골로새서 4장 Swahili
Swahili · 스와힐리어 · 골로새서 (Colossians) · 18절 · 대역: King James Version
| 절 | Swahili | King James Version |
|---|---|---|
| 1 | Nanyi wakuu, watendeeni watumwa wenu kwa uadilifu na haki, mkikumbuka kwamba nanyi pia mnaye Bwana mbinguni. | Masters, give unto your servants that which is just and equal; knowing that ye also have a Master in heaven. |
| 2 | Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu. | Continue in prayer, and watch in the same with thanksgiving; |
| 3 | Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni. | Withal praying also for us, that God would open unto us a door of utterance, to speak the mystery of Christ, for which I am also in bonds: |
| 4 | Basi, ombeni ili niweze kusema kama inavyonipasa na kwa namna itakayodhihirisha siri hiyo. | That I may make it manifest, as I ought to speak. |
| 5 | Muwe na hekima katika uhusiano wenu na watu wasioamini, mkitumia vizuri kila nafasi mliyo nayo. | Walk in wisdom toward them that are without, redeeming the time. |
| 6 | Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja. | Let your speech be alway with grace, seasoned with salt, that ye may know how ye ought to answer every man. |
| 7 | Ndugu yetu mpenzi Tukiko, mfanyakazi mwaminifu na mtumishi mwenzetu katika kazi ya Bwana, atawapeni habari zangu zote. | All my state shall Tychicus declare unto you, who is a beloved brother, and a faithful minister and fellowservant in the Lord: |
| 8 | Ndiyo maana namtuma, ili aichangamshe mioyo yenu kwa kuwaambieni habari zetu. | Whom I have sent unto you for the same purpose, that he might know your estate, and comfort your hearts; |
| 9 | Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpenzi na mwaminifu, ambaye ni mwananchi mwenzenu. Watawapeni habari za mambo yote yanayofanyika hapa. | With Onesimus, a faithful and beloved brother, who is one of you. They shall make known unto you all things which are done here. |
| 10 | Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni). | Aristarchus my fellowprisoner saluteth you, and Marcus, sister’s son to Barnabas, (touching whom ye received commandments: if he come unto you, receive him;) |
| 11 | Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya Utawala wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu. | And Jesus, which is called Justus, who are of the circumcision. These only are my fellowworkers unto the kingdom of God, which have been a comfort unto me. |
| 12 | Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu anawasalimuni. Daima anawaombeeni ninyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu. | Epaphras, who is one of you, a servant of Christ, saluteth you, always labouring fervently for you in prayers, that ye may stand perfect and complete in all the will of God. |
| 13 | Naweza kushuhudia kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu na kwa ajili ya watu wa Laodikea na Hierapoli. | For I bear him record, that he hath a great zeal for you, and them that are in Laodicea, and them in Hierapolis. |
| 14 | Luka, daktari wetu mpenzi, na Dema, wanawasalimuni. | Luke, the beloved physician, and Demas, greet you. |
| 15 | Salamu zetu kwa ndugu zetu wa Laodikea; msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake. | Salute the brethren which are in Laodicea, and Nymphas, and the church which is in his house. |
| 16 | Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na ninyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata kwao. | And when this epistle is read among you, cause that it be read also in the church of the Laodiceans; and that ye likewise read the epistle from Laodicea. |
| 17 | Mwambieni Arkipo aitekeleze vizuri ile huduma aliyokabidhiwa na Bwana. | And say to Archippus, Take heed to the ministry which thou hast received in the Lord, that thou fulfil it. |
| 18 | Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi. | The salutation by the hand of me Paul. Remember my bonds. Grace be with you. Amen. Written from Rome to the Colossians by Tychicus and Onesimus. |
Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL