데살로니가전서 5장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 데살로니가전서 (1 Thessalonians) · 28절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati na majira yatakapotukia mambo haya. | But of the times and the seasons, brethren, ye have no need that I write unto you. |
| 2 | Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. | For yourselves know perfectly that the day of the Lord so cometh as a thief in the night. |
| 3 | Watu watakapokuwa wanasema: "Kila kitu ni shwari na salama" ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. | For when they shall say, Peace and safety; then sudden destruction cometh upon them, as travail upon a woman with child; and they shall not escape. |
| 4 | Lakini ninyi ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. | But ye, brethren, are not in darkness, that that day should overtake you as a thief. |
| 5 | Ninyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza. | Ye are all the children of light, and the children of the day: we are not of the night, nor of darkness. |
| 6 | Basi, tusilale usingizi kama wengine; tunapaswa kukesha na kuwa na kiasi. | Therefore let us not sleep, as do others; but let us watch and be sober. |
| 7 | Wanaolala hulala usiku, na walevi hulewa usiku. | For they that sleep sleep in the night; and they that be drunken are drunken in the night. |
| 8 | Lakini sisi ni watu wa mchana na tunapaswa kuwa na kiasi. Tunapaswa kuvaa imani na upendo kama vazi la kujikinga kifuani, na tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. | But let us, who are of the day, be sober, putting on the breastplate of faith and love; and for an helmet, the hope of salvation. |
| 9 | Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadhabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, | For God hath not appointed us to wrath, but to obtain salvation by our Lord Jesus Christ, |
| 10 | ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tu hai au tumekufa. | Who died for us, that, whether we wake or sleep, we should live together with him. |
| 11 | Kwa hiyo farijianeni na kusaidiana ninyi kwa ninyi kama mnavyofanya sasa. | Wherefore comfort yourselves together, and edify one another, even as also ye do. |
| 12 | Ndugu, tunawaombeni muwastahi wale wanaofanya kazi kati yenu, wale wanaowaongoza na kuwafundisheni kuhusu maisha ya Kikristo. | And we beseech you, brethren, to know them which labour among you, and are over you in the Lord, and admonish you; |
| 13 | Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa sababu ya kazi wanayofanya. Muwe na amani kati yenu. | And to esteem them very highly in love for their work’s sake. And be at peace among yourselves. |
| 14 | Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote. | Now we exhort you, brethren, warn them that are unruly, comfort the feebleminded, support the weak, be patient toward all men. |
| 15 | Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote. | See that none render evil for evil unto any man; but ever follow that which is good, both among yourselves, and to all men. |
| 16 | Furahini daima, | Rejoice evermore. |
| 17 | salini kila wakati | Pray without ceasing. |
| 18 | na muwe na shukrani katika kila hali. Hayo ndiyo anayotaka Mungu kwenu katika kuungana kwenu na Kristo Yesu. | In every thing give thanks: for this is the will of God in Christ Jesus concerning you. |
| 19 | Msimpinge Roho Mtakatifu; | Quench not the Spirit. |
| 20 | msidharau unabii. | Despise not prophesyings. |
| 21 | Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema, | Prove all things; hold fast that which is good. |
| 22 | na epukeni kila aina ya uovu. | Abstain from all appearance of evil. |
| 23 | Mungu anayetupatia amani awafanye ninyi watakatifu kwa kila namna na kuzilinda nafsi zenu--roho, mioyo na miili yenu--mbali na hatia yoyote wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. | And the very God of peace sanctify you wholly; and I pray God your whole spirit and soul and body be preserved blameless unto the coming of our Lord Jesus Christ. |
| 24 | Yeye anayewaita ninyi atafanya hivyo kwani ni mwaminifu. | Faithful is he that calleth you, who also will do it. |
| 25 | Ndugu, tuombeeni na sisi pia. | Brethren, pray for us. |
| 26 | Wasalimuni ndugu wote kwa ishara ya upendo. | Greet all the brethren with an holy kiss. |
| 27 | Nawahimizeni kwa jina la Bwana muwasomee ndugu zetu wote barua hii. | I charge you by the Lord that this epistle be read unto all the holy brethren. |
| 28 | Tunawatakieni neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. | The grace of our Lord Jesus Christ be with you. Amen. The first epistle unto the Thessalonians was written from Athens. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL