로그인

갈라디아서 1장 Swahili

Swahili · 스와힐리어 · 갈라디아서 (Galatians) · 24절 · 대역: King James Version

절SwahiliKing James Version
1 Mimi Paulo mtume, Paul, an apostle, (not of men, neither by man, but by Jesus Christ, and God the Father, who raised him from the dead;)
2 na ndugu wote walio pamoja nami, tunayaandikia makanisa yaliyoko Galatia. Mimi nimepata kuwa mtume si kutokana na mamlaka ya binadamu, wala si kwa nguvu ya mtu, bali kwa uwezo wa Yesu Kristo na wa Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka wafu. And all the brethren which are with me, unto the churches of Galatia:
3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Grace be to you and peace from God the Father, and from our Lord Jesus Christ,
4 Kristo alijitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba, ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu mbaya wa sasa. Who gave himself for our sins, that he might deliver us from this present evil world, according to the will of God and our Father:
5 Kwake yeye uwe utukufu milele! Amina. To whom be glory for ever and ever. Amen.
6 Nashangaa kwamba muda mfupi tu umepita, nanyi mnamwasi yule aliyewaita kwa neema ya Kristo, mkafuata Habari Njema ya namna nyingine. I marvel that ye are so soon removed from him that called you into the grace of Christ unto another gospel:
7 Lakini hakuna "Habari Njema" nyingine. Ukweli ni kwamba wako watu wanaowavurugeni, watu wanaotaka kuipotosha Habari Njema ya Kristo. Which is not another; but there be some that trouble you, and would pervert the gospel of Christ.
8 Lakini, hata kama mmoja wetu au malaika kutoka mbinguni, atawahubirieni Habari Njema tofauti na ile tuliyowahubirieni sisi, basi huyo na alaaniwe! But though we, or an angel from heaven, preach any other gospel unto you than that which we have preached unto you, let him be accursed.
9 Tulikwisha sema, na sasa nasema tena: kama mtu yeyote anawahubirieni Habari Njema ya aina nyingine, tofauti na ile mliyokwisha pokea, huyo na alaaniwe! As we said before, so say I now again, If any man preach any other gospel unto you than that ye have received, let him be accursed.
10 Sasa nataka kibali cha nani: cha binadamu, ama cha Mungu? Au je, nataka kuwapendeza watu? Kama ningefanya hivyo, mimi singekuwa kamwe mtumishi wa Kristo. For do I now persuade men, or God? or do I seek to please men? for if I yet pleased men, I should not be the servant of Christ.
11 Ndugu, napenda mfahamu kwamba ile Habari Njema niliyoihubiri si ujumbe wa kibinadamu. But I certify you, brethren, that the gospel which was preached of me is not after man.
12 Wala mimi sikuipokea kutoka kwa binadamu, wala sikufundishwa na mtu. Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyenifunulia. For I neither received it of man, neither was I taught it, but by the revelation of Jesus Christ.
13 Bila shaka mlikwisha sikia jinsi nilivyokuwa ninaishi zamani kwa kuzingatia dini ya Kiyahudi, na jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kupita kiasi na kutaka kuliharibu kabisa. For ye have heard of my conversation in time past in the Jews’ religion, how that beyond measure I persecuted the church of God, and wasted it:
14 Naam, mimi niliwashinda wengi wa wananchi wenzangu wa rika langu katika kuizingatia dini ya Kiyahudi, nikajitahidi sana kuyashika mapokeo ya wazee wetu. And profited in the Jews’ religion above many my equals in mine own nation, being more exceedingly zealous of the traditions of my fathers.
15 Lakini Mungu, kwa neema yake, alikuwa ameniteua hata kabla sijazaliwa, akaniita nimtumikie. But when it pleased God, who separated me from my mother’s womb, and called me by his grace,
16 Mara tu alipoamua kunifunulia Mwanae kusudi niihubiri Habari Njema yake kwa watu wa mataifa mengine, bila kutafuta maoni ya binadamu, To reveal his Son in me, that I might preach him among the heathen; immediately I conferred not with flesh and blood:
17 na bila kwenda kwanza Yerusalemu kwa wale waliopata kuwa mitume kabla yangu, nilikwenda kwanza Arabia, kisha nikarudi tena Damasko. Neither went I up to Jerusalem to them which were apostles before me; but I went into Arabia, and returned again unto Damascus.
18 Ilikuwa tu baada ya miaka mitatu, ndipo nilipokwenda Yerusalemu kuonana na Kefa; nilikaa kwake siku kumi na tano. Then after three years I went up to Jerusalem to see Peter, and abode with him fifteen days.
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. But other of the apostles saw I none, save James the Lord’s brother.
20 Haya ninayowaandikieni, Mungu anajua; sisemi uongo. Now the things which I write unto you, behold, before God, I lie not.
21 Baadaye nilikwenda katika tarafa za Siria na Kilikia. Afterwards I came into the regions of Syria and Cilicia;
22 Wakati huo, mimi binafsi sikujulikana kwa jumuiya za Wakristo kule Yudea. And was unknown by face unto the churches of Judea which were in Christ:
23 Walichokuwa wanajua ni kile tu walichosikia: "Mtu yule aliyekuwa akitutesa hapo awali, sasa anaihubiri imani ileile aliyokuwa anajaribu kuiangamiza." But they had heard only, That he which persecuted us in times past now preacheth the faith which once he destroyed.
24 Basi, wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu. And they glorified God in me.

Swahili — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: 공개 도메인 (Public Domain)
King James Version — getbible.net(CrossWire SWORD 모듈)에서 가져옴 · 라이선스: GPL