누가복음 13장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 누가복음 (Luke) · 35절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Wakati huo watu fulani walikuja, wakamweleza Yesu juu ya watu wa Galilaya ambao Pilato alikuwa amewaua wakati walipokuwa wanachinja wanyama wao wa tambiko. | There were present at that season some that told him of the Galileans, whose blood Pilate had mingled with their sacrifices. |
| 2 | Naye Yesu akawaambia, "Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo? | And Jesus answering said unto them, Suppose ye that these Galileans were sinners above all the Galileans, because they suffered such things? |
| 3 | Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu, mtaangamia kama wao. | I tell you, Nay: but, except ye repent, ye shall all likewise perish. |
| 4 | Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu? | Or those eighteen, upon whom the tower in Siloam fell, and slew them, think ye that they were sinners above all men that dwelt in Jerusalem? |
| 5 | Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao." | I tell you, Nay: but, except ye repent, ye shall all likewise perish. |
| 6 | Kisha, Yesu akawaambia mfano huu: "Mtu mmoja alikuwa na mtini katika shamba lake. Mtu huyu akaenda akitaka kuchuma matunda yake, lakini akaukuta haujazaa hata tunda moja. | He spake also this parable; A certain man had a fig tree planted in his vineyard; and he came and sought fruit thereon, and found none. |
| 7 | Basi, akamwambia mfanyakazi wake: Angalia! Kwa miaka mitatu nimekuwa nikija kuchuma matunda ya mtini huu, nami nisiambulie kitu. Ukate! Kwa nini uitumie ardhi bure? | Then said he unto the dresser of his vineyard, Behold, these three years I come seeking fruit on this fig tree, and find none: cut it down; why cumbereth it the ground? |
| 8 | Lakini naye akamjibu: Bwana, tuuache tena mwaka huu; nitauzungushia mtaro na kuutilia mbolea. | And he answering said unto him, Lord, let it alone this year also, till I shall dig about it, and dung it: |
| 9 | Kama ukizaa matunda mwaka ujao, vema; la sivyo, basi utaweza kuukata." | And if it bear fruit, well: and if not, then after that thou shalt cut it down. |
| 10 | Yesu alikuwa akifundisha katika sunagogi moja siku ya Sabato. | And he was teaching in one of the synagogues on the sabbath. |
| 11 | Na hapo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa mgonjwa kwa miaka kumi na minane kutokana na pepo aliyekuwa amempagaa. Kwa sababu hiyo, mwili wake ulikuwa umepindika vibaya hata asiweze kusimama wima. | And, behold, there was a woman which had a spirit of infirmity eighteen years, and was bowed together, and could in no wise lift up herself. |
| 12 | Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, "Mama, umeponywa ugonjwa wako." | And when Jesus saw her, he called her to him, and said unto her, Woman, thou art loosed from thine infirmity. |
| 13 | Akamwekea mikono, na mara mwili wake ukawa wima tena, akawa anamtukuza Mungu. | And he laid his hands on her: and immediately she was made straight, and glorified God. |
| 14 | Lakini mkuu wa sunagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo akawaambia wale watu walikusanyika pale, "Mnazo siku sita za kufanya kazi. Basi, fikeni siku hizo mkaponywe magonjwa yenu; lakini msije siku ya Sabato." | And the ruler of the synagogue answered with indignation, because that Jesus had healed on the sabbath day, and said unto the people, There are six days in which men ought to work: in them therefore come and be healed, and not on the sabbath day. |
| 15 | Hapo Bwana akamjibu, "Enyi wanafiki! Nani kati yenu hangemfungua ng'ombe au punda wake kutoka zizini ampeleke kunywa maji, hata kama siku hiyo ni ya Sabato? | The Lord then answered him, and said, Thou hypocrite, doth not each one of you on the sabbath loose his ox or his ass from the stall, and lead him away to watering? |
| 16 | Sasa, hapa yupo binti wa Abrahamu ambaye Shetani alimfanya kilema kwa muda wa miaka kumi na minane. Je, haikuwa vizuri kumfungulia vifungo vyake siku ya Sabato?" | And ought not this woman, being a daughter of Abraham, whom Satan hath bound, lo, these eighteen years, be loosed from this bond on the sabbath day? |
| 17 | Alipokwisha sema hayo, wapinzani wake waliona aibu lakini watu wengine wote wakajaa furaha kwa sababu ya mambo yote aliyotenda. | And when he had said these things, all his adversaries were ashamed: and all the people rejoiced for all the glorious things that were done by him. |
| 18 | Yesu akauliza: "Ufalme wa Mungu unafanana na nini? Nitaulinganisha na nini? | Then said he, Unto what is the kingdom of God like? and whereunto shall I resemble it? |
| 19 | NI kama mbegu ya haradali aliyotwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake; ikaota hata ikawa mti. Ndege wa angani wakajenga viota vyao katika matawi yake." | It is like a grain of mustard seed, which a man took, and cast into his garden; and it grew, and waxed a great tree; and the fowls of the air lodged in the branches of it. |
| 20 | Tena akauliza: "Nitaulinganisha Ufalme wa Mungu na nini? | And again he said, Whereunto shall I liken the kingdom of God? |
| 21 | Ni kama chachu aliyoitwaa mama mmoja na kuichanganya pamoja na unga debe moja kisha unga wote ukaumuka wote." | It is like leaven, which a woman took and hid in three measures of meal, till the whole was leavened. |
| 22 | Yesu alindelea na safari yake kwenda Yerusalemu huku akipitia mijini na vijijini, akihubiri. | And he went through the cities and villages, teaching, and journeying toward Jerusalem. |
| 23 | Mtu mmoja akamwuliza, "Je, Mwalimu, watu watakaookoka ni wachache?" | Then said one unto him, Lord, are there few that be saved? And he said unto them, |
| 24 | Yesu akawaambia, "Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; maana nawaambieni, wengi watajaribu kuingia lakini hawataweza. | Strive to enter in at the strait gate: for many, I say unto you, will seek to enter in, and shall not be able. |
| 25 | "Wakati utakuja ambapo mwenye nyumba atainuka na kufunga mlango. Ninyi mtasimama nje na kuanza kupiga hodi mkisema: Bwana, tufungulie mlango. Lakini yeye atawajibu: Sijui mmetoka wapi. | When once the master of the house is risen up, and hath shut to the door, and ye begin to stand without, and to knock at the door, saying, Lord, Lord, open unto us; and he shall answer and say unto you, I know you not whence ye are: |
| 26 | Nanyi mtaanza kumwambia: Sisi ndio wale tuliokula na kunywa pamoja nawe; na wewe ulifundisha katika vijiji vyetu. | Then shall ye begin to say, We have eaten and drunk in thy presence, and thou hast taught in our streets. |
| 27 | Lakini yeye atasema: Sijui ninyi mmetoka wapi; ondokeni mbele yangu, enyi nyote watenda maovu. | But he shall say, I tell you, I know you not whence ye are; depart from me, all ye workers of iniquity. |
| 28 | Ndipo mtakuwa na kulia na kusaga meno, wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka na Yakobo, na manabii wote wapo katika Ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje! | There shall be weeping and gnashing of teeth, when ye shall see Abraham, and Isaac, and Jacob, and all the prophets, in the kingdom of God, and you yourselves thrust out. |
| 29 | Watu watakuja kutoka mashariki na magharibi, kutoka kaskazini na kusini, watakuja na kukaa kwenye karamu katika Ufalme wa Mungu. | And they shall come from the east, and from the west, and from the north, and from the south, and shall sit down in the kingdom of God. |
| 30 | Naam, wale walio wa mwisho watakuwa wa kwanza; na wale walio wa kwanza watakuwa wa mwisho." | And, behold, there are last which shall be first, and there are first which shall be last. |
| 31 | Wakati huohuo, Mafarisayo na watu wengine walimwendea Yesu wakamwambia, "Ondoka hapa uende mahali pengine, kwa maana Herode anataka kukuua." | The same day there came certain of the Pharisees, saying unto him, Get thee out, and depart hence: for Herod will kill thee. |
| 32 | Yesu akawajibu, "Nendeni mkamwambie huyo mbweha hivi: Leo na kesho ninafukuza pepo na kuponya wagonjwa, na siku ya tatu nitakamilisha kazi yangu. | And he said unto them, Go ye, and tell that fox, Behold, I cast out devils, and I do cures to day and to morrow, and the third day I shall be perfected. |
| 33 | Hata hivyo, kwa leo, kesho na kesho kutwa, ni lazima niendelee na safari yangu, kwa sababu si sawa nabii auawe nje ya Yerusalemu. | Nevertheless I must walk to day, and to morrow, and the day following: for it cannot be that a prophet perish out of Jerusalem. |
| 34 | "Yerusalemu! We Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako pamoja kama kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, Lakini wewe umekataa. | O Jerusalem, Jerusalem, which killest the prophets, and stonest them that are sent unto thee; how often would I have gathered thy children together, as a hen doth gather her brood under her wings, and ye would not! |
| 35 | Haya, utaachiwa mwenyewe nyumba yako. Naam, hakika nawaambieni, hamtaniona mpaka wakati utakapofika mseme: Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana." | Behold, your house is left unto you desolate: and verily I say unto you, Ye shall not see me, until the time come when ye shall say, Blessed is he that cometh in the name of the Lord. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL