누가복음 18장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 43절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonyesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa. | And he spake a parable unto them to this end, that men ought always to pray, and not to faint; |
| 2 | Alisema: "Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. | Saying, There was in a city a judge, which feared not God, neither regarded man: |
| 3 | Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane, ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake kutoka kwa adui yake. | And there was a widow in that city; and she came unto him, saying, Avenge me of mine adversary. |
| 4 | Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupenda kumtetea huyo mjane; lakini, mwishowe akajisemea: Ingawa mimi simchi Mungu wala simjali binadamu, | And he would not for a while: but afterward he said within himself, Though I fear not God, nor regard man; |
| 5 | lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua, nitamtetea; la sivyo ataendelea kufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!" | Yet because this widow troubleth me, I will avenge her, lest by her continual coming she weary me. |
| 6 | Basi, Bwana akaendelea kusema, "Sikieni jinsi alivyosema huyo hakimu mbaya. | And the Lord said, Hear what the unjust judge saith. |
| 7 | Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza? | And shall not God avenge his own elect, which cry day and night unto him, though he bear long with them? |
| 8 | Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je, kutakuwako na imani duniani wakati Mwana wa Mtu atakapokuja?" | I tell you that he will avenge them speedily. Nevertheless when the Son of man cometh, shall he find faith on the earth? |
| 9 | Halafu Yesu aliwaambia pia mfano wa wale ambao walijiona kuwa wema na kuwadharau wengine. | And he spake this parable unto certain which trusted in themselves that they were righteous, and despised others: |
| 10 | "Watu wawili walipanda kwenda Hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo, na mwingine mtoza ushuru. | Two men went up into the temple to pray; the one a Pharisee, and the other a publican. |
| 11 | Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtoza ushuru. | The Pharisee stood and prayed thus with himself, God, I thank thee, that I am not as other men are, extortioners, unjust, adulterers, or even as this publican. |
| 12 | Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu. | I fast twice in the week, I give tithes of all that I possess. |
| 13 | Lakini yule mtoza ushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi. | And the publican, standing afar off, would not lift up so much as his eyes unto heaven, but smote upon his breast, saying, God be merciful to me a sinner. |
| 14 | Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa." | I tell you, this man went down to his house justified rather than the other: for every one that exalteth himself shall be abased; and he that humbleth himself shall be exalted. |
| 15 | Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali. | And they brought unto him also infants, that he would touch them: but when his disciples saw it, they rebuked them. |
| 16 | Lakini Yesu akawaita kwake akisema: "Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu kama hawa. | But Jesus called them unto him, and said, Suffer little children to come unto me, and forbid them not: for of such is the kingdom of God. |
| 17 | Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika Ufalme huo." | Verily I say unto you, Whosoever shall not receive the kingdom of God as a little child shall in no wise enter therein. |
| 18 | Kiongozi mmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, "Mwalimu mwema, nifanye nini ili niweze kuupata uzima wa milele?" | And a certain ruler asked him, saying, Good Master, what shall I do to inherit eternal life? |
| 19 | Yesu akamwambia, "Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. | And Jesus said unto him, Why callest thou me good? none is good, save one, that is, God. |
| 20 | Unazijua amri: Usizini; usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo; waheshimu baba yako na mama yako." | Thou knowest the commandments, Do not commit adultery, Do not kill, Do not steal, Do not bear false witness, Honour thy father and thy mother. |
| 21 | Yeye akasema, "Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu." | And he said, All these have I kept from my youth up. |
| 22 | Yesu aliposikia hayo akamwambia, "Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: uza kila ulicho nacho, wagawie maskini, na hivyo utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate." | Now when Jesus heard these things, he said unto him, Yet lackest thou one thing: sell all that thou hast, and distribute unto the poor, and thou shalt have treasure in heaven: and come, follow me. |
| 23 | Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana. | And when he heard this, he was very sorrowful: for he was very rich. |
| 24 | Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, "Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu! | And when Jesus saw that he was very sorrowful, he said, How hardly shall they that have riches enter into the kingdom of God! |
| 25 | Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu." | For it is easier for a camel to go through a needle’s eye, than for a rich man to enter into the kingdom of God. |
| 26 | Wale watu waliposikia hayo, wakasema, "Nani basi, atakayeokolewa?" | And they that heard it said, Who then can be saved? |
| 27 | Yesu akajibu, "Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu." | And he said, The things which are impossible with men are possible with God. |
| 28 | Naye Petro akamwuliza, "Na sisi je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!" | Then Peter said, Lo, we have left all, and followed thee. |
| 29 | Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au kaka au wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, | And he said unto them, Verily I say unto you, There is no man that hath left house, or parents, or brethren, or wife, or children, for the kingdom of God’s sake, |
| 30 | atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na kupokea uzima wa milele wakati ujao." | Who shall not receive manifold more in this present time, and in the world to come life everlasting. |
| 31 | Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, "Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa. | Then he took unto him the twelve, and said unto them, Behold, we go up to Jerusalem, and all things that are written by the prophets concerning the Son of man shall be accomplished. |
| 32 | Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate. | For he shall be delivered unto the Gentiles, and shall be mocked, and spitefully entreated, and spitted on: |
| 33 | Watampiga mijeledi, watamuua; lakini siku ya tatu atafufuka." | And they shall scourge him, and put him to death: and the third day he shall rise again. |
| 34 | Lakini wao hawakuelewa hata kidogo jambo hilo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa. | And they understood none of these things: and this saying was hid from them, neither knew they the things which were spoken. |
| 35 | Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba. | And it came to pass, that as he was come nigh unto Jericho, a certain blind man sat by the way side begging: |
| 36 | Aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, "Kuna nini?" | And hearing the multitude pass by, he asked what it meant. |
| 37 | Wakamwambia, "Yesu wa Nazareti anapita." | And they told him, that Jesus of Nazareth passeth by. |
| 38 | Naye akapaza sauti akisema, "Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!" | And he cried, saying, Jesus, thou Son of David, have mercy on me. |
| 39 | Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: "Mwana wa Daudi, nihurumie;" | And they which went before rebuked him, that he should hold his peace: but he cried so much the more, Thou Son of David, have mercy on me. |
| 40 | Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza, | And Jesus stood, and commanded him to be brought unto him: and when he was come near, he asked him, |
| 41 | "Unataka nikufanyie nini?" Naye akamjibu, "Bwana, naomba nipate kuona tena." | Saying, What wilt thou that I shall do unto thee? And he said, Lord, that I may receive my sight. |
| 42 | Yesu akamwambia, "Ona! Imani yako imekuponya." | And Jesus said unto him, Receive thy sight: thy faith hath saved thee. |
| 43 | Na mara yule aliyekuwa kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu. | And immediately he received his sight, and followed him, glorifying God: and all the people, when they saw it, gave praise unto God. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL