로그인

누가복음 4장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 44절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani. And Jesus being full of the Holy Ghost returned from Jordan, and was led by the Spirit into the wilderness,
2 Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa. Being forty days tempted of the devil. And in those days he did eat nothing: and when they were ended, he afterward hungered.
3 Ndipo Ibilisi akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate." And the devil said unto him, If thou be the Son of God, command this stone that it be made bread.
4 Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Mtu haishi kwa mkate tu." And Jesus answered him, saying, It is written, That man shall not live by bread alone, but by every word of God.
5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia, And the devil, taking him up into an high mountain, shewed unto him all the kingdoms of the world in a moment of time.
6 "Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza. And the devil said unto him, All this power will I give thee, and the glory of them: for that is delivered unto me; and to whomsoever I will I give it.
7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu." If thou therefore wilt worship me, all shall be thine.
8 Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake." And Jesus answered and said unto him, Get thee behind me, Satan: for it is written, Thou shalt worship the Lord thy God, and him only shalt thou serve.
9 Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, kwenye mnara wa Hekalu, akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, And he brought him to Jerusalem, and set him on a pinnacle of the temple, and said unto him, If thou be the Son of God, cast thyself down from hence:
10 kwa maana imeandikwa: Atawaamuru malaika wake wakulinde, For it is written, He shall give his angels charge over thee, to keep thee:
11 na tena, Watakuchukua mikononi mwao usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe." And in their hands they shall bear thee up, lest at any time thou dash thy foot against a stone.
12 Lakini Yesu akamjibu, "Imeandikwa: Usimjaribu Bwana Mungu wako." And Jesus answering said unto him, It is said, Thou shalt not tempt the Lord thy God.
13 Ibilisi alipokwishamjaribu kwa kila njia, akamwacha kwa muda. And when the devil had ended all the temptation, he departed from him for a season.
14 Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani. And Jesus returned in the power of the Spirit into Galilee: and there went out a fame of him through all the region round about.
15 Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote. And he taught in their synagogues, being glorified of all.
16 Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti. And he came to Nazareth, where he had been brought up: and, as his custom was, he went into the synagogue on the sabbath day, and stood up for to read.
17 Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa: And there was delivered unto him the book of the prophet Esaias. And when he had opened the book, he found the place where it was written,
18 "Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa, The Spirit of the Lord is upon me, because he hath anointed me to preach the gospel to the poor; he hath sent me to heal the brokenhearted, to preach deliverance to the captives, and recovering of sight to the blind, to set at liberty them that are bruised,
19 na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana." To preach the acceptable year of the Lord.
20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho. And he closed the book, and he gave it again to the minister, and sat down. And the eyes of all them that were in the synagogue were fastened on him.
21 Naye akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo." And he began to say unto them, This day is this scripture fulfilled in your ears.
22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?" And all bare him witness, and wondered at the gracious words which proceeded out of his mouth. And they said, Is not this Joseph’s son?
23 Naye akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: Mganga jiponye mwenyewe, na pia mtasema: Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako." And he said unto them, Ye will surely say unto me this proverb, Physician, heal thyself: whatsoever we have heard done in Capernaum, do also here in thy country.
24 Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake. And he said, Verily I say unto you, No prophet is accepted in his own country.
25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote. But I tell you of a truth, many widows were in Israel in the days of Elias, when the heaven was shut up three years and six months, when great famine was throughout all the land;
26 Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni. But unto none of them was Elias sent, save unto Sarepta, a city of Sidon, unto a woman that was a widow.
27 Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyeji wa Siria." And many lepers were in Israel in the time of Eliseus the prophet; and none of them was cleansed, saving Naaman the Syrian.
28 Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana. And all they in the synagogue, when they heard these things, were filled with wrath,
29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini. And rose up, and thrust him out of the city, and led him unto the brow of the hill whereon their city was built, that they might cast him down headlong.
30 Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake. But he passing through the midst of them went his way,
31 Kisha Yesu akashuka mpaka Kafarnaumu katika mkoa wa Galilaya, akawa anawafundisha watu siku ya Sabato. And came down to Capernaum, a city of Galilee, and taught them on the sabbath days.
32 Wakastaajabia uwezo aliokuwa nao katika kufundisha. And they were astonished at his doctrine: for his word was with power.
33 Na katika lile sunagogi kulikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na roho ya pepo mchafu; akapiga ukelele wa kuziba masikio: And in the synagogue there was a man, which had a spirit of an unclean devil, and cried out with a loud voice,
34 "We! Yesu wa Nazareti! Kwa nini unatuingilia? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakufahamu wewe ni nani. Wewe ni mjumbe Mtakatifu wa Mungu!" Saying, Let us alone; what have we to do with thee, thou Jesus of Nazareth? art thou come to destroy us? I know thee who thou art; the Holy One of God.
35 Lakini Yesu akamkemea huyo pepo akisema: "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Basi, huyo pepo baada ya kumwangusha yule mtu chini, akamtoka bila kumdhuru hata kidogo. And Jesus rebuked him, saying, Hold thy peace, and come out of him. And when the devil had thrown him in the midst, he came out of him, and hurt him not.
36 Watu wote wakashangaa, wakawa wanaambiana, "Hili ni jambo la ajabu, maana kwa uwezo na nguvu anawaamuru pepo wachafu watoke, nao wanatoka!" And they were all amazed, and spake among themselves, saying, What a word is this! for with authority and power he commandeth the unclean spirits, and they come out.
37 Habari zake zikaenea mahali pote katika mkoa ule. And the fame of him went out into every place of the country round about.
38 Yesu alitoka katika lile sunagogi, akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa na homa kali; wakamwomba amponye. And he arose out of the synagogue, and entered into Simon’s house. And Simon’s wife’s mother was taken with a great fever; and they besought him for her.
39 Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia. And he stood over her, and rebuked the fever; and it left her: and immediately she arose and ministered unto them.
40 Jua lilipokuwa linatua, wote waliokuwa na wagonjwa wao mbalimbali waliwaleta kwake; naye akaweka mikono yake juu ya kila mmoja wao, akawaponya wote. Now when the sun was setting, all they that had any sick with divers diseases brought them unto him; and he laid his hands on every one of them, and healed them.
41 Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: "Wewe u Mwana wa Mungu!" Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walimfahamu kwamba yeye ndiye Kristo. And devils also came out of many, crying out, and saying, Thou art Christ the Son of God. And he rebuking them suffered them not to speak: for they knew that he was Christ.
42 Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao. And when it was day, he departed and went into a desert place: and the people sought him, and came unto him, and stayed him, that he should not depart from them.
43 Lakini yeye akawaambia, "Ninapaswa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu katika miji mingine pia, maana nilitumwa kwa ajili hiyo." And he said unto them, I must preach the kingdom of God to other cities also: for therefore am I sent.
44 Akawa anahubiri katika masunagogi ya Yudea. And he preached in the synagogues of Galilee.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL