로그인

데살로니가후서 3장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 데살로니가후서 (2 Thessalonians) · 18절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu. Finally, brethren, pray for us, that the word of the Lord may have free course, and be glorified, even as it is with you:
2 Ombeni pia ili Mungu atuokoe na watu wapotovu na waovu, maana si wote wanaoamini ujumbe huu. And that we may be delivered from unreasonable and wicked men: for all men have not faith.
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Yeye atawaimarisheni na kuwalinda salama na yule Mwovu. But the Lord is faithful, who shall stablish you, and keep you from evil.
4 Naye Bwana anatupatia tumaini kubwa juu yenu, na hatuna shaka kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaambieni. And we have confidence in the Lord touching you, that ye both do and will do the things which we command you.
5 Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika uvumilivu tunaopewa na Kristo. And the Lord direct your hearts into the love of God, and into the patient waiting for Christ.
6 Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa. Now we command you, brethren, in the name of our Lord Jesus Christ, that ye withdraw yourselves from every brother that walketh disorderly, and not after the tradition which he received of us.
7 Ninyi wenyewe mnajua kwamba mnapaswa kufuata mfano wetu. Sisi tulipokuwa nanyi hatukuwa wavivu; For yourselves know how ye ought to follow us: for we behaved not ourselves disorderly among you;
8 hatukula chakula kwa mtu yeyote bila ya kumlipa. Tulifanya kazi kwa bidii na taabu mchana na usiku ili tusiwe mzigo kwa mtu yeyote kati yenu. Neither did we eat any man’s bread for nought; but wrought with labour and travail night and day, that we might not be chargeable to any of you:
9 Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu tunataka kuwapeni mfano. Not because we have not power, but to make ourselves an ensample unto you to follow us.
10 Tulipokuwa pamoja nanyi tulikuwa tukiwaambieni, "Mtu asiyefanya kazi, asile." For even when we were with you, this we commanded you, that if any would not work, neither should he eat.
11 Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya watu wengine. For we hear that there are some which walk among you disorderly, working not at all, but are busybodies.
12 Kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo tunawaamuru na kuwaonya watu hao wawe na nidhamu na kufanya kazi ili wajipatie maslahi yao wenyewe. Now them that are such we command and exhort by our Lord Jesus Christ, that with quietness they work, and eat their own bread.
13 Lakini ninyi ndugu, msichoke kutenda mema. But ye, brethren, be not weary in well doing.
14 Huenda kwamba huko kuna mtu ambaye hatautii huu ujumbe tunaowapelekeeni katika barua hii. Ikiwa hivyo, basi, mfichueni mtu huyo na msiwe na uhusiano wowote naye kusudi aone aibu. And if any man obey not our word by this epistle, note that man, and have no company with him, that he may be ashamed.
15 Lakini msimtendee mtu huyo kama adui, bali mwonyeni kama ndugu. Yet count him not as an enemy, but admonish him as a brother.
16 Bwana mwenyewe ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote. Now the Lord of peace himself give you peace always by all means. The Lord be with you all.
17 Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika. The salutation of Paul with mine own hand, which is the token in every epistle: so I write.
18 Tunawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. The grace of our Lord Jesus Christ be with you all. Amen. The second epistle to the Thessalonians was written from Athens.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL