로그인

고린도전서 12장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 고린도전서 (1 Corinthians) · 31절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya: Now concerning spiritual gifts, brethren, I would not have you ignorant.
2 Mnajua kwamba, kabla ya kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa na sanamu tupu. Ye know that ye were Gentiles, carried away unto these dumb idols, even as ye were led.
3 Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema: "Yesu alaaniwe!" Hali kadhalika, mtu yeyote hawezi kusema: "Yesu ni Bwana," asipoongozwa na Roho Mtakatifu. Wherefore I give you to understand, that no man speaking by the Spirit of God calleth Jesus accursed: and that no man can say that Jesus is the Lord, but by the Holy Ghost.
4 Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja. Now there are diversities of gifts, but the same Spirit.
5 Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja. And there are differences of administrations, but the same Lord.
6 Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote. And there are diversities of operations, but it is the same God which worketh all in all.
7 Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote. But the manifestation of the Spirit is given to every man to profit withal.
8 Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu apendavyo Roho huyohuyo. For to one is given by the Spirit the word of wisdom; to another the word of knowledge by the same Spirit;
9 Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha kuponya; To another faith by the same Spirit; to another the gifts of healing by the same Spirit;
10 humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua. To another the working of miracles; to another prophecy; to another discerning of spirits; to another divers kinds of tongues; to another the interpretation of tongues:
11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe. But all these worketh that one and the selfsame Spirit, dividing to every man severally as he will.
12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote--ingawaje ni vingi--hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo. For as the body is one, and hath many members, and all the members of that one body, being many, are one body: so also is Christ.
13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja. For by one Spirit are we all baptized into one body, whether we be Jews or Gentiles, whether we be bond or free; and have been all made to drink into one Spirit.
14 Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi. For the body is not one member, but many.
15 Kama mguu ungejisemea: "Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili", je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha! If the foot shall say, Because I am not the hand, I am not of the body; is it therefore not of the body?
16 Kama sikio lingejisemea: "Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili", je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La! And if the ear shall say, Because I am not the eye, I am not of the body; is it therefore not of the body?
17 Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa? If the whole body were an eye, where were the hearing? If the whole were hearing, where were the smelling?
18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda. But now hath God set the members every one of them in the body, as it hath pleased him.
19 Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? And if they were all one member, where were the body?
20 Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja. But now are they many members, yet but one body.
21 Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: "Sikuhitaji wewe", wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: "Siwahitaji ninyi." And the eye cannot say unto the hand, I have no need of thee: nor again the head to the feet, I have no need of you.
22 Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi. Nay, much more those members of the body, which seem to be more feeble, are necessary:
23 Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi, And those members of the body, which we think to be less honourable, upon these we bestow more abundant honour; and our uncomely parts have more abundant comeliness.
24 ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima, For our comely parts have no need: but God hath tempered the body together, having given more abundant honour to that part which lacked:
25 ili kusiweko na utengano katika mwili bali viungo vyote vishughulikiane. That there should be no schism in the body; but that the members should have the same care one for another.
26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho. And whether one member suffer, all the members suffer with it; or one member be honoured, all the members rejoice with it.
27 Basi, ninyi nyote ni mwili wa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwili huo. Now ye are the body of Christ, and members in particular.
28 Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni. And God hath set some in the church, first apostles, secondarily prophets, thirdly teachers, after that miracles, then gifts of healings, helps, governments, diversities of tongues.
29 Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza? Are all apostles? are all prophets? are all teachers? are all workers of miracles?
30 Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha? Have all the gifts of healing? do all speak with tongues? do all interpret?
31 Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote. But covet earnestly the best gifts: and yet shew I unto you a more excellent way.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL