselves in modest apparel, with shamefacedness and sobriety; not with broided hair, or gold, or pearls, or costly array; |
| 10 | bali kwa matendo mema kama iwapasavyo wanawake wamchao Mungu. | But (which becometh women professing godliness) with good works. |
| 11 | Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. | Let the woman learn in silence with all subjection. |
| 12 | Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya. | But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in silence. |
| 13 | Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa. | For Adam was first formed, then Eve. |
| 14 | Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu. | And Adam was not deceived, but the woman being deceived was in the transgression. |
| 15 | Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu. | Notwithstanding she shall be saved in childbearing, if they continue in faith and charity and holiness with sobriety. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL